Mpenzi wangu ameondoka na mtoto mchanga

Naomba ushauri wa kweli, hata kama utakuwa mchungu. Sitafuti watu wa kunifariji tu; natafuta mitazamo tofauti ili nifanye uamuzi sahihi kuhusu maisha yangu na mustakabali wa mtoto wangu.
Good mimi nitakushauri ila ushauri wangu sio sheria

Binafsi nimewahi pia kutokuelewana na manzi fulani hivi issue ikawa km hivyo ilichukua km wiki tuna sort out mpaka yakaisha, mimi nilitumia tu ujanja wa kuzaliwa sio kingine inabidi akili yako iwe inachaji kumzidi yeye akikuzidi akili humuwezi, mwanamke anapenda mwanaume kiongozi anaemwongoza.

Lakini hua wanasema kitu kimoja niliwahi elekezwa km mwanaume ukiwa jeshini unafundishwa unapoenda kwenye uwanja wa vita usitumie vile tu ulivyofundishwa inabidi ujiongeze kwa kutumia ujanja wa porini ili uweze ku-survive.

Sasa suala km hilo limekukuta inabidi ujiongezee na ujanja wako wa kuweza kum-convince yeye asahau yaliyotokea. Issue ni kwamba unam-convince vipi? Hapo ni wewe na akili yako ndio maana Bible ikasema ishini nao kwa akili.

Kuna mbinu nyingi za kufanya suala hilo liishe na mbinu moja wapo ni kumkutanisha yeye na huyo manzi uliemnyonya mate kwenye camera, mzungumze wote kwa pamoja ili muyamalize wote kwa pamoja. Hii ni mbinu ngumu ila inawezekana kabisa ukiamua.

Narudia tena lazima utumie ujanja wa porini hata km utaonekana wewe ni mporipori haupo kimjini potelea pote ilimradi ya kwako yanakuendea na hicho ndicho huyo manzi alikua anakitaka kumthibitishia kwamba ni yeye pekee ndie unaempenda (kitu ambacho sio kweli) ila km mwanaume lazima uwe mjanja kumuhakikishia hata kwa kumdanganya kwa kutumia uongo wenye faida na manufaa kwako na kwake ili mjenge familia na kulea mtoto pamoja.

Kitu kingine huyo anachohitaji ni mapumziko yaan apate short break awe mbali na wewe kwa hio kuondoka haina maana kwamba mmeachana au hakupendi ila ameenda kupumzika.

Kikubwa unachotakiwa kufanya usipanic sana yaan manzi umeweza kumgonga ukaweza kumtia mimba ukaweza kulea mimba mpaka mtoto amezaliwa unapanic nini mwanaume?

Angalia wapi pa kuanzia ikiwezekana mfuate alipo zungumza nae ana kwa ana tumia akili zako zote ulizotumia kumtongoza lazima akae kwenye mfumo na atafungasha mabegi na kurudi.

Nitakufundisha tactic moja ya muhimu sana inaitwa counter-pressing hii inakuaje? Huyo manzi yeye si anagoma na ameondoka? Anataka umfanyie kitu kinaitwa counter-pressing.

Basi ngoja nitumie mfano rahisi sana umewahi bonyeza switch ukaona bulb haiwaki?, hivi ukibonyeza mara moja ukaona bulb haiwaki unaacha au unabonyeza tena switch ili uone ni umeme umezima au umekatika, luku imeisha au kuna hitilafu ya umeme au bulb imeungua au waya umeliwa na panya au circuit breaker imejizima kuzuia moto usiwake kwa hio umeme haufiki kwenye bulb?

Sasa hio ndio ninaiita counter-pressing itabidi uanze kubonyeza switch mara ya kwanza kisha uone bulb inawaka ukiona haiwaki angalia switch nyingi kuhakiki km bulb nyingine zinawaka, ukiona zinawaka basi tatizo litakua ni upande huo wa bulb yako kuanzia kwenye switch, waya, circuit breaker hadi kwenye bulb yenyewe.

Swali; unaanzia wapi?

Unaanzia kwenye switch, waya, circuit breaker au kwenye bulb (mpenzi wako mama watoto)?

Utafanya counter-pressing kwa sababu wewe hautaki kupoteza huu mchezo unaoitwa mapenzi kwa hio press the button look at the problem first kuanzia kwenye switch mpaka kwenye bulb (huyu ni mkeo).

Baada ya hapo angalia ulikosea wapi shida ni nini kwanini bulb haiwaki fungua circuit breaker angalia labda imejizima kuzuia moto usiwake kwa sababu kulikua na short circuit.

Natumia umeme kukuelewesha ili ujue ni nini kimetokea, hapo wewe unashindwa kuelewana na yeye sababu wewe ukiwa km switch haupati muunganiko na yeye akiwa km bulb sababu umeme haufiki kwake yeye.

Kwa hio unachotakiwa kufanya ni kubonye switch zaidi ya mara 3 kabla ya kuangalia km tatizo ni switch mbovu imeungua inabidi ubadirishe uweke switch mpya au la uone kwamba waya una shida umeliwa na panya kwa hio hakuna mawasiliano kati ya switch na bulb au la bulb imeungua kwa hio haifai tena kwa matumizi.

Sasa basi kwa sababu switch (wewe) ni nzima na bulb (yeye) ni nzima, km ukipress km ulivyofanya ila bulb ikawa haiwaki rudi uangalie je waya na circuit breaker haina shida, sasa hapa ndio hapo kwenye kusuluhisha tatizo nilipokwambia muite yeye muweke chini muite hio manzi uliyoipiga mate na wewe mkae chini mzungumze maana kilichotokea sio kwamba bulb mbovu ila circuit breaker imejizima, kwa hio unachotakiwa kufanya ni kuipandisha circuit breaker isome ON sio OFF.

Akili, hao viumbe wanataka uishi nao kwa akili. Jumlisha na ujanja wako wa kuzaliwa.

Nimeeleza kwa kadri nivyoweza kukuelewesha km haujaelewa au unaona mbinu hii ni ngumu basi kuna data utakua haujaziweka wazi ume-play victim ikiwa ya kwamba wewe ndio mwenye makosa ya wazi.

Km wewe ndio mwenye makosa ya wazi hata ukitumia hio counter-pressing haitosaidi.

Elewa neno makosa sio kosa ni makosa mengi yanaongozana leo hilo kesho lile na kuendelea yanafuatana pamoja na huchoki kukosea kila siku unakosea wewe tu mpaka mtu anachoka anasema eeh imetosha sasa ngoja niondoke zangu huyoo anapaa anakuacha mwenyewe. Kwanini? Kwa sababu wewe hauchoki kumkosea.

Ila km ni kosa hilo tu tumia hio counter-pressing umemaliza kesi. Press hio button Buddha.

NB: Counter-pressing is the immediate, coordinated attempt to win the ball back seconds after losing it.
 
Japokuwa yote umeyataka mwenyewe,
Kutoweka mipaka na wanawake wengine

Lakini ushauri wangu ni huu ,

Kuhusu mtoto usiwaze ataishi vipi ata yeye hajaondoka kwa kukurupuka wakati bado mjamzito inaonekana halishakuwa amepanga mkakati wote.

Chakufanya wewe usimtafute wala usitake kujua habari za mtoto
Ukiendelea kumtafuta ndiyo hutampata kabisa .

Endelea na mishe zako za kutafuta pesa huyo mwanamke atarudi mwenyewe , kwani sahizi soko la single mother ni gumu mno.

Lakini pia uache ujinga

Akirudi ukajitambulishe kwao na dini akikisha yeye ndiyo ana fata dini yako.
 
Nenda nyumbani kwao ukaongee na wazazi wake, itamfanya aone kweli unampenda na kumhitaji japo ulimsaliti.

Usijali kwamba hukujitambulisha rasmi.
Unataka mwenzio aonekane jambazi
Mwizi kajipeleka polisi,je atawezwa kuonelewa huruma
1. Moja umemzalisha mtoto wao bila hata kujitambulisha wala kutoa mahari
2. Ume cheat unazani unaweza kutoka salama hapo mtu
 
Mwanamke huwa hasemi tuachane kama hana pa kwenda au hana mtu , kama amekwambia muachane mara kwa mara huyo hatanii? Muache aende zake baada ya muda atakutafuta , kwa sasa usihangaike nae
 
Huyo kwao wamemwambia arudi nyumbani au ni kichaa cha uzazi kimepanda, wewe relax hata mwezi bila kumtafuta ukiona na yeye kakaa kimya mwezi mzima endelea na mambo yako.
 
Umetenda kosa la usaliti ambalo hua halisameheki,
People don't cheat by chance,they cheat by choice,

Mwanamke hua hasahau hata siku moja,atakwambia yameisha ila kiukweli hayajaisha,msaliti hua haaminiwi hata siku moja,huyo Mwanamke ameona kwanini aishi kwa kujitesa na mtu asiye muamini tena?
ndio maana kaondoka,

Ushauri wangu,kama huyo mtoto ni wako,basi usiache kumuhudumia coz huo ni wajibu wako,
Kuhusu huyo Mwanamke,usimfuatilie sana au kumuomba msamaha kila siku,endelea na maisha yako kama kawaida,
Huyo Mwanamke itafika kipindi,yeye ndie atakaye kutafuta,ila binafsi sioni future yeyote hapo coz huyo Mwanamke hatokuamini tena wala kua na imani na wewe tena.
 
Wanasemaga poteza ndo ujue thamani ya kitu..nilikuwa nadhani mimi ni strong sana hila ili alilofanya limeniumiza sana..na its okay watu wakiniona kama mzembe au mlaini..
 
Wewe ni NI SHEMALE? mwenye uume maana umenichanganya hapo mwenzio alikua na ujauzito wa miezi 7 alafu na wewe unabusiana na mwanamke mwenzio
 
Mbali na hayo yoote kama mleta mada hana makando kando mengine huyo dada aliyeondoka kuna haya ✌
 
Kwanza nakuchana ukweli.

1. Mwanamke kaona hapo hakuna future na kakaa na wewe kashapiga hesabu hakuna lolote hapo ni kupoteza muda

2. Hata kazi unayofanya inaonekana ni ya kupata hela ya kula na kuvaa tu, kwa hiyo bro dada kaona harufu ya njaa.

3. Huna akili, usaliti unaanza kwenye penzi jipya je ukifikisha miaka 20 ya ndoa si utatembea mpaka na mbuzi wako kama ukibahatika kufuga!!! yaani penzi jipya mtoto wa kwanza unaleta uchafu!!!! halafu utabemenda hako katoto bure msingizie wachawi.

4. Mwanamke huwa hasamehi usaliti, na ukiona umesaliti na umesamehewa mnaishi jua hiyo unatengenezewa revenge.

NB; huyo mwanamke kama yuko jf aje pm yangu nimfundishe tukutengenezee kisukari chako taratibuuu!!! hicho ki abdala kichwa wazi chako kinachofanya ubusu ovyo wanawake kiache kudinda utulie uhamie kwa manabii wa uongo wazitafune hela zako ili mpaka unafukiwa historia yako ya mali iwe fupi na usiache ugomvi.
 
Wanasemaga poteza ndo ujue thamani ya kitu..nilikuwa nadhani mimi ni strong sana hila ili alilofanya limeniumiza sana..na its okay watu wakiniona kama mzembe au mlaini..
Haya punguza malalamiko humu vaa ujasili enda kwao kama ni kutuma washenga/wazee kwa mila zao&za kwenu fuata taratibu umuoe kwanza kakuvumilia na ujinga kaufanya kawakosea wazazi heshima kuishi na wewe hadi anazaa kwao hawakutambui na bado unacheat unataka aendelee kubeba maumivu yote yale akikuvumilia! Fanya fasta kabla hawajakaa sawa na ba mtoto wake😝
 
Kuna asilimia nyingi huyo MTOTO SIO WAKO sasa ame ondoka na kumpeleka kwa baba halisi wa mtoto.
 
Ingekua huyo Mwanamke ndio amecheat na mleta mada akaamua kumuacha,basi angeanzisha uzi humu wa kujisifia,

Cheating harms both men and woman,tearing down trust,destroying emotional safety and often ending committed relationship,

Mleta mada anavuna alicho kipanda.
 
kabisa,
ila nyie wanaume huwa mnajisifu kuwa tunasamehe.

Usaliti hasa kwenye ndoa ni kitu kibaya sana kinaleta dosari kubwa isiyofutika na kupitia usaliti mambo mengi na migogoro visasi vinaanzia hapo.
 
kabisa,
ila nyie wanaume huwa mnajisifu kuwa tunasamehe.

Usaliti hasa kwenye ndoa ni kitu kibaya sana kinaleta dosari kubwa isiyofutika na kupitia usaliti mambo mengi na migogoro visasi vinaanzia hapo.
Hapo kwenye Wanaume weka Wavulana,
wanaume tunaelewa kua usaliti hua hausameheki wala hausahauliki,na ndio nilichokiongea kwenye comment yangu # 26
 
Duuuuuuh wewe ni Nesi?
 
Hapo kwenye Wanaume weka Wavulana,
wanaume tunaelewa kua usaliti hua hausameheki wala hausahauliki,na ndio nilichokiongea kwenye comment yangu # 26
Sawa sawa bwana ice,
hivi na uko ma mbelez wanaume wana akili kama za wanaume wetu wa huku gizani????
 
Duuuuuuh wewe ni Nesi?
Huo unesi nautoa wapi?? kwa akili hizi biology, chemistry na physics nilipata sifuri kabisa. hata huyo msahihishaji alivumilia sana kusahihisha mpaka kuniandikia hiyo sifuri.

Sema mi nahuhudhuria sana vikao sina dharau na wamama walio nizidi umri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…