Mpenzi wangu ananiangalia kwa jicho la ukali kweli

Mpenzi wangu ananiangalia kwa jicho la ukali kweli

Equation x

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2017
Posts
33,679
Reaction score
49,841
Huyu mpenzi wangu simuelewi kabisa, tangu mchana leo amekuwa mkali kweli na ananiangalia kwa jicho la hasira.

Na ameanza kubadilika baada ya kuniona nakula nazi mbichi tatu, mihogo mibichi sita, na sasa namalizia karanga mbichi sado moja.

Sasa sijui, hapendi nile vitu vya asili; au anataka nile vyakula vya viwandani tu?

Wakuu nisaidieni, kwa nini amebadilika hivi, tatizo linaweza kuwa nini?​
 
Back
Top Bottom