Mpenzi wangu anapenda kutumia lugha ngumu

Mpenzi wangu anapenda kutumia lugha ngumu

Wala hata sikufuata tendo. Nilikua nampenda tu. Yan imagine, mimi nasoma Dar yeye yuko Tabora na makaz ni Dar, ila akifunga chuo mimi ndio natika Dar kwenda Tabora nimsindike kurud Dar.. 😂😂.
Mapenzi ni ya kifala sanaaa.
Nilikuaga sina akil sijui.??!!!

Maana nikikumbuka niliokua nayafanya those 10 yrs ago, kwakwel nabak najicheka sana
Yap ni mapenzi yalikuwa ,mwenzio nishasafiri kutoka Dar mpaka Bukoba sehemu inaitwa Rwamishenye kumfuata dada mmoja alikuwa nesi mtaa huo alafu nikamkuta na linjemba kwake ,akanitambulisha Kama mdogo wake ,😃😃, kwa Mara ya Kwanza nililila kisa penzi ,safari ya kurudi Dar nilikuwa natamani nijitupe kwenye lami nife .

Ila ushujaa wa moyo niksurvive nasasa naishi .
Ukweli mapenzi ni upofu ,hako kanesi Sasa hivi nikikaona najicheka kuwa pale nilipenda nini ?
 
Baada ya kujitunza kwa muda mrefu (mashallah),takribani week 3 zilizopita nikampata kijana mmoja tall, handsome, then black (Mungu anajua kumbaa mashallah) baada ya kunitaka kwa kipindi kirefu basi na Mimi nikaamua kum-bless moyo wangu na ye akanibless Wa kwake.

Binafsi nampenda sana na hii ni baada ya yeye kuonesha Kila dalili iliyo nzuri juu yangu.

Lakini tatizo lake ni Moja ana lugha ngumu, yani akiongea na Mimi utadhani anaoengea na msela nwenzake, mara utasikia ananiita majina magumu ukilinganisha na jinsia yangu na status yangu, majina kama jembe, jeshi, kamanda, ndo majina yangu siku hizi, licha ya mm kumuita romantic names ila yy harespond in a good way.

Binafsi sifurahii hali hii hata sjui nifanyeje Kuna muda nawaza ndo ataongea hivi na ba mkwe wake hivi🤔Mfano angalia mazungumzo ya simu baina yetu muda mfupi uliopita

(simu inaita)..
YEYE: Oy oy
MIMI: yes babe nambie
YEYE: kama Kawa?
MIMI: Fresh kabisa
YEYE: Pande zip?
MIMI: Nipo home kwa sasa ila nataka kutoka mara Moja.
YEYE: unaenda wapi?
MIMI:Naelekea ofisini mara Moja nimesahau PC
YEYE: ok, Sema nini mwanangu usikawie kurudi,Nina ubao kinyama, naomba unitolee kitu cha Dona natimba hapo Soon
MIMI: poa usijali
YEYE:Nakubali..

(Nilivorudi nikapika tukala halafu Akala Tena)
Ova.
Mfungie 3 kavu awe romantic
 
Kwa kiasi tu mfano siwezi kumwita mpenzi wangu "mwanangu", ni marafiki ndio tunaitana ivyo ila hayo maneno mengine kama natimba, kitu cha dona, ubao, kinyama/kinoma nayatumia tu hata kwa mpenzi
Mwenzio Naitwa jeshi wakati hata depol Sjawahi timba.
 
Back
Top Bottom