Mpenzi wangu anatumia muda mwingi sana ku-chat na ex wake, na kila nikimuuliza anasema ni mazoea tu!

Mpenzi wangu anatumia muda mwingi sana ku-chat na ex wake, na kila nikimuuliza anasema ni mazoea tu!

Wewe ni Mwanaume au Mwanamke? una Miaka mingapi? kwa kifupi achana tu na huyo Mpenzi wako hakupendi utapata mwingine.
 
Unakwama sana kijana.... Shida ni nini udomo zege au huna pesa daah nchoka mimi
 
Wakuu

Moyo wangu unaumia sana, naona kama unavuja damu kutokana na maumivu ninayoyapitia karibu kila siku.

Mpenzi wangu anatumia muda mwingi sana ku-chat na ex wake, na kila nikimuuliza anasema ni mazoea tu, hakuna kinachoendelea. Nilijaribu kujidanganya, nikajifanya niko sawa, lakini moyoni kulikuwa na kelele za maumivu yasiyoisha.

Kila notification ikilia, tabasamu lake lilinifanya nijisikie mgeni kwenye uhusiano wangu mwenyewe. Nilianza kujiuliza kama ni walishaachana, kwa nini bado ana nafasi kubwa kwenye penzi letu?

Siku moja nilikaa kimya, nikachagua kusikiliza zaidi kuliko kuuliza. Niliona jinsi anavyocheka, jinsi anavyopotea kwenye mazungumzo yao. Hapo ndipo niligundua kuwa si mazungumzo yakawaida, yaliniuma sana.

Nilimkalia chini na kusema kwa utulivu, ‘Sipigani na ex wako, napigania heshima na nafasi yangu.’
Alikaa kimya. Na kwenye ule ukimya, nilijua ama mahusiano yetu yameisha muda.

Naomba ushauri wako, nifanye nini kuhusu mkasa huu, kwani bado nampenda sana na nilikuwa na ndoto kubwa sana na huyu mpenzi wangu.
Wewe naweeeee! Wa kwangu nilikuta picha kwenye profile ya dogo ameweka mtu anayefanana naye kidogo kumbe ni mwanamziki wa Marekani sijui Anaitwa nani vile? Nitam-search, na kweli dogo wanafanana wakisimama hapa unaweza kukubali kwamba ni babake! Na kule shuleni kwao kumbe walikuwa wanamwita hivyo! Kwa vile mimi nilikuwa simfahamu huyo mwanamziki naliuliza mara moja tu kwa sauti kubwa! Mama mtu alilia sana mpaka nikamhurumia! Dawa ya huyo kama huwezi kumwacha kwa amani, na wewe anza kuongea na X wako tena kwa sauti kubwa mwe ngoma sare sare maua!
 
Back
Top Bottom