Mpenzi wangu anatumia muda mwingi sana ku-chat na ex wake, na kila nikimuuliza anasema ni mazoea tu!

Mpenzi wangu anatumia muda mwingi sana ku-chat na ex wake, na kila nikimuuliza anasema ni mazoea tu!

Wakuu

Moyo wangu unaumia sana, naona kama unavuja damu kutokana na maumivu ninayoyapitia karibu kila siku.

Mpenzi wangu anatumia muda mwingi sana ku-chat na ex wake, na kila nikimuuliza anasema ni mazoea tu, hakuna kinachoendelea. Nilijaribu kujidanganya, nikajifanya niko sawa, lakini moyoni kulikuwa na kelele za maumivu yasiyoisha.

Kila notification ikilia, tabasamu lake lilinifanya nijisikie mgeni kwenye uhusiano wangu mwenyewe. Nilianza kujiuliza kama ni walishaachana, kwa nini bado ana nafasi kubwa kwenye penzi letu?

Siku moja nilikaa kimya, nikachagua kusikiliza zaidi kuliko kuuliza. Niliona jinsi anavyocheka, jinsi anavyopotea kwenye mazungumzo yao. Hapo ndipo niligundua kuwa si mazungumzo yakawaida, yaliniuma sana.

Nilimkalia chini na kusema kwa utulivu, ‘Sipigani na ex wako, napigania heshima na nafasi yangu.’
Alikaa kimya. Na kwenye ule ukimya, nilijua ama mahusiano yetu yameisha muda.

Naomba ushauri wako, nifanye nini kuhusu mkasa huu, kwani bado nampenda sana na nilikuwa na ndoto kubwa sana na huyu mpenzi wangu.
Nawe fake kama huna ex uanze kufanya kama afanyavyo uone. Nadhani anaomba muachane kistaarabu tu mwanangu
 
  • Hapo umesha achwa kitambo. jibu unalo
  • Na hawezi kurudi kama zaman.
  • Amekuona umepelea mahari.
  • Afu amekudharau anakuweza tiari. Atawezaje kuchat na mwamba mbele yako? aseeee mim navunja simu.

HUYO MPENZI MFANYE TU AWE EX WAKO PIA, BAADAE ATAKUKUMBUKA NAWEWE.
Yaan kufika akachart na mtu wake mbele yako amekuchoka anafanya kusudi ili umfukuze
achana nae, hakufai tena la sivo utalea watoto wa ex wake.
usikaze fuvu kuvumilia ujinga wake,
aman ya moyo ni muhimu kwako na mama na baba yako.
 
Mleta mada anaonekana bado ni kijana ndogo Hebu acheni kumsimanga ila mpeni ushauri mzuri aokoe uhusiano wake na mpenzi wake
 
Yawezekana mpenzi wako na ex wake waliachana kwa hasira, alikosewa vibaya au alichwa akakurupuka kuingia kwenye mahusiano na wewe.

Saiv either memories zinamtesa au kuna aina ya heka heka zinamtesa.

Cha kufanya kaa nae mbali, focus na mishe zako & epuka kukaa mwenyewe jichange kwenye mpira, pool table, vijiweni au popote patakapokuepusha na stress za kumuwaza.

Mapenzi ni field ya ajabu hela zako, tombaring capacity, uanaume wako & wema wako havina msaada siku za wapendanao zikitimia.
We jamaa umepiga spana kila mahali hujaacha lengo kbsa😂
 
Wakuu

Moyo wangu unaumia sana, naona kama unavuja damu kutokana na maumivu ninayoyapitia karibu kila siku.

Mpenzi wangu anatumia muda mwingi sana ku-chat na ex wake, na kila nikimuuliza anasema ni mazoea tu, hakuna kinachoendelea. Nilijaribu kujidanganya, nikajifanya niko sawa, lakini moyoni kulikuwa na kelele za maumivu yasiyoisha.

Kila notification ikilia, tabasamu lake lilinifanya nijisikie mgeni kwenye uhusiano wangu mwenyewe. Nilianza kujiuliza kama ni walishaachana, kwa nini bado ana nafasi kubwa kwenye penzi letu?

Siku moja nilikaa kimya, nikachagua kusikiliza zaidi kuliko kuuliza. Niliona jinsi anavyocheka, jinsi anavyopotea kwenye mazungumzo yao. Hapo ndipo niligundua kuwa si mazungumzo yakawaida, yaliniuma sana.

Nilimkalia chini na kusema kwa utulivu, ‘Sipigani na ex wako, napigania heshima na nafasi yangu.’
Alikaa kimya. Na kwenye ule ukimya, nilijua ama mahusiano yetu yameisha muda.

Naomba ushauri wako, nifanye nini kuhusu mkasa huu, kwani bado nampenda sana na nilikuwa na ndoto kubwa sana na huyu mpenzi wangu.
Kuwa busy basi 🖐️
 
Anza upya uelekeo mpya.... Hapo hapakufai tena.... Utachakazwa
 
Kichwa cha uzi kiwe" MPENZI WETU ANACHATI SANA NA MPENZI WAKE WA ZAMANI"

Nakopa maneno utakufa vibaya sana wewe,
Sasa si ufanye yako, achana na yake ,
Kinafikia tena nasema hivi unapata wapi muda wa kushika simu yake huna kazi za kufanya"
 
Back
Top Bottom