Mpenzi wangu mjamzito ila nimeambiwa kundi lake la damu haliendani na langu

Siyo kene, kwenye
 
Umeongea kitalam sana japo sijaelewa ila naomba kuuliza sasa hii ni mimba ya kwanza sio ya pili inakuwaje anilazimishe nitume hela au inakuwaje hapo, kwa ulivyochambua hilo jambo umesema mtoto wa pili ndo shida
Rudia kusoma vizuri alichoandika mkuu..mbona hata mimi nimeelewa.
Huyo mtoto wa kwanza ni lazima mchome hiyo sindano..
 
Jaman ndo maana mnapewa ushauri mpime kabla ya kujazana mimba mambo ndo haya hamtaki lipia dose cha laki mbili😹😹😹
Kulipia sio issue ila lazima nipate uhakika sio kupigwa kizembe kama mimba sio yangu jee??

Ila hebu nikuulize nimejaribu kuangalia huko akili bandia inasema sindano ziwe mbili moja week ya 28 -30 ingine masaa 72 hadi siku 28 baada ya kujifungua sasa hapo inakuwaje mfano je akichoma moja tu inakuwaje??

Asahiv nipo serious sasa tuache utani
 
Mtoto hurithi RhD Antigen ( chembechembe aina ya protini inayobebwa na Chembe Chembe hai nyekundu za Damu ) na kazi ya RhD Antigen ndio inayotanabaisha kundi lako la Damu kama ni A, B, AB, au O.

Sasa mtoto hurithi Kopi hizo kutoka Kwa Baba au Mama au Baba na Mama yake Kwa pamoja.

Inatokea mtoto anashindwa kurithi Kopi kutoka Kwa wazazi wote ,hii ndo inaitwa Rh Negative.



Sasa mfano, Mama ambaye ni RhD Negative, Akijazwa mimba na Baba ambaye ni RhD Positive , mtoto wa tumbon atarithi Kopi ya Positive kutoka Kwa Baba.


Kitakachotokea , Kinga ya Mwili ya mama itamtambua Mtoto huyo kama ADUI na kuanza kuzalisha Askari ( Rhesus Antibodies ) Hawa askari hupenya kwenye Placenta ( kondo) na kuingia kwenye Mzunguko wa Damu wa mtoto na kuanza Kuzivunjavunja Chembechembe hai nyekundu za Damu (RBC) Ambazo ndizo zimebeba RhD Antigens.

Nadhan unaelewa, chembechembe nyekundu za Damu zinaposhambuliwa na kuvunjwa vunjwa matokeo yake ni ni upungufu wa Damu, manjano ,magonjwa ya kutokwa na Damu , matatizo ya Ini, figo, ukuaji mbaya wa mtoto tumbon, Mtoto kufia tumbon, mimba kuharibika, kujifungua kabla ya wakati, kujifungua mtoto njiti n.k.



Kwanini Mimba ya kwanza Inakua salama?? Mimba ya kwanza unakuta Kinga ya mama haijazalisha askari wa kutosha, hivo utaanza kuzalisha taratibuuu taratibu mwishoowe kabisa Mtoto anazaliwa salama sababu Kinga ilikua haijajitosheleza.


Sasa baada ya hapo, kuanzia Mimba ya pili na kuendelea, tayari Mwili wa mama Kinga yake Inakua imeshazalisha askari wa kutosha, kwahiyo ni mwendo wa kushambulia na kuua tu .
 
Sio lazima awe ametoa anaweza asifahamu kama aliwahi kunasa ikaharibika. Huwa ni salama kuchoma tu hiyo anti D
 
Jaman si umeambiwa saiv lazima au na akijifungua anachomwa nyingine mtoto kama Kuna lilobaki
 
Hapa sasa nimeelewa vizuri sana asante ubarikiwe. Kwahyo kuna uwezekano kama hiyo dawa asipopata kwenye huu ujauzito wa kwanza inaweza kupelekea askari wakawa wengi kiasi kwamba mimba za pili na kuendelea askari wakaua wavamizi wote hata kabla hawajafika popote??
 
Sio lazima awe ametoa anaweza asifahamu kama aliwahi kunasa ikaharibika. Huwa ni salama kuchoma tu hiyo anti D
Asante nashukuru. Naomba kuuliza kwa kujifunza japo sio kwa umuhim

Je mwanamke akiwa bikira anajijua kabisa hajawahi kushiriki michezo yoyote hatarishi akikutana na issue kama hii inakuwaje, tunafuata utaratibu huo huo au
 
Umeongea kitalam sana japo sijaelewa ila naomba kuuliza sasa hii ni mimba ya kwanza sio ya pili inakuwaje anilazimishe nitume hela au inakuwaje hapo, kwa ulivyochambua hilo jambo umesema mtoto wa pili ndo shida
Ila viumbe wa siku hizi jamani. Hapa nachokiona hata akizaa poa tu, ila issue ni laki mbili! Umepoteza kiasi gani cha pesa toka uanze kujitambua mkuu! Piga moyo konde, kama ulijua utaenda nae tu alivyo, hajachagua kuwa na hilo group, toa pesa apate tiba. Imeshindikana, potezea, ila bahati mbaya mtoto akizaliwa na akaitwa wako, akajaambiwa ulimkana, jiandae na fedheha.
 
Asante nashukuru. Naomba kuuliza kwa kujifunza japo sio kwa umuhim

Je mwanamke akiwa bikira anajijua kabisa hajawahi kushiriki michezo yoyote hatarishi akikutana na issue kama hii inakuwaje, tunafuata utaratibu huo huo au
Kama ni hivyo, haina haja. Ni kusubiri ajifungue kwanza. Wanavyosema, kwa ujauzito wa kwanza anachoma masaa 72 baada ya kujifungua, na hapo ni endapo tu kama mtoto atakuwa na blood group ya baba. Kama ana kundi la damu la mama ambalo halina ile Rh, hamna haja ya kuchoma

Lakini kwa ujauzito wa pili na kuendelea kama mtoto wa kwanza alikuwa na kundi la damu la baba, basi ni muhimu akachoma kabla ujauzito kukuwa.
 
Mkuu hilo limeisha wacha tu nitoe sadaka akiwa wangu powa asipokuwa wangu powa kikubwa nitahakikisha ni kweli hiyo pesa inatumika kwa kazi hiyo na si vinginevyoo maana naweza kutuma pesa ikalipia vikoba wakati kuna maandalizi ya kujifungua n.k
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…