Mpenzi wangu mjamzito ila nimeambiwa kundi lake la damu haliendani na langu

Wacha ubishi wewe andazi toa hiyo hela mama akachome sindano. Mimba itaharibika hiyo! Na kama haitaharibika basi atakuwa siyo mtoto wako huyo!
 
Asante nashukuru. Naomba kuuliza kwa kujifunza japo sio kwa umuhim

Je mwanamke akiwa bikira anajijua kabisa hajawahi kushiriki michezo yoyote hatarishi akikutana na issue kama hii inakuwaje, tunafuata utaratibu huo huo au
Lakini pia, kwa upande wa mhudumu wa afya ni ngumu sana kuamini kwamba ni ujauzito wa kwanza, sababu bado kuna uwezekano kwamba huenda aliwahi kushika na asijue na ikaharibika kabla ya mwenyewe kujua. Na mengine ni maswala ya uaminifu zaidi ambayo mwenza hataki mwenzake ajue. Sasa hawezi kurisk hii mtoto afie tumboni ilihali kuna yanayoweza kufanyika. Mwisho wa siku pesa ni karatasi tu, cha muhimu uhai.

Nawaza tu na makande yangu tumboni niliyoshiba usiku
 
Asante Mungu akubariki yani unajibu vizuri bila hasira mkuu japo maswali yangu kidogo yanakwaza ila unanivumilia wewe ni mtu na nusu.


Sasa hapo hapo nina swali la nyongeza, je mtoto wa kwanza akifuata group la mama kuna uwezekano watoto wote wanaofuata wakafuata Rh ya mama au itakuwa tunaendelea kupima kwa kila atakapojifungua mtoto kuona ana chaji ya aina gani ili endapo kama huyo aliefuatia amechukua + basi ile process sasa ifanyike
 
Kúanzia mimba ya pili + zitakua mimba zinatoka chini ya miezi mitatu,

na kuhusu dawa atachomwa Kila abebapo Mimba zake zote .
 
Samahani wew ni kabila gani?
 
Ni kweli upo sahihi kabisa. Nimeshaelewa nitafanya taratibu zote kuona itakuwaje kwasabu bado tupo kwenye muda sahihi maana tumeambiwa kati ya week 28-30 na sasa ni week ya 28 na siku 4
 
Mtoto anaweza kuchukua kundi la damu la aidha mama, au baba. Wa kwanza anaweza kuwa na la mama, wa pili la baba, wa tatu la baba, wa nne la mama nk. Kwa maana hiyo kila akijifungua, ni lazima mtoto apime kundi la damu ili wajue wanamsaidia vipi mama, na pia watoto watakaofuata
 
Mkuu sikudai kwakweli ✊
 

Kama yeye kapimwa na kundi lake la damu ni O negative, cha kufanya ni kuhakikisha kwamba nawe unapimwa ili kujua kundi lako la damu ni lipi. (Negative au positive?)

Kama kundi lako ni negative basi itakuwa sawa, lakini kama utapimwa na kundi lako likawa Positive kuna sindano hiyo ambayo mkeo itabidi achomwe.

Hiyo sindano ni muhimu kwa sababu mwili wa mkeo huchukulia kundi la damu yako kama kigeni kwake hivyo hutengeneza kinga dhidi yake. Ili kuzuia hilo lisitokee mama huchomwa sindano.

Kama hatachomwa hiyo sindano baada ya kujifungua mtoto wake wa kwanza salama basi kuna hatari ya kupoteza (kuharibika) mimba zitakazofuata.

Kwa hiyo hakikisha mnapimwa makundi yenu ya damu na mwenzako achomwe hiyo sindano kwa utaratibu mtakaopewa hospitalini kama makundi yenu ni tofauti (negative kwa positive) ili muweze kuendelea kujenga familia yenu na watoto wenu wawe salama.

Kila la kheri.
 
Muonee huruma kijana wa watu, angalau anaonesha nia ya kuhudumia na kulea. Wengine wanakula kona wakipata habari hizi
Ila huyu sasa nikioa nikiweka ndani kizazi chetu si kitakuwa cha sindano maisha yote hivi watoto watakuwa na akili kweli sio kwa ubaya ila najaribu kuwaza ni kama watakuwa watoto wa kutengeneza hivi
 
Asante, wengine wanasema sindano mbili wengine moja naomba kuuliza je tunaweza kuchoma moja baada ya kujifungua ukilinganisha na hali ya kiuchumi ilivyo kwa sasa au ni lazima achome mbili maana hali ni ngumu mkuu
 
Ila huyu sasa nikioa nikiweka ndani kizazi chetu si kitakuwa cha sindano maisha yote hivi watoto watakuwa na akili kweli sio kwa ubaya ila najaribu kuwaza ni kama watakuwa watoto wa kutengeneza hivi
Huu sio ugonjwa, sio vizuri kuwaza hivi. Ni kama maumbile tu au rangi ya ngozi, wengine weusi, wengine maji ya kunde. Mimba hazitabiriki, na hazifanani. Wengine hawana issue hizi za kundi la damu lakini wanayopitia, hili lako ni jepesi sana
 
Huu sio ugonjwa, sio vizuri kuwaza hivi. Ni kama maumbile tu au rangi ya ngozi, wengine weusi, wengine maji ya kunde. Mimba hazitabiriki, na hazifanani. Wengine hawana issue hizi za kundi la damu lakini wanayopitia, hili lako ni jepesi sana
Asante nimekuelewa sana. Nashukuru kwa muda wako
 
Mkuu hilo limeisha wacha tu nitoe sadaka akiwa wangu powa asipokuwa wangu powa kikubwa nitahakikisha ni kweli hiyo pesa inatumika kwa kazi hiyo na si vinginevyoo maana naweza kutuma pesa ikalipia vikoba wakati kuna maandalizi ya kujifungua n.k
Hhhahahahahaha hapo mchawi uwepo wako kuhakikisha kweli hiyo pesa inalipwa. Japo mi binafsi naona kuna code furani hujaweka wazi. Inaelekea haaminiki tu
 
😂😂😂😂 Hizo ndo mambo nisizopenda…. Sasa kwani yeye mwanamke hana hiyo 200k Issue hiyo ndogo akishindwa ku-clear sasa atakuwa na msaada gani kwako mkuu?

Mtoto hajazaliwa ushaanza kuachiwa majukumu he!!

Anyway ushajikoroga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…