Mpiga picha wa Diamond atoa machozi baada ya kuzawadiwa gari

Yah kuna umuhimu wa kumzawadia jukwaani maana lilikuwa tukio la kutoa shukrani kwa watu wake sasa kwanini ajifiche
 
Big up kwa management ya diamond. Inajua kucheza na akili za mashabiki
 
Inategemea na makubaliano waliyoingia,navyojua Lukamba ameajiriwa na WCB kwahiyo analipwa mshahara kwa mwezi na other benefits kama Perdiem kipindi cha safari.

Let's say kama WCB wanamlipa labda 1.5m kwa mwezi anaweza kweli kununua altezza ya mil 12 kwa mshahara bila kukopa Bank? Je wafanyakazi wa Dr Mengi,Mo,Bakhresa Wote wana magari? Mimi kama mwajiri nakuajiri nakulipa mshahara ambao ndani yake una House allowance,Transport Allowance,Medical Allowance etc Wewe ndio utajua utautumia vipi.

Kwa Mujibu wa maelezo ya Diamond alikuja kustuka kwamba Lukamba anahitaji usafiri binafsi baada ya Kuibiwa Laptop na wezi so yeye kama yeye akajiongeza kumnunulia gari sio mbaya.
 
Ukiacha tu mshahara,zile shift za ulaya amerika na afrika kwenye show ni hela ndefu sana mana ni pa diemu,plus kumake hapa na pale,alikuwa na uwezo kabisa wa kupata hata ka Nissan Marc au starlet hata used tu ya M7,any way life is about priorities,simlaumu kwa chochote kile...
 
Ila kwa mfanyakazi wa kawaida kununua gari kwa mshahara bila mikopo ni ngumu ila kwa wasanii au mtu anayefanya kazi na wasanii inabidi awe na usafiri kutokana na kazi zao nyingi zinafanyika mida ya wanga au wanatoka kazini mida ya wanga.
 

Na Mimi nimeshangaa, yani miaka yote hyo lukamba alikua Hana gari? , that's weird, ndio maana mavoko aliondoka, Mavoko hakua ata na bajaji, kuna something fishy going on in wasafi
 
Kifesi alijenga nyumba Mwanza na Kununua gari akiwa wcb.
 
A

Akili ndogo kwenda Ulaya ndio sababu ya kununua gari? na huko vijijini Shitimbi watadai ukienda Dar basi lazima ununue baiskeli,gari kitu gani bana

Nimeongea hivyo on the implication kwamba safari lazima zinakuwa na malipo maalum zaidi ya mshahara kama zilivyo taasisi nyingine kama "per diem" n.k. Kumbe huko ni tofauti. Basi sawa nimejifunza kitu kipya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…