A
Anonymous
Guest
Kuna malalamiko kutoka Kijiji cha Mwamapuli, Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe mkoani Katavi, kuhusu geti linalodaiwa kukusanya ushuru wa mazao kinyume na taratibu.
Kwa mujibu wa wanaotoa taarifa hizi, geti hilo halifanyi kazi mchana, bali huanza shughuli zake kuanzia jioni hadi usiku. Inadaiwa kuwa nyakati hizo kuna mgambo na sungusungu wanaosimamisha magari yaliyobeba mazao na kuwatoza faini kuanzia Shilingi 20,000 na kuendelea. Pia kuna madai kwamba fedha zinazokusanywa hugawanywa kati ya wahusika ifikapo asubuhi.
Wananchi wanaomba mamlaka husika, ikiwemo TAKUKURU na vyombo vingine vya uchunguzi, kufuatilia kwa kina tuhuma hizi ili kubaini ukweli na kuchukua hatua stahiki endapo kutabainika kuwa kuna ukiukwaji wa sheria au matumizi mabaya ya madaraka.
Wanaotoa malalamiko hayo wanaeleza kuwa uchunguzi unaweza kufanyika kwa urahisi kwa kufanya ufuatiliaji wa siri katika eneo hilo, hasa kuanzia saa 12 jioni na kuendelea, ambapo wanadai shughuli hizo hufanyika.