Daby
JF-Expert Member
- Oct 26, 2014
- 34,954
- 80,256
Serikali nyingi nilizoshuhudia hasa Africa zikiangushwa imechangiwa kwa kiasi kikubwa na hamu ya madiliko kwa wananchi walio wengi.[mass support]Ina maana hata JPM akifufuka leo akigombea kupitia ACT unadhani asingekutwa na kilichomkuta Mpina?
Nlisema hapa, chadema kabla hata ya uchaguzi serikali za mitaa 90% ya wagombea wao walikatwa. Sasa hapo unashindaje?
Asilimia kubwa ya watu wakiyahitaji mabadiliko hakuna sheria mbovu wala jeshi imara kiasi gani litaweza kuyazuia. Humo humo utakuta mwalimu anayesimamia uchaguzi anahitaji mabadiliko, askari anayetumwa kulinda vituo vya uchaguzi, mkurugenzi n.k....
Chama tawala kikishaliona hili usually kuna options mbili...moja ni ile ya kutumia mabavu kubakia madarakani na nyingine ni kusurrender na kukubali kweli watu wanayataka mabadiliko kwa namna yoyote ile....
South Africa ANC ilianza kupoteza mvuto viongozi wakahama wakaanzisha vyama juzi kati wamepata 26%.....
Kenya [special case]
Zambia another case..
Botswana BDP kiongozi mkuu alitoka hadharani akatangaza kushindwa....
Je, Watanzania wanaonyesha nia ya dhati ya kuyataka mabadiliko? Jibu unalo.
Mabadiliko ni kama cancer ikishafika stage 4 ndiyo basi tena. Back 2010-2015 ungeniuliza tulifikia stage gani ningekuambia stage 3.....tulibakia kidogo tufike 4....
Ukiniuliza kwasasa tupo stage gani nitakuambia ndiyo kwanza tupo stage 1...... angalia hoja zinazosimamiwa na baadhi ya watu waliojitokeza hadharani[ regardless of their political reasons/wings] hakuna wa kuwaunga mkono[kwa taifa lenye ml60+]....
There's a lot to unfold...... by the way, muda mwingi sipendi mijadala ya kisiasa maana muda mwingi tunaishia kujadili tu hapa jukwaani na kuumiza vichwa lakini hakuna la maana tunalofanya kubadilisha mambo.