Mpina agonga mwamba Mahakama kuu Kesi ya Spika/ Mapingamizi ya Serikali yakubalika kwa Jaji

Mpina agonga mwamba Mahakama kuu Kesi ya Spika/ Mapingamizi ya Serikali yakubalika kwa Jaji

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610

Wakili Makore ambaye ni miongoni mwa Mawakili wa Mbunge wa Kisesa (CCM) Luhaga Mpina waliokuwa mstari wa mbele kumsimamia kwenye kesi aliyokuwa ameifungua Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala ndogo ya Dar es Salaam dhidi ya Spika wa Bunge la Tanzania ,Waziri wa Kilimo na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) akipinga kuondolewa Bungeni au kusimamishwa kuhudhuria vikao 15 vya Bunge ameeleza kilichojitokeza Mahakamani hapo hadi kufikia mteja wao 'kuangukia pua' kwenye kesi hiyo.

Wakili wa Serikali afafanua
Wakili wa Serikali Mkuu Hangi Chang'aa aliyekuwa anaongoza jopo la Mawakili wa serikali katika kesi iliyokuwa imefunguliwa na Mbunge wa jimbo la Kisesa (CCM) Luhaga Mpina dhidi ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Waziri wa Kilimo na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), kesi ambayo Mbunge huyo 'ameangukia pua' amesema Mahakama haina mamlaka ya kuingilia kazi au majukumu yaliyofanywa na Bunge kwa mujibu wa kanuni na sheria labda itokee vinginevyo

Akizungumza na Jambo TV leo, Alhamisi Oktoba 24.2024 muda mfupi baada ya Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala ndogo ya Dar es Salaam kukubaliana na mapingamizi yaliyowekwa na serikali kwenye kesi hiyo, Chang'aa amesema serikali imepokea kwa faraja maamuzi hayo kwa kuwa inaamini Mahakama imetenda maamuzi sahihi ambayo waliyataraj

PIA SOMA
- Kesi ya Mpina dhidi ya Bashe na Spika Tulia imeanza kusikilizwa Mahakamani leo Agost 28, 2024

- Kuelekea 2025 - Luhaga Mpina amshtaki Spika Tulia na Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa kuondolewa Bungeni kinyume na Sheria

- Mawakili wa Mpina walivyoijibu Serikali kesi aliyomfungulia Spika, Waziri wa Kilimo

- Mpina afungua kesi dhidi ya Spika wa Bunge, Waziri wa Fedha, Waziri wa Kilimo, Kamishna wa TRA, AG na Makampuni ya kuagiza Sukari
 
Nilimshangaa sana mpina kukubali kutumia mahakama ambazo zinaamua kesi Kwa kupigiwa simu kutoka magogoni kwenye soko la samaki.yaani alienda lakini mshindi anajulukana
Mahakama za kihanisi hizi. Speaker akikosea hawezi kuachwa afanye anavyojisikia!

Soma hii

We can interfere if speaker’s decision violates Parliament rules, says SC

Feb 13, 2017 07:59 PM IST India

The Supreme Court told the government on Monday that it can interfere with the Lok Sabha speaker’s decision if it violates the rules or procedures of Parliament..​

“If the speaker says blue is green, then we will ask the speaker to say it’s blue. We can’t let it go as green,” a bench headed by Chief Justice JS Khehar told attorney general Mukul Rohatgi, who had told the court that a speaker’s decision cannot be challenged in court.
 
Eti mahakama za Juma zimekataa maombi ya Mpina kuingilia Bunge. Ujinga, MAhakama za kishenzi!
Soma hii!

We can interfere if speaker’s decision violates Parliament rules, says SC

Feb 13, 2017 07:59 PM IST

The Supreme Court told the government on Monday that it can interfere with the Lok Sabha speaker’s decision if it violated the rules or procedures of Parliament..​

“If the speaker says blue is green, then we will ask the speaker to say it’s blue. We can’t let it go as green,” a bench headed by Chief Justice JS Khehar told attorney general Mukul Rohatgi, who had told the court that a speaker’s decision cannot be challenged in court.
 
Acha Mpina ajionee kwa kiwango gani yeye na wanaccm wenzake wameshiriki kubaribu mifumo ya kutoa haki nchi hii. Utashangaa mtu kama Mpina anaona huu ujinga, lakini ukimwambia adai katiba mpya hayuko tayari, anasimama na mtazamo wa chama chake.

Wanaccm huwa wanaamini hizi mahakama ni kwa ajili ya kukomoa wapinzani, huku wakidhani wao wako salama.
 
Mahakama haina mamlaka ya kuingilia kazi au majukumu yaliyofanywa na Bunge kwa mujibu wa kanuni na sheria labda itokee vinginevyo
Kwanza, Ningependa kuziona hizo kanuni, na sheria zinazozuia mahakama kufanya maamuzi juu ya kilichofanywa na Bunge; pili, ningependa kujua mazingira yanayotuhusu " labda itokee vinginevyo"!
====
Kwa haraka haraka kwenye tovuti ya Mahakama nimeikuta maelezo haya

"Kazi Kuu
Kutafsiri Sheria mbalimbali na maamuzi ya kiutawala ya utekelezaji. Kusikiliza na kuamua kesi zilizowasilishwa katika mahakama za sheria".
---
Sasa Bunge limefanya maamuzi ya kiutawala kwa kutumia taratibu na Sheria iliyoanzisha Bunge, inakuwaje Sasa mahakamani inasusa kufanya maamuzi ya haki juu ya shauri walilopelekewa?
 
Tuna katiba ya ovyo sana,hakuna check and balance,kila kitu ni siasa tu. Mhimili uliojichimbia zaidi una weza kufanya lolote bila kuingiliwa na mhimili mwingine 😏😏
 
Mbombo ngafu, ubaya ubwela. Mahakama yasema haiwezi kuingilia mambo yanayofanyika Bungeni, labda tu yawe yamevunja katiba..

Huu uamuzi umeandikwa kwa lugha ya Bibi Eliza (RIP), najua CDM hapa watatoka patupu kwa sababu wakati watu wanasoma, wao wamejificha makorongoni na kwenye majumba na magari mabovu
 

Attachments

HATA yeye nafikiri kama ana akili timamu alikuwa anajuwa kuwa hatashinda hiyo kesi na mawakili wake 100
 
mpina yuko nyuma ya walanguzi na wasioipendea mema nchi yetu kangunkia PUA
 
IMG_8078.jpeg


Katika Mahakama Kuu ya Tanzania, kesi iliyokuwa ikimhusisha Mheshimiwa Luhaga Joelson Mpina, Mbunge wa Kisesa, dhidi ya Spika wa Bunge na wengine imehitimishwa kwa uamuzi wa mahakama. Kesi hii, ambayo ilivutia hisia za umma kutokana na masuala ya haki, maadili, na nguvu za Bunge, ilihusu adhabu ya kusimamishwa kwa Mheshimiwa Mpina kutokana na tuhuma alizotoa dhidi ya Waziri wa Kilimo.

Kwa mujibu wa uamuzi wa Mahakama Kuu, Spika wa Bunge alikuwa ndani ya mamlaka yake kumtaka Mheshimiwa Mpina athibitishe madai yake kuhusu Waziri wa Kilimo kudanganya juu ya kiwango cha sukari nchini. Mheshimiwa Mpina alikabidhi vielelezo vya madai yake kwa Spika, lakini alitoa nyaraka hizo kwa vyombo vya habari kabla ya Bunge kuzipitia, jambo lililoonekana kukiuka maadili ya Bunge. Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge ilimkuta na hatia na kuamua kumsimamisha vikao 15 vya Bunge.

Mheshimiwa Mpina aliwasilisha kesi mahakamani akidai kuwa kusimamishwa kwake kulikuwa kinyume na Katiba, akisisitiza kuwa hakupata nafasi ya kusikilizwa ipasavyo na adhabu hiyo inaathiri uwakilishi wa wananchi wa Kisesa. Hata hivyo, Mahakama Kuu imeamua kuwa haina mamlaka ya kuingilia maamuzi ya Bunge yaliyofanyika ndani ya sheria na kanuni za Bunge, kwa mujibu wa ibara ya 100 ya Katiba inayolinda uhuru wa Bunge.

Uamuzi huu unaashiria umuhimu wa kuheshimu mgawanyo wa madaraka na kuhakikisha kuwa mihimili ya dola haivuki mipaka yake. Hata hivyo, jambo hili huwa linaleta ukakasi pale ambapo serikali kuonekana kuingilie almost mihimili yote ya nchi ikiwemo Bunge na Mahakama.

Kwa upande mwingine, Mahakama imebainisha kuwa inaweza kuingilia kati endapo Bunge linapofanya uamuzi nje ya mamlaka au kinyume na Katiba. Mahakama imehitimisha kwa kufuta kesi hii kwa hoja ya ukosefu wa mamlaka.

Kwa mujibu wa uamuzi huu, ni wazi kuwa Bunge lina nafasi kubwa katika kusimamia maadili ya wabunge wake lakini linasisitizwa kufuata kanuni za kikatiba kwa haki na uwazi.



View: https://youtu.be/rmrZbtePvb8?si=jgw4kltfWE_8pU3K
 

Attachments

  • IMG_8078.jpeg
    IMG_8078.jpeg
    194.5 KB · Views: 4
Back
Top Bottom