Mpina ampongeza Rais Samia kwa kumuondoa January Makamba TANESCO, alihusika na ufisadi wa kutisha

Mpina ampongeza Rais Samia kwa kumuondoa January Makamba TANESCO, alihusika na ufisadi wa kutisha

Mbunge asiyepoa wa jimbo la Kisesa wilaya Meatu Mh Mpina akichangia bajeti ya wizara ya Nishati na madini amempongeza Rais Samia kwa kumfukuza waziri January Makamba kwenye wizara hiyo kwani alihusika na dili na ufisadi mkubwa sana kwenye wizara hiyo.

Mfano wa ufisadi ni kuajiri wafanyakazi 6 bila kutoa tangazo wala kuwafanyia interview, wafanyakazi hao walikuja kuhusika moja kwa moja na katakata ya umeme iliyokuwa imeshika kasi nchini.

Ufisadi namba mbili ni kufuta vituo vyote vya huduma kwa wateja mikoani na kucentralize huduma Dares salaam kwa kampuni la Airlink ambalo halijulikani lililetwa na nani, na wananchi kutozwa gharama kila wanapopiga huduma kwa wateja ambapo hizo hela haieleweki analipwa nani.

Ufisadi namba tatu ni mradi wa kuweka umeme kwenye mji wa serikali Mtumba ambapo January Makamba alipandisha gharama kutoka billioni 41 hadi billion 50 bila kuelezwa sababu ni nini!

View attachment 2973633
Huyu Mbunge anazungumza maneno Kuntu ninampenda sana anasema ukweli kuliko Wabunge wengine Mungu amlinde amin. January alikuwa ni Mfisadi ndio Maana Rais Magufuli alimuondoa katika Uwaziri.
 
Un
Mbakama rinuja?

Hajawahi kufaa popote pale..., sema tu kwenye mafamilia kuna siri kubwa, huwenda hata hapo kwao alikuwa mpigaji sana, mtu hawezi kuacha chenji mezani
Unaloliona leo msingi wake umejengwa jana.
 
Huyu mpina nae ni walewale.... Kwani hatujui ufisadi na uuwaji alioufanya Kanda ya ziwa kwa wavuvi?, ameua na kutesa wavuvi bila huruma. Anayasema haya yote sababu yupo nje ya mfumo. Watu wa Aina ya mpina ni hatari Sana, amalizie ubunge wake asitegemee kurudi 2025.
Anayasema kwasababu yeye ni mbunge sio waziri na kazi ya mbunge ni hiyo.

Ukiwa mbunge kazi yako ni kuisimamia serikali na ukiwa waziri wewe upo upande wa serikali.

Kinachotushangaza ni wabunge wengine kuwa chawa WA serikali badala ya kuisimamia serikali.
 
Back
Top Bottom