Mpina ataka mdahalo na Mwigulu ufisadi wa Trilioni 30

Mpina ataka mdahalo na Mwigulu ufisadi wa Trilioni 30

Hicho kias cha pesa watu wala hawapelekwi mahakamani wala kushtakiwa lakini kuna dada amekula nyama ya swala amepigwa miaka 20 dah kweli sheria zipo kwa ajili ya maskini
 
Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina ameomba kufanya mdahalo na Waziri wa Fedha, Dk. Mwigulu Nchemba live kwenye Televisheni kuzungumzia kashfa ya ufisadi wa Trilioni 30 alizochambua kutoka ripoti ya CAG ili kukata mzizi wa fitna.

Mpina alisema wakati anachangia ripoti ya CAG, Waziri Mwigulu alimfanyia fujo kwa kumkatiza kwa kujifanya anampa taarifa kumbe ulikuwa ni ujanja wa kumpotezea muda ashindwe kudadavua vizuri ufisadi wa Trilioni 30.

Hivyo Mpina amemuomba Waziri Mwigulu kukubali ashiriki mdahalo live kwenye luninga wakizungumzia ufisadi huo wa Trilioni 30.
Aseme kwanza pesa zawavuvi alikusanya kiasi gani nazikowapi kwanini alifanya unyama ule?
 
Hujamuelewa kuna hoja mbili tofauti za Mpina moja ya Trilioni 30 kupitia ripoti ya CAG na ya pili Trilioni 280 ni za miamala shuku kupitia ripoti FIU ambazo hazimo kwenye ripoti ya CAG usichanganye mambo
Wengi uwa wanakurupuka kujibu fikra tafakuri hawana
 
Wewe na yeye wote akili moja .
Makusanyo ya nchi nzima hayafiki trillion 25...
Uje useme tumeibiwa trillion 280..?
I think ana kitu tumsikilize.
Kwa mtazamo wangu wa haraka haraka, tunaambiwa makusanyo ni T30 na hapo ni baada ya CCM na Co (Miamala Shuku) wao kuchukua zao mapema.

Now lets assume kusingekuwa na huu wizi wa CCM maana ni wengi na wanachepusha mapato yetu sio kwa maElfu bali kwa maBillion ya TSh.

Bila wizi wao tungekusanya pesa nyingi sana.
 
Back
Top Bottom