Mpina atakiwa apeleke Ushahidi wa Madai yake kwamba Maagizo ya Waziri Mkuu Majaliwa hayatekelezwi na Watendaji wa Serikali!

Mpina atakiwa apeleke Ushahidi wa Madai yake kwamba Maagizo ya Waziri Mkuu Majaliwa hayatekelezwi na Watendaji wa Serikali!

Magufuli hayupo Sasa wapinzani wako wapi?
Wapinzani wana Serikali?
Hao Magufuli aliokuwa anawahujumu, kuwafunga hata kuwaua - leo ghafla wawe na majukumu ya kiserikali? Uko serious kweli ?

Tupeni matokeo ya "Mafiga matatu" ya Magufuli.
 
Akizungumza Bungeni leo Lugaha Mpina amedai ya kuwa kuna maagizo aliyatoa Waziri Mkuu na hayafanyiwi kazi na Waziri Mkuu yupo kimya hatua inayoonesha labda naye ameridhia

Hata hivyo hoja zake zilipingwa na Waziri Jennista Mhagama akidai ya kuwa hazina ukweli kwamba maagizo yanafanyiwa kazi na machache sana inawezekana bado hayajafanyiwa kazi

Mpina amesema kuwa tangu Waziri Mkuu akataze ‘Kamatakamata ya Mifugo bila kushirikisha Wananchi’, jambo hilo limekuwa likiendelea katika baadhi ya maeneo akidai na ushahidi upo

Spika wa Bunge amemtaka Mpina kuwasilisha Ushahidi wa mambo hayo kabla yeye hajatolea uamuzi jambo hilo ikiwa ni kweli Mpina amedanganya Bunge au la (Taarifa ya Waziri Mhagama)
==

MY TAKE
Hapa nadhani Mpina keshaingia Kwenye 18 akishindwa kuleta ushahidi atatupwa nje ya Bunge hadi mwakani 2024

Akirudi Ripoti ya CAG ishajadiliwa na maazimio yameshatolewa

Mungu wa mbinguni awabariki!
Unahitaji ushahidi gani kiongozi .
 
Magufuli hayupo Sasa wapinzani wako wapi?
Ndio hayuko ila maamuzi na matendo yake tunayo leo na yanatusumbua mno. Mfano hilo Bunge, miongoni mwa madudu yake mengi aliyotuachia.

Na leo hii hatuna namna ya kufanya maana Katiba yetu mbovu hairuhusu sisi wananchi kuliwajibisha Bunge.
Inasema hadi kwenye uchaguzi, ambao ni kila baada ya miaka 5; yaani tuvumilie uharibifu, hasara, ufisadi nk mpaka miaka 5 ipite!

Na chaguzi zenyewe, hayati Magufuli alituonyesha kuwa si kitu, bali ni maigizo tu.
Ndio maana tunataka Katiba mpya Sasa hivi.
 
Siku hizi Uchawa na Usanii unalipa sana, Yaani katika Bunge la leo kama kuna Mpinzani ni huyu Jamaa MPINA! Mtu mmoja analiamsha Bunge zima. Yeye kazungumzia miaka ya nyuma na mifano katoa mifugo zaidi ya Elfu 3 kuuza kiholela. Wao wanadao kasema haya yametokea baada ya Hotuba ya Waziri Mkuu majuzi.

Kwani bunge sasa hivi au futuhi ndani ya jengo la bunge?
 
Tuanzie kwanza aliupataje ubunge wake, kwa kura au kuhujumu wagombea wengine apite bila kupingwa? Kama ameingia kwa njia za kihuni basi maagizo yake ni ya kupuuzwa.
Toka hapa wewe Nyumbu. Tunajadili yaliyojili Bungeni hivi karibuni. Hivi nyie CHADEMA vichwa vyenu vimejaa takataka gani lakini?
 
Akizungumza Bungeni leo Lugaha Mpina amedai ya kuwa kuna maagizo aliyatoa Waziri Mkuu na hayafanyiwi kazi na Waziri Mkuu yupo kimya hatua inayoonesha labda naye ameridhia

Hata hivyo hoja zake zilipingwa na Waziri Jennista Mhagama akidai ya kuwa hazina ukweli kwamba maagizo yanafanyiwa kazi na machache sana inawezekana bado hayajafanyiwa kazi

Mpina amesema kuwa tangu Waziri Mkuu akataze ‘Kamatakamata ya Mifugo bila kushirikisha Wananchi’, jambo hilo limekuwa likiendelea katika baadhi ya maeneo akidai na ushahidi upo

Spika wa Bunge amemtaka Mpina kuwasilisha Ushahidi wa mambo hayo kabla yeye hajatolea uamuzi jambo hilo ikiwa ni kweli Mpina amedanganya Bunge au la (Taarifa ya Waziri Mhagama)
==

MY TAKE
Hapa nadhani Mpina keshaingia Kwenye 18 akishindwa kuleta ushahidi atatupwa nje ya Bunge hadi mwakani 2024

Akirudi Ripoti ya CAG ishajadiliwa na maazimio yameshatolewa

Mungu wa mbinguni awabariki!
Leo kichwa chako umekirudisha mahali pake sawaswa kabisa.
 
Wapinzani wana Serikali?
Hao Magufuli aliokuwa anawahujumu, kuwafunga hata kuwaua - leo ghafla wawe na majukumu ya kiserikali? Uko serious kweli ?

Tupeni matokeo ya "Mafiga matatu" ya Magufuli.
Mbowe anavyobugia asali bila kupaliwa hatuoni ajabu kumshambulia JPM.

Kwa sasa ni kulamba na kulala fofofo
 
Luhanga Mpina karibu CHADEMA Bro.
CHADEMA haimo Bungeni (kasoro yule wa Nkasi, ambaye naye ni kama CCM); lakini mbona hata huko nje ya Bunge imekuwa kama haipo?
Hii dawa ya ganzi iliyodungwa kweli itakwisha karibuni?
 
Mbowe anavyobugia asali bila kupaliwa hatuoni ajabu kumshambulia JPM.

Kwa sasa ni kulamba na kulala fofofo
Yaani umeshiba propganda unadhani kila mtu yuko kama wewe.

Madhaifu na mabaya ya utawala na sera zake mbovu haviwezi kufutwa na propganda mfu kama hizi za kwenu.

Mwendazake alitutia hasara, na leo tunaendelea kulipa hasara na gharama.

Jikite kwenye hoja na mada.
 
CHADEMA haimo Bungeni (kasoro yule wa Nkasi, ambaye naye ni kama CCM); lakini mbona hata huko nje ya Bunge imekuwa kama haipo?
Hii dawa ya ganzi iliyodungwa kweli itakwisha karibuni?
2025
 
Kuna kipindi flani nikiwa kijijini ziara ya waziri mkuu ilinikuta, kulikua na mgogoro wa wananchi na REA kuhusu kufikishiwa umeme Kijiji B, akajitokeza mwananchi Moja akilalamikia nguzo za umeme zilizotumika Kijiji A zimebaki basi akamwomba waziri mkuu wapelekwe umeme kijijini kwao yaani Kijiji B.

Na waziri mkuu akatoa agizo Hilo jambo litekelezwe ziara ikaisha waziri karudi zake. Zikapita kama wiki nikajifanya kimbelembele nikashawishi tukafatilie kwa meneja TANESCO wilaya mwenyekiti akaunda kamati ndogo kufatilia tukaenda mpaka kwa meneja wa wilaya.

Tukajitambulisha baada ya kujitambulisha na kumweleza kilicho tuleta kwanza alishangaa akauliza kama Kuna yeyote anaefahamu utaratibu wa taarifa na maagizo ya kikazi nikamwambia najua.

Akauliza zinakuwaje nikajibu zipo njia nyingi zingine kwa mdomo zingine kwa barua zingine ki digitali, akauliza nyie nani amewaambia mfatilie taarifa za wanasiasa za majukwaani, nikamuuliza unamaana gani? Akasema serikali inao utaratibu wake kama Yale maagizo yasingekuwa ya kisiasa Hilo jambo lingeshatekelezwa kwa hiyo hawafanyii kazi maneno ya jukwaani.
 
Back
Top Bottom