Mpina, Bashe, Kamati ya Maadili, Spika, Wazalishaji na Bodi ya sukari nani kweli?

Mpina, Bashe, Kamati ya Maadili, Spika, Wazalishaji na Bodi ya sukari nani kweli?

saidoo25

JF-Expert Member
Joined
Jul 4, 2022
Posts
624
Reaction score
1,456
MJADALA wa Kashfa ya Sukari umezungumza sana ndani ya Bunge na nje ya Bunge hadi kusababisha Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina kufukuzwa bungeni baada ya kumtuhumu Waziri wa Kilimo Hussein Bashe kusema uongo kuhusu utoaji wa vibali vya waagizaji sukari nje ya nchi.

Jana Profesa Bengesi wa Bodi ya Sukari naye amezungumza kuhusiana na kashfa hiyo na uzuri watanzania wote tumewasikia kuanzia Mpina, Bashe, Kamati ya Bunge ya Maadili, Spika Tulia, Wazalishaji wa sukari na Bodi yenyewe ya Sukari kama wananchi sasa tumuamini nani?
 
Bashe katembeza rushwa vizuri wote hawaoni point za Mpina wala wazalishaji wa sukari
 
MJADALA wa Kashfa ya Sukari umezungumza sana ndani ya Bunge na nje ya Bunge hadi kusababisha Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina kufukuzwa bungeni baada ya kumtuhumu Waziri wa Kilimo Hussein Bashe kusema uongo kuhusu utoaji wa vibali vya waagizaji sukari nje ya nchi.

Jana Profesa Bengesi wa Bodi ya Sukari naye amezungumza kuhusiana na kashfa hiyo na uzuri watanzania wote tumewasikia kuanzia Mpina, Bashe, Kamati ya Bunge ya Maadili, Spika Tulia, Wazalishaji wa sukari na Bodi yenyewe ya Sukari kama wananchi sasa tumuamini nani?
Tumia jicho la tatu, (fikiria nje ya sanduku) utapata jibu, soma pia kuhusu ostracism utanishukuru
 
Mpina mganga njaa, amehongwa na wamiliki wa viwanda vya sukari
 
Yaani umeona body ya sukari ina hoja kweli zaidi ya porojo baada ya kukutana na waandishi wasiouliza maswali ya msingi.

Watu wanazungumzia kucheleweshewa vibali vya 2023/24 walivyoomba. Yeye analeta hadithi za vibali vya 2022/23.

Watu wanazungumzia lead time ya kuagiza viwandani (ambapo viwanda lazima viongoze production capacity) na kupanga shipping arrangement ambapo ‘optimal time’ ni miezi miwili mpaka mitatu. Yeye analeta habari za kwenda kununua kwenye maghala ya wafanyabiashara wa Uganda kwa week moja.

Sanasana body ya sukari ilichoonyesha na yenyewe ni sehemu ya genge la wahuni.
 
Hiyo kesi hata mwanafunzi wa mwaka wa kwanza sheria anaweza kuitolea maamuzi.
 
Back
Top Bottom