Mpina bila kukatwa angebaki CCM milele, ni hasira tu zilezile za watangulizi wake.

Mpina bila kukatwa angebaki CCM milele, ni hasira tu zilezile za watangulizi wake.

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
18,154
Reaction score
17,491
Mpina amekuwa mbunge wa CCM kwa miaka 20, na alikuwa anaomba kuemdelea kuwa mbunge kabla ya kukatwa jina lake na kutimkia ACT.

Tunaposema safari ya vyama vya upinzani bado ni ndefu sana maana yake ndiyo hii. Mpina hakipendi chama cha ACT, bali amelazimika tu kama walivyolazimika akina Mrema, Slaa, Lowasa, Sumaye, Membe na wengine. Hii ni kusema vyama vya upinzani hakuna watu wenye hadhi. Hata Mpina atarudi CCM baada ya kumaliza mission yake ya kuidhoofisha ACT, au hasira zake zikishuka au atakapolazimishwa kurudi CCM.

Mpina huyu ataanza kudaiwa kila aina ya kodi aliyoikwepa kulipa wakati akiwa mbunge wa CCM, atarudi tu CCM alikozoea. Silaha kubwa ya CCM ni kukunyooshea mambo yote ambayo uliyapindisha wakati ukiwa kada wa CCM. Watazinusa biashara zako zote ili kuona ulichepuka wapi ili ulipe kodi zako zote, wataangalia kuona kama una ardhi ambayo uliipata bila kufuata taratibu, au kama kuna jengo ambalo umelijenga bila kufuata utaratibu wataanza kukunyooshea pale ulipopindisha. TRA, Ardhi na mipango miji watakuwa wageni wako kila siku kuhakikisha unalipa kikamilifu mapato yako. Kama ulikuwa na wafanyakazi ambao ulikuwa huwalipi haki zao vizuri wataanza kudai ili walipwe lizizo zao na mafao yao mbalimbali.
 
Mpina amekuwa mbunge wa CCM kwa miaka 20, na alikuwa anaomba kuemdelea kuwa mbunge kabla ya kukatwa jina lake na kutimkia ACT.

Tunaposema safari ya vyama vya upinzani bado ni ndefu sana. Mpina hakipendi chama cha ACT, bali amelazimika tu kama walivyolazimika akina Mrema, Slaa, Lowasa, Sumaye, Membe na wengine. Hii ni kusema vyama vya upinzani hakuna watu wenye hadhi. Hata Mpina atarudi CCM baada ya kumaliza mission yake ya kuidhoofisha ACT, au hasira zake zikishuka au atakapolazimishwa kurudi CCM.

Mpina huyu ataanza kudaiwa kila aina ya kodi aliyoikwepa kulipa wakati akiwa mbunge wa CCM, atarudi tu CCM alikozoea.
Hio ndio silaha ya CCM wanayoitumia mpaka majimboni. Jimbo akipewa mpinzani tu ujue wananchi kazi mnayo😁!

Mtatengwa na chama cha mbogamboga hela za miradi mtazisikia kwa majirani tu. Miaka 10 hata moram wala mtaro hautawekwa ili kuwakomoa.
 
Mpina amekuwa mbunge wa CCM kwa miaka 20, na alikuwa anaomba kuemdelea kuwa mbunge kabla ya kukatwa jina lake na kutimkia ACT.

Tunaposema safari ya vyama vya upinzani bado ni ndefu sana. Mpina hakipendi chama cha ACT, bali amelazimika tu kama walivyolazimika akina Mrema, Slaa, Lowasa, Sumaye, Membe na wengine. Hii ni kusema vyama vya upinzani hakuna watu wenye hadhi. Hata Mpina atarudi CCM baada ya kumaliza mission yake ya kuidhoofisha ACT, au hasira zake zikishuka au atakapolazimishwa kurudi CCM.

Mpina huyu ataanza kudaiwa kila aina ya kodi aliyoikwepa kulipa wakati akiwa mbunge wa CCM, atarudi tu CCM alikozoea.
Kweli.
 
Back
Top Bottom