Mpina anajielewa sana, ameamua kuachana na Katiba ya JMT 1977 inayompa uhuru wa kutoa maoni yake, akaona awakaange directly kwenye kanuni zao za bunge.
Ni kweli, Spika kusema taarifa aliyowasilisha Mpina kwake na kuundiwa kamati ilikuwa ya siri, hiyo siri inakuja vipi ikiwa wakati wa utoaji wa taarifa husika bunge lilikuwa live likirusha matangazo yake kwa njia za Tv na radio? kwani hapo wananchi hawakuona na kusikia?!
Spika Tulia hajui anachofanya, ameamua kumlinda Bashe na mama Abdul na kuigeuzia hii kesi upande wa bunge, kama vile tuhuma za Mpina zililihusu Bunge, wakati ukweli Mpina alimtuhumu Bashe kusema uongo bungeni.
Ajabu mpaka leo Bashe yuko kimya, hii maana yake hana majibu, ameamua kunyamaza akijua atalindwa na mama Abdul, huyu mama kwa ukimya wake anaendelea kutoa kibali kwa Bashe atupige apendavyo mbele ya safari, BBT na sukari havitoshi!. kweli wanakula kwa urefu wa kamba zao.
Ni kiongozi wa ajabu sana kuwahi kuliongoza hili taifa, hajui kabisa anachofanya ikulu, tunapigwa kila upande ametulia akitazama anajibatiza na jina kujiita chura kiziwi, kiongozi asiyeweza kujibu tuhuma zinazoihusu serikali yake ni mzigo kwa taifa.
Nimalizie kwa kuwakumbusha wale chawa kina@Tlaatlaah &
Stuxnet, Mpina ameamua kujilipua hajali chochote, dhamira yake inamsukuma kusema ukweli na yupo tayari kulipia gharama za ukweli wake sababu anajua ukweli unamuweka huru.
Njaa zenu vichwani na matumboni mwenu havipo kwa Mpina, anawatumikia watanganyika na wapiga kura wake, adhabu yoyote mtakayompa kwa kuzidi kuwaonesha udhaifu wenu kwake yupo tayari.
Kamati inayomuita Bashe mtuhumiwa, kisha kumuacha Mpina mtoa hoja na kumuadhibu bila kumsikiliza, ni ya ajabu, ilivunja Katiba ya nchi.
Nasimama na Mpina.