Mpina: Kifungu kilichotumiwa na Spika Tulia kunituhumu na kunihukumu hakipo!

Mpina: Kifungu kilichotumiwa na Spika Tulia kunituhumu na kunihukumu hakipo!

hii ndio ile inaitwa ujuaji mwingi Mbele kiza 🤣

kwamba eti mzalendo anapeleka uongo na upotoshaji wake mwenyewe wa kubuni na kutunga mahakamani 🐒

hivi anatumia akili au nanatumia forces za upotoshaji za mwabukusi kwamba katika hali ya dharura tunatumia utaratibu anaotaka yeye kusolve changamoto za nchi 🤣
 
Wasije wakamfilikunjombe akiangalia tu, ndo hofu yangu

Nia yao ilikua hiyo ndio maana wamehamaki kuwa alipoongea na vyombo vya habari. Walidhani atawaletea ushahidi halafu wakishaupokea na kugundua kuwa taarifa yake ni ya kweli basi wangetafuta namna mbaya sana halafu wananchi tungeshangaa tu mmtu ameangushwa chali . Kamati inamwagiwa mabilini mengine wanagawana na monita wao wanasema ushahidi na taarifa yake haina ukweli wowote na hapo wananchi tusingejua chocho tena kuhusiana na Wizi na utapeli huo mkubwa uliofanya na wanaCCM na serikali yao .
 
Garma
hii ndio ile inaitwa ujuaji mwingi Mbele kiza 🤣

kwamba eti mzalendo anapeleka uongo na upotoshaji wake mwenyewe wa kubuni na kutunga mahakamani 🐒

hivi anatumia akili au nanatumia forces za upotoshaji za mwabukusi kwamba katika hali ya dharura tunatumia utaratibu anaotaka yeye kusolve changamoto za nchi 🤣
 
Hahaha zitto junior sikiliza vizuri ukija uwe na hoja usije ukaanza kuleta uchawa.
Huyu ni mropokaji tu anayetafuta attention. Hata hiyo kanuni anayolalamikia hawezi thibitisha. Mimi sijawahi kuunga mkono haya mafisadi ya CCM maana ni wasaka vyeo. Huyu akiteuliwa uwaziri na samia kabla ya 2025 mtakuja kuona atakavyogeuka chawa ndio mtanielewa. Gwajima yuko wapi? Polepole yuko wapi, na kunambi yuko wapi??
 
Mpina anajielewa sana, ameamua kuachana na Katiba ya JMT 1977 inayompa uhuru wa kutoa maoni yake, akaona awakaange directly kwenye kanuni zao za bunge.

Ni kweli, Spika kusema taarifa aliyowasilisha Mpina kwake na kuundiwa kamati ilikuwa ya siri, hiyo siri inakuja vipi ikiwa wakati wa utoaji wa taarifa husika bunge lilikuwa live likirusha matangazo yake kwa njia za Tv na radio? kwani hapo wananchi hawakuona na kusikia?!

Spika Tulia hajui anachofanya, ameamua kumlinda Bashe na mama Abdul na kuigeuzia hii kesi upande wa bunge, kama vile tuhuma za Mpina zililihusu Bunge, wakati ukweli Mpina alimtuhumu Bashe kusema uongo bungeni.

Ajabu mpaka leo Bashe yuko kimya, hii maana yake hana majibu, ameamua kunyamaza akijua atalindwa na mama Abdul, huyu mama kwa ukimya wake anaendelea kutoa kibali kwa Bashe atupige apendavyo mbele ya safari, BBT na sukari havitoshi!. kweli wanakula kwa urefu wa kamba zao.

Ni kiongozi wa ajabu sana kuwahi kuliongoza hili taifa, hajui kabisa anachofanya ikulu, tunapigwa kila upande ametulia akitazama anajibatiza na jina kujiita chura kiziwi, kiongozi asiyeweza kujibu tuhuma zinazoihusu serikali yake ni mzigo kwa taifa.

Nimalizie kwa kuwakumbusha wale chawa kina@Tlaatlaah & Stuxnet Mpina ameamua kujilipua hajali chochote, dhamira yake inamsukuma kusema ukweli na yupo tayari kulipia gharama za ukweli wake sababu anajua ukweli unamuweka huru.

Njaa zenu vichwani na matumboni mwenu havipo kwa Mpina, anawatumikia watanganyika na wapiga kura wake, adhabu yoyote mtakayompa kwa kuzidi kuwaonesha udhaifu wenu kwake yupo tayari.

Kamati inayomuita Bashe mtuhumiwa, kisha kumuacha Mpina mtoa hoja na kumuadhibu bila kumsikiliza, ni ya ajabu, ilivunja Katiba ya nchi.

Nasimama na Mpina.
Hata kama wasipotenda Haki tulishawaona tulia akili yake ipo uchi na anatetea majambazi wenzake, Hana akili wala uwezo wa kupingana kihoja na mpina, mkimbizi Bashe ndio kabisa debe tupu lilishindwa hata kusimama kujibu linatetewa kama haliwezi kuongea.
 
Back
Top Bottom