ndolelejiUduhe
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,837
- 3,027
Kwa sababu watu wengi wa Nchi hii na Africa yote wanaupenda sana ufisadi ndio maana kitu chochote cha maana kikianzishwa na wakakabidhiwa kukiendesha kitu cha kwanza watakachokifanya ni kutengeneza mipango na mbinu zao za kupiga pesa kupitia hicho walichokabidhiwa !Ulifuatilia hoja zilizotolewa na wapinzani kuhusu mushkeli mkubwa uliomo kwenye uamuzi wa kununua ndege kwa cash bila business plan wala kuzingatia taratibu za manunuzi?
Huo mzaha wa mitaani kuhusu “mapanga boi” sio hoja ya kujadiliwa kwenye mada hii.
It was a bad decision; it still is. ATCL haitafufuka na italiletea taifa hasara ya mabilioni tukiendelea na ujinga wa kununua ndege “gizani” na kuzitumia bila mpangilio makini wa kibiashara.
Kuhusu watu kuzipanda, watazipanda tu zikiwepo kwa malipo kama wanavyopanda zingine zilizopo kwenye soko. Tanzania hatujawahi kuwa na shida ya usafiri wa ndege.
Hata SGR serikali ikipaparika kuendekeza hizo Safari fupi za abiria kufurahisha mashabiki kabla mradi haujakamilika na kuanza kusafirisha mizigo mikubwa itaishia kwenye mawe. TAZARA na TRC pamoja na ukongwe zinaponea ruzuku hadi leo.
Haya sio masuala ya propaganda nyepesi nyepesi.
Au nasema Uongo ndugu zanguni ????! 😳🙄