Mpira wa Tanzania ni wa kibosi. Mashabiki, wachezaji na viongozi wote ni mabosi

Mpira wa Tanzania ni wa kibosi. Mashabiki, wachezaji na viongozi wote ni mabosi

Mganguzi

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2022
Posts
1,604
Reaction score
3,715
Ndiyo, nimeona tofauti ya mashabiki wa Tanzania na nchi zingine. Yanga jana imefungwa lakini mashabiki walichangia kuwavuruga wachezaji wetu! Ile kelele na lile vibe, ni lazima timu yoyote inayokwenda kucheza uwanja ule ijipange!

Sisi mashabiki wa Kitanzania tukiingia uwanjani utaona watu wamekaa kama wanasubiri masufuria ya wali, wengine wanaongea na simu, wengine wanapiga selfie, wako wanaotembeza vitumbua, wapo waliokaa wanatafuna bisi, mabosi nao utaona wamekaa, wanasubiri goli lifungwe ndio washangilie baada ya hapo wanakaa tena.

Kama hatuwezi hakuna haja ya kwenda viwanjani!
 
Ndio nimeona tofauti ya mashabiki wa Tanzania na nchi zingine ,yanga Jana imefungwa lakini mashabiki walichangia kuwavuruga wachezaji wetu ! Ile kelele na lile vibe ,ni lazima timu yoyote inayokwenda kucheza uwanja ule ijipange! Sisi mashabiki wa kitanzania tukiingia uwanjani utaona watu wamekaa kama wanasubiri masufuria ya wali, wengine wanaongea na cm ,wengine wanapiga selfie ,wako wanaotembeza vitumbua, wapo waliokaa wanatafuna popcorn, mabosi nao utaona wamekaa ,wanasubiri goli lifungwe ndio washangilie baada ya hapo wanakaa tena, kama hatuwezi hakuna haja ya kwenda viwanjani
Hi sababu ya kelele siyo sababu geniun
 
Sema wenzetu wanajua kushangilia
 
Kama ni hivyo basi mkuu tutafute kundi la mama lishe tuliingize uwanjani washangilie kama majini kwa nguvu na parapanda ili ushauri wako utimie.
 
Back
Top Bottom