Mpira wa Tanzania unaharibiwa na vilabu viwili -- Simba na Yanga

Mimi nakupinga
Hakuna mtu anataka kuwekeza kwenye hasara simba na yanga ndo timu zinazofanya vizur nazina mashabiki wengi kama ulivosema, lazima mtu awekeze anapo weza kupata faida.

Mo kabka hajaja sima alikua african lyon kama sikosei watu wakaiita ni simba ndogo, kwann mo akaamua kuwekeza simba kwa sababu kuna fans wengi zaidi ambai ndio walengwa.

Twende kwa gsm amedhamini timu ngapi na je ni timu gani ameweka nguvu kubwa ni yanga kwa sababu ina fans wengi na hao ndio walengwa kibiashara.

Twende faida za kinchi timu nyingi zimekuwa zikiingia michuano yakimataifa kwa mfano kmc namungo azam yanga na simba ilaa wote wamekua wakifeli isipokua simba ambaye kaifanya ligi yetu ionekane moja ya ligi bora africa,
asa ni kivip simba inadumza soka letu? Na vipi yanga anadumaza soka letu? Kama ni hujuma kila nchi inahujuma zake za kiisoka.
 
kama ni mpezi wa timu za ulaya na wingereza !.kuna mfano unaweza nipa zipo timu mbili tu ndo zinaendesha ligi mfano kama kwetu
Spain Barca na Madrid.
Germany Bayern peke yake.
 
Spain Barca na Madrid.
Germany Bayern peke yake.
Huwezi kuona Barca, Madrid au Bayern akishangiliwa zaidi akiwa ugenini kuliko timu mwenyeji na hii ndio tofauti na hapa kwetu.
Kiukweli simba na yanga hazijawahi kucheza ugenini mechi za ligi kuu au FA, maana kila mkoa wanakoenda wanakuta mashabiki wao wamejaa kuliko timu mwenyeji.Nchi nzima tunashabikia timu mbili tu za simba na yanga.

Huwezi kuona Barca ina mashabiki wengi nyumbani kwa Real Betis. Pia Real betis ikicheza na levante mashabiki wakutosha wanakuwepo.Ila kwetu sasa, derby ya mbeya city vs mbeya kwanza inakosa mashabiki wakutosha ila Mbeya kwanza vs yanga mashabiki wa kutosha wanakuwepo na wengi wakiwa wanaishangilia yanga.

Yaani mwenyeji wa Namtumbo anaipenda zaidi yanga au simba kuliko Namtumbo united, ulaya haipo hiyo.
 
Soka limegubikwa na usimba na uyanga sana...
 
Yaani ukweli mtupu na ili mpira wa Tanzania ukue lazima Yanga na Simba zishuke daraja. Nakumbuka ezi za Nyota Nyekundu na Costal union tanga , pamba Mwanza Lipuli Mbeya Majimaji Songea Kurugenzi na cda Dodoma Balimi na Coffee Bukoba Pan African Dar na timu nyingine nyingi zilikufa kwa ajili ya Yanga na Simba
 
Umewaza mbali sana. Usimba na uyanga unadumaza soka la Tanzania. Wawekezaji wamejikita kwenye timu mbili ambazo ni yanga na simba, hapa tusitegemee ushindani.

Kwa upande wa Azam na hela zao lakini hawafanyi vizuri, tatizo nini?
Tatizo hizi timu zinaingizwa hadi kwenye siasa, na hili ni tatizo kubwa. Wanasiasa wanachukulia hizi timu katika maslahi yao na wateja wao ambao ni mashabiki wa simba au yanga tu.

Ni ngumu sana kwa vilabu vingine kuwa na nguvu kwakuwa siasa ina nafasi na historia kubwa sana kwenye ustawi wa vilabu hivi.

Ili tufanikiwe kutoka kwenye club mbili hadi nne au tano zenye nguvu zaidi, kuna haja ya kupunguza siasa kwenye mpira.

Timu kama AZAM, nadhani ina kila sababu ya kuwa giant kwenye ligi yetu, lakin utaona pamoja na fedha, Facilitiea na mipango mizuri waliyo nayo, bado wana sua sua kwenye mpira wetu, ubingwa kwa zaidi ya miaka 70 upo kwenye mikono ya timu mbili tu.

Tunahitaji kuwa na timu strong walau nne hadi tano, ambazo zitakuwa zinabadilishana ubingwa kulingana na maandalizi yao, na ili hili lifanikiwe, TFF ianzishe mikakati ya kuinua walau timu mbili au tatu zije kushindana na simba na yanga (note, ninafahamu kazi ya TFF lakini, wao wana sehem kubwa ya kuimarisha vilabu kupitia serikali)

Siasa ni adui mkubwa sana wa mpira wetu,.
 

Shukurani sana kwa ufafanuzi mkuu
 
KENYA wamezidhoofisha GOR mahia na AFC Leopards wamefika wapi?SIMBA na YANGA ndio wanachangamsha mpira wa nchi hii...Mpira wetu sisi ni wa mdomoni tu tukitaka kufanikiwa kama Taifa ni kujenga academies nyingi nchi nzima zizalishe wachezaji watakaokuwa na fikra za kucheza mpira nje....Hizi Simba na Yanga zina umuhimu wake pia coz mpira bila ushabiki haunogi
 
Hao wachezaji watakao toka kwenye hizo academy, wote watasajiliwa na simba au yanga?

Kiufupi ni hivi mkuu, hata hizi timu nyingine si kwamba zinawachezaji wabaya! ukitaka kuthibitisha hili, angalia mwenendo wa ligi yetu mpaka sasa na nafasi ya waamuzi katika kuamua matokeo.

Hata tuwe na academy 100, bado Usimba na uyanga utaharibu mpira wetu!

Kikubwa ni kutoa siasa, hii itasaidia sana!
 
Dawa ni kunyanyua timu nyingine zifike level ya simba na yanga...kama Congo walivyoinyanyua tp mazembe.....south mamelodi sundown
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…