Mpunga unaoingia baada ya kutinga Hatua ya Robo Fainali kati ya Yanga na Simba

Mpunga unaoingia baada ya kutinga Hatua ya Robo Fainali kati ya Yanga na Simba

Mtanzanias

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2021
Posts
1,747
Reaction score
3,725
Ni vizuri pia tukawajuza umate umate utakaoingizwa na hizi timu 2 baada ya kutinga Hatua ya Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho na Klabu Bingwa Afrika, mgawanyo ndio huu;

Yanga: Milioni 820 kutoka CAF + Bilioni 1.5 kutoka wadhamini wao Kampuni ya Haier + Milioni 40 zawadi ya Rais Samia, jumla ni Bilioni 2.36.

Simba: Bilioni 1.5 kutoka CAF + Milioni 45 zawadi ya Rais Samia, jumla ni Bilioni 1.97.

Kupanga ni kuchagua, kila timu inavuna ilichopanda.
 
Kila mtu apambane timu yake iwe Bora, kwa ujinga huu ndo maana vijijini watu hawana maendeleo, wakishajiona wote maskini wanaridhika na Hali zao hakuna anayewaza kujinasua ni kuombeana uchawi tu

Kwa akili hizi na hakika hata Simba na Yanga wakishuka daraja kwa pamoja watu wataona sawa tu, si tumeshuka wote!!!

Mi ni Yanga dam dam ila umeandika upuuzi tu!
 
Kila mtu apambane timu yake iwe Bora, kwa ujinga huu ndo maana vijijini watu hawana maendeleo, wakishajiona wote maskini wanaridhika na Hali zao hakuna anayewaza kujinasua ni kuombeana uchawi tu...
Yanga akuna wapuuzi dizaini yako, usijipendekeze wewe kolo
 
Mdhamini anauhusiano gani na zawadi ya kufuzu kwenda robo fainali?
YANGA; 820MIL, KUTOKA CAF+ 1.5B KUTOKA WADHAMINI WAO KAMPUNI YA HAIER +40MIL ZAWADI YA MAMA SAMIA TOTAL=2.36BIL

Mdhamini wa Simba VISIT TANZANIA ni BURE anatangaza utalii wa nchi sio kwa malipo
 
Mdhamini anauhusiano gani na zawadi ya kufuzu kwenda robo fainali?
Uzi umeuelewa au unatujazia saver tu hapa, umeambiwa pesa ambayo kila timu itaipata baada ya kutinga robo fainali, aijalishi ni kutoka caf, ni pesa inayotokana na vyanzo vyote kuanzia wadhamini wa timu husika.

CAF wenyewe na fedha wanazopewa kama zawadi, mimi sijalenga zawadi za caf peke yake, kuwa muelewa, kama simba anacho chanzo kingine pengine atukijui tunaomba utuwekee hapa ni shingapi na sio blah blah, tunajua michuano ya kimataifa wadhamini wao ni Visit Tanzania basi tuwekee wanawapa shingapi
 
Yanga kwa nini mnapenda attention sana?
Mnapenda kila alilofanya Simba muonekane zaidi?
Ni sawa na mtoto wa tajiri, wenzake wamefaulu wamepata zawadi yeye anaenda kuchota hela ndani, eti wako sawa.
Tena umepatiaaa haswaaaa, [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom