Mpwa usije Mjini. Najua hutanielewa lakini ndo ukweli

Mpwa usije Mjini. Najua hutanielewa lakini ndo ukweli

umetudanganya pakubwa sana

mchele bei ya chini ni 1100, buguruni mnyamani na hata tabata ni 1200.

mbagala kilo ni 1000.

bei max 1800 kwa kilo.

Bei ya gesi tu hapa Dar sio sawa na shinyanga.

Dar biashara zinaenda sana tofauti na mikoani.

Dar ukiwa na sera ya hakuna kulala unaweza ingiza elfu 20 kwa siku shinda sana kariakoo

Dar kutamu bwana, karibuni Dar wapwa!!

Dar ndio imeibeba Tanzania
Usiwadanganye, kuna Mabinti wawili nawajua wamedai talaka wamekuja Dar walipo Hali ni mbaya kuliko maelezo, mwenzao walimuacha kwenye ndoa akawa analeta vurugu ili apewe talaka awafuate Bahati nzuri ukatokea msiba Kwa mume wakaja Dar msibani amekutana na wenzake, karudi huku katulia heshima juu, anawasikitikia tu. Mmoja mwenyeji wake alipofika Ubungo alimzimia simu, mwingine analala chini mlo mmoja kumbe yale aliyoyaona kijijini ilikuwa ni mashamsham ya December [emoji3][emoji3]
 
ppole zao naiman. maisha hayako flat, kila sehem kuna wenye nazo na wasio nazo.

kama hao wadada bado wako Dar naomba uwape namba zangu niwasaidie vibarua hata vya usafi

kuna bar hapa tabata inatafuta wahudumu, wafanya usafi n.k

phone; 0747850270
 
Tunapambana. Anataka aje mjini nimtafutie kazi. Elimu yenyewe ni ya hapa na pale. Ni kidato cha nne. Anajua kusoma na kuandika kwa speed jinsi alivyonambia. Anasema anakuja nimtafutie kazi. Kazi gani? Asije mjini. Sitaki undugu lawama.
Kuna kazi za kufanya usafi kwenye majengo..kukaanga chips..Kusomba kokoto, kubeba Zege..bodaboda. .bajaji..kutembeza Karanga...kupika vitafunwa.. KUUZA MADUKA...

Muache aje mjini apambane.

Wewe unadhani kazi Ni kufanya kwenye kiti Cha kuzunguka na kiyoyozi.
 
Usiwadanganye, kuna Mabinti wawili nawajua wamedai talaka wamekuja Dar walipo Hali ni mbaya kuliko maelezo, mwenzao walimuacha kwenye ndoa akawa analeta vurugu ili apewe talaka awafuate Bahati nzuri ukatokea msiba Kwa mume wakaja Dar msibani amekutana na wenzake, karudi huku katulia heshima juu, anawasikitikia tu. Mmoja mwenyeji wake alipofika Ubungo alimzimia simu, mwingine analala chini mlo mmoja kumbe yale aliyoyaona kijijini ilikuwa ni mashamsham ya December [emoji3][emoji3]
Huo Ni mwanzo ..Mambo yanaweza badilika
 
ppole zao naiman. maisha hayako flat, kila sehem kuna wenye nazo na wasio nazo.

kama hao wadada bado wako Dar naomba uwape namba zangu niwasaidie vibarua hata vya usafi

kuna bar hapa tabata inatafuta wahudumu, wafanya usafi n.k

phone; 0747850270
Ngoja Kwanza wapigike nitawapa wameondoka Kwa waume zao kwa majivuno mno wakijua Dar ukifika Tu bila jasho wala kuhangaika unafikia kula bata [emoji3][emoji3][emoji3]
 
Ngoja Kwanza wapigike nitawapa wameondoka Kwa waume zao kwa majivuno mno wakijua Dar ukifika Tu bila jasho wala kuhangaika unafikia kula bata [emoji3][emoji3][emoji3]
utajipunguzia thawabu tu dada we wasaidie wenzio
 
Meseji uliyonitumia mpwa nmeipata.unasema unataka kuja mjini. Mwaka jana ulisema hivyo nikakueleza kuwa subiri kwanza. Naona unasisitiza nikuelekeze home uje mjini.

USIJE MJINI. hizo picha unazoniona nmepiga na kurusha kule insta asilimia kubwa siyo maisha ninayoishi. Nielewe tu. Huku kazi hamna.makampuni mengi yamefungwa na mengine kupunguza wafanya kazi.

Unafahami bei ya mchele? Huku tunanunua kilo moja tsh 2400-2600. Sukari 2700 kwa kilo. Maharagwe tsh 2600-2800 kwa kilo. Nielewe naposema Usije mjini.

Unasema mbona akina Daimondi wamewini laifu kwa kuimba nawe unataka uje kuimba.maisha hayapo hivyo mpwa wangu. Huku Mjini hakuna raha. Usibabaike na picha za watu instagram na facebook.

Unakumbuka kipindi kile mnamsema yule mtoto wa mzee kubwanga alikuwa anaokota makopo kuwa ni chizi?sasa huku mjini kuokota makopo ni moja ya kazi kwa sasa.

Usilazimishe Mpwa.unaweza ukaja ukaolewa.shauri yako. Unaweza ukaja ukawa Chokoraa. Mimi sitokukaribisha home maana najua tutagombana tu. Kama unakuja njoo kwa issues zako mwenyewe.

Ila nakwambia kama hujajipanga USIJE MJINI. watakuoa maisha yakikugonga nawe unataka maisha mazuri.maana naona hata jina umebadilisha unajiita Chidman badala ya Rashid.

Wewe nisubiri ntakuja huko huko tupange jinsi ya kufanya kilimo. Mjini hakuna issue.huwa hatuwaambii tu tukija kuwatembelea. Tunakuwa tumejipanga mwaka mzima.sasa nyie mkituona tumekuja krismasi na magari na nini na nini mnadhani ndo maisha yetu ya kila siku. Nakusisitizia mpwa USIJE MJINI
Kwa nini watu mnapost pictures fake mitandaoni? Mimi hilo ndio jambo silielewi kabisa
 
Back
Top Bottom