Mr. Kuku afikishwa Mahakamani akikabiliwa na mashtaka saba ikiwemo kufanya Biashara Haramu ya Upatu kwa kukusanya bilioni 17

Mr. Kuku afikishwa Mahakamani akikabiliwa na mashtaka saba ikiwemo kufanya Biashara Haramu ya Upatu kwa kukusanya bilioni 17

Huu msemo nauelewa sana toka nimeanza kuuona humu JF!
Yap ukiulewa huu msemo hakika huwezi ingizwa chaka kirahis rahisi, mtu anakuambia biashara fulani au issue fulani inalipa wewe kichwa kichwa unaweka fedha Bro no usifanye hivyo
 
Mwanangu kanipigia simu mda si mrefu. Nilimrushia hio clip! Ameshusha pumzi ya nguvu maana aliweka 3.5M...Nilichomjibu ni kuwa hio hela itafanyia shughuli za kizalendo kujengea barabara na mashule so asiwe na wasiwasi! Iko katika mikono salama.

Amejifariji kwa kusema in business kuna ku win na kujifunza.
Da! Pole yake aisee ni DECI nyingine hiyo huyo ni mdogo wake
 
Kuna jinsi hela inakuwa chungu halafu unasikia kuwa hazirudi huku ukiwa na tumaini kuu kuwa hela utazivuna.

Sikuwahi kuelewa jinsi ya kuvuna wale kuku..nilieleweshwa sana siku hiyo nyumbani lakini wapi.

Kweli maisha ni akili..raha alizokula bro huyo toka 2017.Sasa kwa mfano tu hapo wakatia tia maneno akatoa za uchaguzi kama b10.
B7 akaachiwa then sisi tuliowekeza kuku wetu wa Kidigital tukatangaziwa jamaa amefilisiwa nani atajua?

Kwa sababu huyo jamaa unajua anaweza kuchangia kujengwa kwa Steigler Gorgee kule..au hata akachangia kujenga SGR kipande kidogo tu.
Nchii hii hela zipo na kuna namna tu

Wazee wenzangu wa Mzigo wa kubet twendeni zetu..Kuna Man U leo...kule Inter..
Kweli aisee jamaa kwa level yake aliyofikia anaweza kubargain nao tu.
Hao serikali shida yao ni pesa tu hakuna kingine
 


Mfanyabiashara, Tariq Machibya (29) maarufu kama Mr. Kuku, amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, akikabiliwa na mashtaka saba likiwemo la kufanya biashara ya haramu ya upatu kwa kukusanya fedha za Umma zaidi ya Tsh. 17 bilioni.

Machibya ambaye ni mkazi wa Oysterbay amesomewa mashtaka yake leo 10/08/2020 na Wakili wa Serikali muandamizi mbele ya hakimu mfawidhi wa mahakama hiyo Godfrey Isaya. Akisomewa mashitaka yake, mshtakiwa anakabiliwa na kesi ya Uhujumu Uchumi na 60/2020, kati ya mashitaka hayo 7 yapo ya kusimamia na kuendesha biashara haramu ya upatu, kupokea maingizo ya fedha za umma bila ya kuwa na leseni na kutakatisha fedha.

Mfahamu zaidi Mr. Kuku:
Mr. Kuku Farm ni aina mpya ya DESI?
Fahamu zaidi kuhusu Mr Kuku

Pamoja na yote same date mlitohowa taarifa yangu na kutengeneza taarifa same date. Hakuna jipya nili andika as alert
 
Nikiikumbuka nilivyoliwa pesa na forex nabaki kusema bongo ukifa njaa umejitakiamwenyewd wajinga tupo kwa mamilioni.
NB: nawaonea huruma wastaafu walioweka pesa huko
boss msaada kidogo alikua anafanya vp hiyo shughul huyo m
Mr Kuku??...
 
Back
Top Bottom