Mr. Kuku afikishwa Mahakamani akikabiliwa na mashtaka saba ikiwemo kufanya Biashara Haramu ya Upatu kwa kukusanya bilioni 17

Mr. Kuku afikishwa Mahakamani akikabiliwa na mashtaka saba ikiwemo kufanya Biashara Haramu ya Upatu kwa kukusanya bilioni 17

Hakuna namna aisee...Hakimu akili mil 50 tu anatulia!! Anaweza kuhonga wanaohusika na kesi mil 50 wote na akabaki na Mpunga wa maana.. Hii kesi za upatu ni kama kubet jackpoint tu
Sema mamlaka zinashtuga zikiwa zimechelewa. Mtu kashawaliza watu bil 17 ki uhalisia ni kwamba waliolizwa hawawezi kurudishiwa ila pia hamna jinsi unamfunga mtu mwenye B17
 
Mimi nahisi serikali wanafanya maksudi yaani kamali linaenda wee wanaliacha.Mpunga ukishajaa pomu wanaushukia kama mwewe na kuutaifisha.Poleni vibua kwa kung'ata ndoano ya pyramid business.
Mbwa kamkosa mnyama kang'ata chuma cha reli[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Tuliwaambia kudadeki zenu
Mr kuku ni Ontario aliechangamka
20200711_060626.jpg
 
Mwanangu kanipigia simu mda si mrefu. Nilimrushia hio clip! Ameshusha pumzi ya nguvu maana aliweka 3.5M...Nilichomjibu ni kuwa hio hela itafanyia shughuli za kizalendo kujengea barabara na mashule so asiwe na wasiwasi! Iko katika mikono salama.

Amejifariji kwa kusema in business kuna ku win na kujifunza.
Dah ali invest mazima dadeki. Hv wabongo mbona tu wagumu hv kujifunza.Toka DECI,D9 lakin bado raia wananasa kila mtego tu.Pole zake jamaa.Kesho atakuwa wise kwenye uwekezaji wake.
 
Hakuna pesa ina patikana kirahisi hata siku moja easy come easy go, case closed. Walio panda huu ndio uwe.uzi wa mwisho tafadhali wasije tujazia thread za vilio huku plz
 
Duh, hii ndio bongo! Hatimae jibu limepatikana, kwa mnaokumbuka nilileta bandiko kuulizia uhalali wa ile biashara. Michango ilikuwa ya kutosha but all-in-all bwana alitoa na bwana ametwaa!!!
nimecheka kinoma
 
Watanzaniawengi ni kama Kenge, hawasikii ila damu ikitoka ndio wanashtuka.

Nilionya sana kuhusu hii fursa ila kwa wapenda vya dezo wakawa wanaona tunawabania.

Safi sana.
 
Wabongo tutulie huyo ni mtuhumiwa tusubirie hukumu
 
Kuna jinsi hela inakuwa chungu halafu unasikia kuwa hazirudi huku ukiwa na tumaini kuu kuwa hela utazivuna.

Sikuwahi kuelewa jinsi ya kuvuna wale kuku..nilieleweshwa sana siku hiyo nyumbani lakini wapi.

Kweli maisha ni akili..raha alizokula bro huyo toka 2017.Sasa kwa mfano tu hapo wakatia tia maneno akatoa za uchaguzi kama b10.
B7 akaachiwa then sisi tuliowekeza kuku wetu wa Kidigital tukatangaziwa jamaa amefilisiwa nani atajua?

Kwa sababu huyo jamaa unajua anaweza kuchangia kujengwa kwa Steigler Gorgee kule..au hata akachangia kujenga SGR kipande kidogo tu.
Nchii hii hela zipo na kuna namna tu

Wazee wenzangu wa Mzigo wa kubet twendeni zetu..Kuna Man U leo...kule Inter..
Kwa mujibu wake mwenyewe, April mwaka huu alisema biashara yake ina thamani ya approximately over Bilioni Moja. Kwa kutumia common sense - Hiyo Bilioni 17 ni mahesabu ya kisheria ya pesa zote zilizopita mikononi mwake tangu mwaka 2017. Huenda pesa aliyonayo benki kwa sasa haifiki Bilioni 1!!!

Mr K.PNG
 
Back
Top Bottom