Mr. Kuku afikishwa Mahakamani akikabiliwa na mashtaka saba ikiwemo kufanya Biashara Haramu ya Upatu kwa kukusanya bilioni 17

Mr. Kuku afikishwa Mahakamani akikabiliwa na mashtaka saba ikiwemo kufanya Biashara Haramu ya Upatu kwa kukusanya bilioni 17

This how they did...Huyu hata 1B hajawahi ishika kwa mkupuo

ila serikali kwakujua kujiongeza wakamjumlishia,wakazidisha mwsho

wakamgawanyia kwa mbili wakatoa nane,wakapata jibu ni 17B,***** zao.
😂😂😂😂
 
Watu kama hawa ni potential sana, wabunifu na wathubutu ni wa kuwasapoti na si kuwafunga.

Eti wao wenyewe wezi vile vile! [emoji1][emoji1][emoji1]
Unajua kuna vitu mjini hapa basi tu.

Mbinu za jamaa ni kama wale miamba ya pale Ubungo.
Bus unaziona kabisa unasikia hilo halina AC njoo kwenye hili hahaha ile unakimbilia hilo lenye AC unakuta kavu kavu
 
Inaruhusiwa mkuu ila inabidi uorodheshe kwenye DSE na ukidhi vigezo na msharti ya benki kuu.
Sasa kama upatu ni sio haramu kwanini hii taarifa inakuza msamiati huu "Akiwa anaendesha upatu" mpaka mentally ukimuuliza mtu upatu ni nini atasema utapeli, kwaninj wasiseme "akiwa anaendesha Biashara bila leseni.

Kuna vitu vinakera.
 
Ivi kutakatisha pesa ni nn??????
Ni kujihusisha moja kwa moja au kwa njia nyingine katika kubadili, kuhamisha, kuficha, kupoteza chanzo, kutumia au kujipatia fedha au mali inayoaminika kupatikana kwa njia haramu.

Ili fedha iweze kutakatishwa inapitia kwenye hatua tatu, ambazo ni:

Hatua ya kwanza, Mpitisho (placement)
Fedha iliyopatikana kwa njia ambazo ni haramu inawekwa au kuingizwa katika mfumo wa kawaida wa fedha kuipitia taasisi za kifedha kama benki.

Hatua ya pili, Mtawanyo (Layering)
Hapa mtu anaficha ukweli wa chanzo cha fedha ili kumpa mazingira magumu yeyote anayefuatilia chanzo cha fedha. Katika hatua hii fedha zilizowekwa benki zinatawanywa katika akaunti mbalimbali aidha kwenye benki moja au benki mbali mbali kwa kufanya miamala mbalimbali tena mingi ili tu kuleta ugumu wa kufatilia miamala hiyo.

Hatua ya tatu, Mwingiliano (Integration)
Fedha zile chafu ambazo ziliwekwa benki zinatolewa na kufanyiwa shughuli halali za kimaendeleo hivyo pesa itakayopatikana kwenye shughuli hiyo itakuwa safi na halali kisheria, mfano fedha ya madawa ya kulevya iliyokuwa benki ikitolewa na kununulia basi la kusafirisha watu kwenda mikoani, mapato kwenye basi hilo ambayo ni nauli yatakuwa halali.

Hii ndio maana ya kutakatisha pesa. Dizaini nimewafokea eeh!!?😂😂😂
 
Kipindi yeye ananunua ilikuwa bei ndefu kidogo kama 120m na akalipia 5m Plate Number.

Ila kwa sasa ukiwa na 70m unavuta X6.
Tuje kwenye kilimo mbona juzi kuna mkulima kapata 600M yule wa Avocardo.
 
Wanajidanganya hakuna mwanasheria yeyote atakayeshinda hii kesi , kosa la kwanza ni kuendesha upatu kukusanya fedha bila kuwa na kibali/leseni kwahiyo hapo anaangukia kwenye utakatishaji fedha,watu wanasema sijui analipa kodi mara bla bla ,anaweza akawa analipa kodi kama mfanyabiashara wa kuuza kuku kama kampuni alivyoisajili ila kodi kwa ajili ya kufanya upatu halipi.

Ili kukusanya fedha kwa watu kama wafanyavyo bank ilitakiwa atafute leseni ya kufanya hivyo hapo ndipo kosa lilipo,jamaa ataozea ndani,hatoki leo huyo na utakatishaji pesa.
Kuna bush lawyer wanajipa moyo eti kesi nyepesi atatoka 😆😆😆
 
Kinachofanya ushinde sio wingi/uzito wa tuhuma mkuu,ni case proceedings(mwenendo wa kesi).Kina rugemalila walipewa tuhuma kibaao mwanzo ila kadri muda unavyoenda zina drop moja moja tu,mwisho serikali ikaomba plea bargain...Unawakumbuka wale jamaa wa EFD walikuwa wanapiga 7M per day?,Sidhani kama wapo gerezani sasa hivi..Plea bargain.
Huenda mkuu, mie sio mwenyeji kwenye uwanda wa sheria.
 
Hela jinsi unavyozipata utamu unaongezeka kuzitafuta zaidi. Pia kama ni kuexit labda kuepuka tu mkono wa dola ila asingeweza kutoka na huo mpunga wote. Cha muhimu kama alijua ni kitu haramu anafanya angestop baada ya kufika point flani na kusepa mapema.
Hahahahah shida ni kwamba nina hakika 100% jamaa alikuwa hajui kwamba amekiuka taratibu. Mwanasheria wake ndio wa ku blame maana ndio alimtia ujinga.
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]Daah msalaa sanaa...!! Huyu jamaa kazikusanyaa hasaa alafi ukute hakumshirikisha mumewee noma sana kuna Aunt yangu Desi ilipokufa ilikuwa Mwanzo wa Presha hadi leo hajakaa vizurii...
kumbe hata wewe legendary ulishatwaliwa na wajanja.... 😂 😂 😂 😂 😂
 
Back
Top Bottom