Papaa Mobimba
JF-Expert Member
- Jan 27, 2018
- 882
- 3,337
Mahakama ya Hakimu Mkazi, imemhukumu mfanyabiashara Tariq Machibya maarufu Mr Kuku, kulipa faini ya sh. milioni tano au kwenda jela miaka 5, baada ya kutiwa hatiani kwa makosa mawili ambayo ni kujihusisha na biashara ya upatu kwa kukusanya fedha kutoka kwa umma na kukubali kupokea miamala ya fedha bila ya leseni.
Katika hukumu hiyo, Mr. Kuku amehukumiwa kulipa faini ya Tsh. Milioni 2 au kifungo cha miaka 5 na katika kosa la pili ametakiwa kulipa faini ya Tsh. Milioni 3 au kifungo cha miaka 5. Ikiwa atashindwa kulipa faini, vifungo ni vyote kwa pamoja
Pia mahakama hiyo, imemuamuru fedha sh. bilioni 5.4 ambazo ziko benki ya CRDB kwenye akaunti ya mshtakiwa huyo kwenda kwenye akaunti ya Mkurugenzi ya Mashitaka nchini( DPP) iliyoko benki Kuu ya Tanzania( BoT).
Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu Mkazi Mfawidhi Godfrey Isaya, baada ya upande wa jamhuri kuingia makubaliano ya kulipa kiasi hicho.
Akisoma hukumu hiyo Hakimu Isaya, alisema mshtakiwa anamtia hatiani kama alivyoshitakiwa ambapo mshitakiwa ameshindwa kulipa fedha hizo na alipelekwa rumande.
Pia soma

- Mr. Kuku Farm ni aina mpya ya DESI?
- Fahamu zaidi kuhusu Mr Kuku
- Wadau na wajasiriamali, naomba kujuzwa kuhusu Mr. Kuku Farms na uhalisia wa aina ile ya biashara
- Mtaalam wa kuwekeza kwenye kuku tayari ameshawaliza
- Mr. Kuku afikishwa Mahakamani akikabiliwa na mashtaka saba ikiwemo kufanya Biashara Haramu ya Upatu kwa kukusanya bilioni 17
- Wajasiriliamali wa Tanzania tuna lipi la kujifunza kutokana na makosa ya kiufundi / kitaalam ya Mr. Kuku