Mr. Kuku ahukumiwa kulipa fidia TSh. Bilioni 5.4, faini Tsh. Milioni 5 au jela miaka 5

Mr. Kuku ahukumiwa kulipa fidia TSh. Bilioni 5.4, faini Tsh. Milioni 5 au jela miaka 5

Someni muelewe vizuri ni kwamba ameshakubaliana na DPP. Kwa mfumo mpya wa Plea Bargain

Wameshaangalia kwenye akaunti ana 5.4billion wamekubaliana unakiri kosa tunazichukua hizi halafu tunapunguza mashtaka

So 5.4 ya FIDIA washachukua
Halaf wanakupa adhabu ndogo ya FAINI ya million 5 au Jela miaka mi5

So wameshampukutisha kila kitu dogo hadi hiyo mil5 kashindwa kulipa kaenda rumande
Duuh noma kweli rafiki angu!!! Wangemuacha tu huyu chalii maana hiyo m5 ni kama wemkomoa tu coz wanajua kabisa hana kibunda chote wamelamba dadeki
 
Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu imemhukumu mfanyabiashara, Tariq Machibya (29) maarufu Mr. Kuku kulipa fidia ya Sh5.4 bilioni baada ya kupatikana na hatia ya kushiriki biashara ya upatu na kukubali kupokea miamala ya fedha.

Pia, imemhukumu kulipa faini ya Sh5 milioni au kwenda jela miaka mitano sambamba na kuamuru Sh5.4 bilioni zilizopo kwenye akaunti ya mshtakiwa huyo kuhamishiwa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kwenye akaunti ya mkurugenzi wa mashtaka (DPP).

Hata hivyo, mshtakiwa ameshindwa kulipa faini na kurejeshwa rumande.

Mahakama imetoa hukumu hiyo baada ya kumtia hatiani katika mashtaka mawili ya kushiriki biashara ya upatu na kukubali kupokea miamala ya fedha baada ya kukiri mashtaka yake DPP.

Uuamuzi huo umetolewa leo Jumatano Desemba 16, 2020 na hakimu mkazi mfawidhi, Godfrey Isaya.

Awali, wakili wa Serikali mkuu, Paul Kadushi akisaidiana na wakili wa Serikali mwandamizi, Wankyo Simon amedai kuwa kesi hiyo imeitwa kwa ajili ya kusomewa mashtaka baada ya mshtakiwa huyo kukiri mashtaka yake kwa DPP baada ya kufanya majadiliano naye na kufikia makubaliano Desemba 7, 2020.

Amesema baada ya kufikia makubaliano na DPP amemfutia mashtaka manne kati ya saba yaliyokuwa yanamkabili.

Mashtaka aliyotiwa hatiani ni kusimamia biashara ya upatu na kupokea miamala ya fedha kutoka kwa umma bila kuwa na leseni.

Kati ya Januari 2018 na Mei 2020 katika maeneo mbalimbali ya jijini Dar es Salaam mshtakiwa anadaiwa kusimamia biashara ya upatu.

Machibya anadaiwa alijihusisha na biashara ya upatu kwa kukubali na kukusanya fedha kutoka kwa umma, akijifanya kwamba watafanya ujasiriamali wa ufugaji wa kuku na wangepata faida ya asilimia 70 ya mtaji wa awali waliowekeza kwa miezi minne na asilimia 90 ya mtaji wa awali waliowekeza kwa kipindi cha miezi sita, kiasi ambacho ni kikubwa katika biashara kuliko mtaji uliokusanywa.

Shtaka pili, siku na maeneo hayo mshtakiwa anadaiwa kuwa alikubali na kupokea miamala ya fedha za umma kiasi cha Sh17 bilioni bila kuwa na leseni.

Mwananchi

Pia soma

Fine ipo sawa na kiasi kilichopo kwenye accounts zake [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mzigo unakwenda na anatakiwa alipe nyingine.
Labda mleta mada kakosea kuandika
Hicho kiasi cha 5.4 bilioni kilichopo kwenye acc ya mshtakiwa ambacho kinahamishiwa kwenye akaunti ya DPP ndio faini yenyewe au ndio kutaifisha faini ipo palepale?
 
Saa kashindwa vipi wakati kwenye account yake kulikuwa na bilioni 5?.
Si wangezichukua alafu wamuachie
Hio ni FIDIA faini kashindwa kulipa ndomaana kaenda jela.

Mtu alikuwa na bil5.4 ila kashindwa kulipa mil5

Hahahaaa raha sana saivi yani wanakwangua kila kitu
 
Mr kuku leo hii ameshindwa lipa faini ya 5million?
Hata kama wamepita na hizo za kwenye account,inamaana hakua na upande wa pili ...
Ubaya ni kwamba alikua na makosa ya sh bil 17 so kwa muda wote huu wako wananegotiate ni pamoja na kuuza kila kitu alichonunua kwa hiyo hela. Ndio wamebahatika kupata hiyo bil 5.4

Wakaona sasa inatosha hakuna kitu tena alichoficha basi mnakubaliana wanazikwapua

Suala la Million 5 wanaacha upambane nalo mwenyewe huko na ndugu zako. Dogo kakosa hio hela sahizi karudi kulala na nyapala. Kulala kugeuka kwa filimbi
 
Back
Top Bottom