Mr. Kuku ahukumiwa kulipa fidia TSh. Bilioni 5.4, faini Tsh. Milioni 5 au jela miaka 5

Mr. Kuku ahukumiwa kulipa fidia TSh. Bilioni 5.4, faini Tsh. Milioni 5 au jela miaka 5

Aisee,bora asingekubali,maana unatoka jela unaanza moja du!
Lazima ukubali kwakuwa mashtaka yale waliyopunguza ni kwamba angekua tu jela indefinitely kama kina Ruge waliogoma kuplea

Bora sahivi anajua ana options miaka 5 sana sana atakaa mi3 anatoka au anajua ndugu zake watapata hiyo mil5 wanamlipia anatoka halafu kijana bado anarudi anaanza arifu kwa ujiti
 
Kwahio hio pesa ikichukuliwa na jamuhuri itawapatia waathirika wa huo upatu au ndio watakua wameshiriki kwenye ujenzi wa taifa?
Jamhuri ipi ya kukupa hela? Hio ni ya ujenzi wa taifa la wadanganyika.
 
Sisi Watanzania bhana!Ina maana hadi leo hujui lengo la serekali/lengo la hiyo sheria?Nia ya serekali ni kukusanya mshiko mkubwa kutoka kwa watu wenye hela ndefu na wala siyo kulinda sheria.Sasa hao wa forex wana hela gani ambazo ni significant kwa serekali?Yaani DPP apoteze muda wake kupambana kukusanya hela kwa mtu mwenye million sijui nne au moja?DPP amepewa jukumu maalum la kukusanya hela kutoka kwa watu wenye hela ndefu,yaani kama wewe ni bilionea Tanzania siyo sehemu salama kwa sasa!
OK ndio maana upatu wa kuchangishana elfu 5 huku mtaani hata wakizulumiana wanakwenda polisi na wanasikikizwa wakati ilitakiwa wakifika polisi wawekwe lockup
 
Kumbe dogo tu, pongezi kwake mr kuku
 
Hivi ni kweli jamaa aliweka pesa zote bank?? Hakuna pesa ata alozichimbiaa chini ya ardhi?? Angeweka mpunga bitcoin huo hakuna wa kuusitisha wala ku freeze angepeta sana
 
Choice aliyopewa ni alipe faini ya 5million au jela 5years
Hiyo 5billion ya fidia kuilipa ni lazima;Bila kujali aende jela asiende ndomaana account zake wamezifreeze
Hiyo 5.4 billioni ameshailipa kwa kitendo cha mahakama kuamuru kiasi hicho kihamishiwe kwenye account ya DPP
 
Ndio pesa imeingia BOT?
Choice aliyopewa ni alipe faini ya 5million au jela 5years
Hiyo 5billion ya fidia kuilipa ni lazima;Bila kujali aende jela asiende ndomaana account zake wamezifreeze
 
Hizi kesi sa kukubali mashitaka na kulipa fine ni mbinu za kuibia watu pesa.

Binafsi mpaka leo sijaelewa kosa la mr kuku. Maana kama mradi ulikuwa active na watu wanawekeza kwa free consent sasa kosa lipo wapi?

Leseni
 
Hakuwa na leseni
 
Swaga za sahivi unakaa chemba na DPP mnakubaliana zihamishwe kwenda BOT
 
Miradi mikubwa ya kimkakati lazima itakamilika kwa style hii, freeze account, kubali na DPP yaishe
 
Back
Top Bottom