Mr. Kuku ahukumiwa kulipa fidia TSh. Bilioni 5.4, faini Tsh. Milioni 5 au jela miaka 5

Mr. Kuku ahukumiwa kulipa fidia TSh. Bilioni 5.4, faini Tsh. Milioni 5 au jela miaka 5

Hiyo pesa waliyoichukua 5 billion + na kuihamishia BoT ni pesa waliyotapeliwa watu. Inaonekana watu wengi wamepigwa sana hapa.
Kifupi watanzania wengi wanapenda mteremko kitonga. Akitokea mjanja mwingine lazima wapigwe maboya wengine. Kweli wajinga hawaishi.
 
Faini ya milion tano sio kwamba hana ila akiitoa haraka haraka watamshtukia huyu jamaa pesa bado anayo ni mwendo wa kucheza na akili za watu tu
 
Hizi kesi sa kukubali mashitaka na kulipa fine ni mbinu za kuibia watu pesa.

Binafsi mpaka leo sijaelewa kosa la mr kuku. Maana kama mradi ulikuwa active na watu wanawekeza kwa free consent sasa kosa lipo wapi?
Kosa ni kutaka kuwa tajiri haraka
 
Ninawaelewa sana Wachina, pesa yao wana lala nayo ndani. Hakuna bank manager atakae jua balance halisi ya Mchina.
Kuna wachina walikamatwa Morogoro wakiwa na 200M ndani, pesa za Mabonanza.

Kwa ujinga kama huu ndio maana kina Manji walikuwa wanatunza pesa zao Uswisi.

Laiti kama Manji angekuwa anaweka pesa hapa, angepitia hali ngumu sana na umasikini wa kutisha.
 
Zinaitwa pyramidal scheme, ni kosa kisheria kuendesha shughuli hizo. Haijalishi watu wamehiyari au lah.
Hakuna lolote ni wivu na kuona watu wamebuni namna ya kuendesha miradi huku wakisaka wawekezaji wadogo
 
Hii sheria ni aidha haina sifa za kuwa sheria au inakuwa-abused. Haifai kabisa, haina staha na inajenga taswira kuwa imelenga kupora watu hela zao

Sent from my SM-J530F using JamiiForums mobile app
Yaani sijui tunaishi nchi gani. Baada ya jamaa kuzinguliwa soko la kuku liliyumba sana. Yaani wameua mradi mkubwa ambao huko mbele huenda ungekua na manufaa. Tatizo wivu watanzania tukiona mtu katoboa bila sugu mikononi tunaanza kuita wizi na majina mengine yasiyofaa.
 
Ila jamaa mr kuku ni mbunifu,serikali wangekaa nae chini wamtumie awabunie mradi mwingine wa kuiingizia hela serikali,Huyu jamaa Anko Magu anamfaa katika sekta ya ubunifu wa vyanzo vya mapato
Ni mtu wa kuthubutu. Anakua na business plan halafu anaalika wawekezaji wadogo. Wangeweka usimamizi mzuri ingefaa kuliko kumfilisi
 
Sisi Watanzania bhana!Ina maana hadi leo hujui lengo la serekali/lengo la hiyo sheria?Nia ya serekali ni kukusanya mshiko mkubwa kutoka kwa watu wenye hela ndefu na wala siyo kulinda sheria.Sasa hao wa forex wana hela gani ambazo ni significant kwa serekali?Yaani DPP apoteze muda wake kupambana kukusanya hela kwa mtu mwenye million sijui nne au moja?DPP amepewa jukumu maalum la kukusanya hela kutoka kwa watu wenye hela ndefu,yaani kama wewe ni bilionea Tanzania siyo sehemu salama kwa sasa!
Nasubiri nini kukimbia nchi

Yaani niwe na Bl-5 katika acc zangu za bank then niendelee kuishi Tanzania nitakuwa nimerogwa au!? Kichaa?
 
Yaani sijui tunaishi nchi gani. Baada ya jamaa kuzinguliwa soko la kuku liliyumba sana. Yaani wameua mradi mkubwa ambao huko mbele huenda ungekua na manufaa. Tatizo wivu watanzania tukiona mtu katoboa bila sugu mikononi tunaanza kuita wizi na majina mengine yasiyofaa
Biashara yake ilikuwaje.. naomba unipe ABC zake
 
Pamoja na hivyo dogo alitumia akili nyingi sana kuweza rubuni watu wote hao
 
Back
Top Bottom