Mr. Kuku ahukumiwa kulipa fidia TSh. Bilioni 5.4, faini Tsh. Milioni 5 au jela miaka 5

Mr. Kuku ahukumiwa kulipa fidia TSh. Bilioni 5.4, faini Tsh. Milioni 5 au jela miaka 5

Kwahio hio pesa ikichukuliwa na Jamuhuri itawapatia waathirika wa huo upatu au ndio watakua wameshiriki kwenye ujenzi wa taifa?
Kwa serikali gani? Umesahau ishu ya desi?
 
Mkuu kuna mtu kam mandela alifungwa miaka 27 na hakupoteza ndo iwe iyo miak mitani au kumi??
Ya mungu mengi mkuu
Mkuu Mandela ana stori tofauti kabisa.

Anyway sisemi kupotea kiivyo kama atarudi akiwa sawa kisaikolojia. Maana miaka 34 bado anauwezo wa kufanya makubwa tu maana kuna watu wengi wenye umri zaidi ya huo bado bila bila.

Issue ni kukaa sawa kisaikolojia baada ya kutoka huko.
 
Huyo dogo Anawapoteza maboya hakuna mtu mwenyeakili ya kukusanya pesa ndefu Kiasi hicho akakosa akili ndogo tu ya tahadhari ya kuficha pesa kwenye bank za nje. Huyo dogo Bado mpunga anal tena mrefu tu. Huko jela anaweza kwenda ikawa ni setup kwa wahanga.
 
Hebu tu assume hii kesi tungekua hatuijui (wananchi) yani kesi inakua siri kati ya mahakama na mshtakiwa,unadhani mr kuku angehukumiwa? hela aliyokua nayo 5B ni nyingi sana wangeichukua halafu mshtakiwa anaambiwa sepa kwenu katulie.

lakini shida n kwmba kesi kila mtu anaijua na kati ya wanaoijua kuna waliolizwa na mr kuku,kinachofanyika ni kuwazuga walalamikaji/waliopigwa na mr kuku,sasa wanazugwa vipi?

inatolewa hukumu ambayo mshtakiwa hatakiwi kuilipa (kulingana na walivyompanga) anaambiwa atulie maana akiilipa ataonekana ana hela,walalamikaji/waliopigwa wataona mtu wao hajapata anachostahili,hivyo basi Mshtakiwa anajifanya hana hela kbsa anaenda rumande.

akiwa kule baaada ya mwezi anatolewa,kwasababu kwamba kapata mdhamini kamlipia zile 5m,bila kujua hili wala lile walalamikaji wanapishana na mr kuku pale m/city anasukuma kibaiskeli kakijaza mazaga nyomiiiii anaelekea parking alipopaki crown lake.

Hii kitaalamu inaitwaje unajua? inaitwa "danganya toto kula kande mbichiiiii",mr kuku anakula bata zote tangu day 1 waone ana B zakutosha Bank. Nchi hiiiiii jela ina maskini tu,acha mimi nianzishe Mr.Bata yangu ebu
 
Alibaba angekuwa hapa, saa hizi yuko lupango maana hana duka ila anauza bidhaa sio zake, hiyo ni piramidi scheme na uhujumu uchumi mkubwa..
Alibaba hajawahi chukua hela ya Wafanyabiashara.....modal ya biashara yake ni kuunganisha mteja na mnunuzi .investors wamewekeza kwenye biashara yake inayopata faida ,sio upatu wa kukusanya hela za watu na kuwalipa hela zinazokusanywa kwa wengine ok?
 
Hivi hizi habari za kutapeliwa mnazitoa wapi?

Maana hta mashtaka yake hayahusiani na yeye kuwatapeli watu!
Ponzi scheme ni utapeli tu, maana wale wa mwisho lazima wakose watu wa kuingiza na hapo pesa yao ndio imekwenda
 
Kwahio hio pesa ikichukuliwa na Jamuhuri itawapatia waathirika wa huo upatu au ndio watakua wameshiriki kwenye ujenzi wa taifa?
😂 ukidai utashitakiwa kwa kushiriki utakatishaji wa pesa!
 
Kashaachiwa mchana huu
Una mawasiliano yake huyu mtu? Niko interested sana kufanya naye uwekezaji kwa mtaji wangu.

Kuna kitu hakiko sawa, huu ubongo siyo wa kuuwacha ukawa domant, huyu jamaa ni asset ambayo wengi hamuwezi kuamini.
 
Dah aisee jamaa ukimuangalia kwa macho unajiulza maswali hii B.5 ipo?? kwelii
Screenshot_20201217-131159.jpg
 
Back
Top Bottom