Mr. Kuku ahukumiwa kulipa fidia TSh. Bilioni 5.4, faini Tsh. Milioni 5 au jela miaka 5

Serikali ya kiporaji sana hii
Yani fidia anapaswa kulipwa mwathirika serikali ndio wanachukua fedha zote za wananchi?

Sasa kunatofauti gani kati utapeli wa Mr kuku
Na utapeli wa serikali dhidi ya wananchi wake?

Mimi nilidhani serikali ipo kuhakikisha wananchi wake wako salama na hawatapeliwi kumbe wanafungua kesi kwa maslahi yao
Shame on ccm government
 
Mzee wako alikuwa anajali sana siri zake za kibenki lakini akaenda kwa wakubwa serikalini kuwaaambia jamani nina mamilioni ya dola NMB nataka kuyatoa. Wakamuomba azibakize NMB. Sielewi Mzee wako alikuwa anajali zaidi siri zake au kutishia na kubembelezwa na wazee wa serikali badala ya kuzitoa kimya kimya.

Turudi kwenye mada. Kuhusu siri za wateja, hata Ulaya serikali inajua una kiasi gani benki. Nchi za Umoja wa Ulaya unatakiwa kuripoti miamala ya Euro 10,000 na zaidi kama vile depositing, kwa hiyo akaunti, salio, jina, umezipata pataje, una mpango gani nazo, vyote vitajulikana. Hakuna siri. Na wakitaka kuzikwapua watafanya mchakato wa seizure and forfeiture kama DPP, Jeshi la Polisi na Mahakama walivyofanya kwa Mr. Kuku.
 

bank zetu haziko security kabisa BOT wapi wamepata access yakuchukua Pesa zote??
 
You are shaming the government bila kujua all recommendations za DPP??? Imagine kama waathirika wameamua kutofuatilia fedha zao???
 
Mimi naona hujaelewa swali langu, nauliza hivi account yako binafsi mtu mwingine anawezaje kuingia na kuchukua fedha zako. Ina maana bank haziwezi kuzuia?
 
Hela zilikuwa za mkondo wa taasisi ya kiserikali, aliingiliwa kisiasa.

Ama una miss point yangu, ama unajitia ujinga wa makusudi.

Huko nchi za Ulaya na Marekani, kote, serikali inaweza ku garnish hela, hilo si ninalojadili hapa.

Nimefanya kazi kwenye mifumo ya benki ya kimataifa miaka mingi sana naelewa hili.

Tatizo ni due process.

CEO mstaafu wa CRDB, Charles Kimei, aliwahi kusema kimsingi anamuogopa sana Magufuli, na yuko tayari kufanya lolote atakalosema Magufuli.

Hii kauli kwa CEO wa benki ni kauli ya hatari sana.

Maana yake Magufuli anaweza kumwambia waibe hela benki wazipeleke kwenye kampeni za urais, na yeye kwa sababu anamuogopa sana Magufuli akakubali tu. Tafsiri ni kwamba ukiweka hela zako CRDB ya Kimei, ulikuwa unaweka hela katika benki yenye CEO asiye na banking integrity, anaogopa wanasiasa.

Kauli kama hii ikitolewa na CEO wa benki ya Marekani hapo hapo anatolewa kazini.

Huko Bongo hakuna mifumo iliyokomaa ya kitaasisi, hakuna due diligence. Watu wanaweza kukuona una hela nyingi wakakuonea wivu tu wakakutungia kesi ya uhujumu uchumi wakufilisi.
 
Kama aliandikiwa mkataba hana jinsi
 
Dah aisee jamaa ukimuangalia kwa macho unajiulza maswali hii B.5 ipo?? kweliiView attachment 1652190
Don't use both of ur legs kumesha kina cha maji. Never discard a book's content by the "unglittering" appearance of its cover. Siyo vyote vilivyofubaa na kusawijika ni madakata --- zingine ni pure gold nuggets per excellence.
 
Hadithi Alfuleulela
 
Ndo Hakimu ameamua eti kiasi hichohicho ndo kiwe faini, kwa hiyo walitaka tu hela zake...huyo ndo Mzee wa Chato, asikuone una sh.100 bank...anapita nayo!
Hukusoma kwamba hukumu ilipunguzwa??? Kumbe ulitaka adaiwe 29B??? Yaleyale ya Mbunge Nusrat na gereza!!!
 
Documents, legal papers!?? Wacha maneno, weka mziki
 
Wakinga wanaweza tena unazikuta kwenye ndoo chakavu huwezi kutabiri. Hata wakisafirisha unamkuta mwanaume amevaa ndala miguu imepauka amebeba kapu kumbe na ndani lina nguo chakavu. Kumbe ndani ya nguo kuna milioni 50.
Unatusema vibaya. Tuna magari pia hatutembei kwa miguu tuu.
 
What if alishauriwa akawa hard-headed??? Naona unakandia serikali huoni the other side of the fence.
 
Alibaba angekuwa hapa, saa hizi yuko lupango maana hana duka ila anauza bidhaa sio zake, hiyo ni piramidi scheme na uhujumu uchumi mkubwa..
Yule ni dalali. Anaunganisha wauzaji na wanunuzi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…