Mr. Kuku ahukumiwa kulipa fidia TSh. Bilioni 5.4, faini Tsh. Milioni 5 au jela miaka 5

Huyu jamaa ni raia wa Tanzania?
Kama ni Rais na aliweza kukusanya hizo bilioni za fedha sio wa kuchukulia poa
Wazo lake lingechunguzwa kama lina msaada kwajamii na aelekezwe kufata Sheria na taratibu watu wapate ajira
 
Eti mwizi aliyekamatwa kaonewa kwa vile wezi wengine hawajakamatwa? We ulisikia wapi?

Yawezekana hao akina Q Net ni wajanja na wamezingatia sheria zote husika. Nasikia makampuni haya yameandikishwa kihalali na ukiangalia mikataba yao imekaa kijanja sana. Hata ukiwakamata mahakamani waweza ishia kuangukia pua. Sana sana ni kufuta usajili wao na kuwafukuza nchini.

Mambo ya kisheria kamwe hayaongozwi na hisia wala mihemko kamanda !!!
 
Sioni Kama kashindwa kulipa watu wamechukua hela yote ya kwenye akaunti yako hata wangesema laki tano kwa siku kadhaa angeenda ishu ya wao kufunga akaunti yako sio Jambo dogo...
 
Kumbe mpunga walisepa nao? Hapo sasa tatizo
 
Na ana mke na watoto sasa ndio ubaya, auze ile Jaguar F-Pace ya 2018
Mkuu DPP sio mjinga hivyo, hivi unadhan mazungumzo na mtuhumiwa ni pesa za bank tu ndio zinahusika? Rejea investment jamaa alizokuwa amefanya kule kigamboni yale mabanda na ekari zile ni zaidi ya 2bil. Bado zile gari za kusambazia kuku na asset nyingine.

Kiufupi serikal ilikuwa inadai jamaa kakwapua billion 17. Sasa inachofanya nikukubana mpaka udondoshe tone la mwisho ndio inakupiga teke. Pengine hiyo gari na asset nyingine zilishapigwa mnada kitambo na madalali wa serikali kwa bei ya kutupa



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapana. Sio rahisi kuuza hivyo vitu vingine kimyakimya bila kujulisha mahakama. Alichonyang'anywa ni huo mpunga tu. Kama kuna kingine mahakama ingesema.
 
Jamaa amewadesisha Sana watz vipi wapo waliowahi fanikiwa au ndio sawa na hadithi za mercury na rupia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…