Mzee wako aliingiliwa vipi kisiasa wakati alienda mwenyewe serikalini kusema ana mamilioni ya dola benki ?
Kama ni hela za serikali Mzee wako anawezaje kujiamulia azihamishe benki moja kwenda nyingine kwa utashi wake, wewe ni Ridhiwani Kikwete, Makongoro Nyerere, Hussein Mwinyi au Jesca Magufuli?
Hela za serikali kwa nini Mzee wako alitaka miamala yake iwe siri ?
Badala ya kutukana tukana unaposhindwa kutetea hoja yako, nenda kamhoji Mzee wako undani wa masuala yenyewe kabla ya kuja kutueleza habari za Mzee wako alitaka kutoa ma milioni ya dola, ukibanwa unasema sio zake. Sio kila msomaji atabugia mazima kila kilichoandikwa, tegemea kuhojiwa.
Narudi kwenye mada ya Mr. Kuku, sio ya spichi za Kimei na Magufuli.
"Due process....Due diligence" gani hazikuwepo kama mchakato ulihusisha majadiliano ya seizure and forfeiture baina ya Jeshi la Polisi, Mahakama, Mkurugenzi wa Mashitaka na wakili wa Mr. Kuku?