Mahakama ya Hakimu Mkazi, imemhukumu mfanyabiashara Tariq Machibya maarufu Mr Kuku, kulipa faini ya sh. milioni tano au kwenda jela miaka 5, baada ya kutiwa hatiani kwa makosa mawili ambayo ni kujihusisha na biashara ya upatu kwa kukusanya fedha kutoka kwa umma na kukubali kupokea miamala ya fedha bila ya leseni.
Katika hukumu hiyo, Mr. Kuku amehukumiwa kulipa faini ya Tsh. Milioni 2 au kifungo cha miaka 5 na katika kosa la pili ametakiwa kulipa faini ya Tsh. Milioni 3 au kifungo cha miaka 5. Ikiwa atashindwa kulipa faini, vifungo ni vyote kwa pamoja
Pia mahakama hiyo, imemuamuru fedha sh. bilioni 5.4 ambazo ziko benki ya CRDB kwenye akaunti ya mshtakiwa huyo kwenda kwenye akaunti ya Mkurugenzi ya Mashitaka nchini( DPP) iliyoko benki Kuu ya Tanzania( BoT).
Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu Mkazi Mfawidhi Godfrey Isaya, baada ya upande wa jamhuri kuingia makubaliano ya kulipa kiasi hicho.
Akisoma hukumu hiyo Hakimu Isaya, alisema mshtakiwa anamtia hatiani kama alivyoshitakiwa ambapo mshitakiwa ameshindwa kulipa fedha hizo na alipelekwa rumande.
Pia soma