Amani Msumari
JF-Expert Member
- Aug 21, 2016
- 1,830
- 972
Wanabodi,
Tujiandae kusikia chochote kutoka kwenye viunga vya siasa za Upinzani. Bundi ametua kwenye mti wa mzambarau halafu akaruka na kwenda kutua mti wa msumbawanga (taja kabila).
Kule kwenye mti wa mzambarau, kachero hashikiki hatamaniki. Unaambiwa amevimba Kama koboko. Kasema Kama mbwai na iwe mbwai yeye ndie mpeperusha fulagi. Nyepesi anahaha kutaka suluhu ila kachero hataki kusikia ukizingatia keshaingiza pensheni yake huko kununua mbolea na viatilifu vingine vya kuukuza mti wa mzambarau.
Kule kwenye mti wa msumbawanga, unaambiwa Mr. Know Ol hafuati maelekezo Wala utaratibu. Amesema yeye ni alwatan almaarufu. Yeye ndio kajiweka juu ya kila kitu na ndio maana inasemekana cheamani na KM wamesusa kimtindo. Mr No Everithingi anaonekana kuwa mzoefu wa mapambano ya kipontio Pilato ila n mwepesi mithili ya unyoya wa kuku yanapokuja masuala ya kikaisari. Cheamani alisikika akisema "mwaka huu Kama nitapata wabunge 20 itakuwa muujiza".
Haya jogoo ameshawika, upande wa pili wazee wa mchicha, matembele, sukumawiki na spinachi nasikia mambo yao kwatu. Wanateleza Kama wako kwenye mgongo wa ngisi. Sasa hivi wamekodisha mwewe wanampanda na amewaongezea umaarufu.
Tusubiri
Amani Msumari
Tanga (kwasasa Kigamboni kumsabahi baba Kegan)