Uchaguzi 2020 Mr. Much know na Kachero waamsha wenge upinzani: Vurugu zimeanza tayari

Uchaguzi 2020 Mr. Much know na Kachero waamsha wenge upinzani: Vurugu zimeanza tayari

Amani Msumari

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2016
Posts
1,830
Reaction score
972
Wanabodi,

Tujiandae kusikia chochote kutoka kwenye viunga vya siasa za Upinzani. Bundi ametua kwenye mti wa mzambarau halafu akaruka na kwenda kutua mti wa msumbawanga (taja kabila).

Kule kwenye mti wa mzambarau, kachero hashikiki hatamaniki. Unaambiwa amevimba Kama koboko. Kasema Kama mbwai na iwe mbwai yeye ndie mpeperusha fulagi. Nyepesi anahaha kutaka suluhu ila kachero hataki kusikia ukizingatia keshaingiza pensheni yake huko kununua mbolea na viatilifu vingine vya kuukuza mti wa mzambarau.

Kule kwenye mti wa msumbawanga, unaambiwa Mr. Know Ol hafuati maelekezo Wala utaratibu. Amesema yeye ni alwatan almaarufu. Yeye ndio kajiweka juu ya kila kitu na ndio maana inasemekana cheamani na KM wamesusa kimtindo. Mr No Everithingi anaonekana kuwa mzoefu wa mapambano ya kipontio Pilato ila n mwepesi mithili ya unyoya wa kuku yanapokuja masuala ya kikaisari. Cheamani alisikika akisema "mwaka huu Kama nitapata wabunge 20 itakuwa muujiza".

Haya jogoo ameshawika, upande wa pili wazee wa mchicha, matembele, sukumawiki na spinachi nasikia mambo yao kwatu. Wanateleza Kama wako kwenye mgongo wa ngisi. Sasa hivi wamekodisha mwewe wanampanda na amewaongezea umaarufu.

Tusubiri

Amani Msumari
Tanga (kwasasa Kigamboni kumsabahi baba Kegan)
 
Ingekuwa ni wewe umetumia kiinua mgongo chako kukodisha shamba na ukaanza kupalilia mti ghafla mwenye shamba anakuambia achana na huo mti, tupalilie mti wa jirani.

Wale vijana uliowaandika kazi na wawekezaji wenzanko unawasikia tuu huko kwa media wanamnadi mkulima mwenzako. Wee utakubaliana na hilo?
 
Ila huko Upinzani bunda ameshalia
Ni kweli mkuu lakini kukomaa kwa chama ni pamoja na uwezo wa kuzima uasi ndani yake bila kukiathiri chama chenyewe. Ni kama uasi uliojitokeza kwenye kile chama kingine ulioanzia kwenye vinyongo vya kukatwa waliongoza kura za maoni mpaka watu wanatishia kuuza mechi kwa timu pinzani.

Naamini vyama vyote vitavuka majaribu haya ya kupita. Uhondo wa mpira ni timu zinazoshindana zije uwanjani zikiwa na wachezaji walio fit 100% ndipo mashabiki mtafurahia ushindi maana utakua wa haki. Ushindi wa hila wa kununua mechi au kumuhonga refa au wa mezani hua haufurahishi
 
Unamuongelea yule ambaye anajua kila kitu mpk akikosolewa anapeleka roho za watu peponi?
Sina hakika. Huyu Machi No n kuwa yeye anawakrashi wenzake na kujiona anajua vyote na kuwa yeye n maarufu zaidi ya msumbawanga. Sidhani Kama umachi noo wake umepelekea kudhulumu uhai
 
Back
Top Bottom