Bhaghosha
JF-Expert Member
- Oct 30, 2010
- 234
- 183
Juzi tumeona maendeleo ya ujenzi wa kiwanja cha mpira cha AFCON kule arusha. Lakini, huwezi kuamini, hadi sasa serikali imeshindwa kuhitimisha michoro ya AFCON City kuuzunguka uwanja. Sababu zinatajwa, vigogo wanang'ang'ania maeneo yao yapangiwe vivutio vizuri zaidi tofauti na wataalaumu wa mipango miji wanavyoona inafaa. matokeo yake michoro na ramani zimeshindikana kupitishwa. Tatizo hili linasababisha uendelezwaji wa eneo sambamba na ujenzi wa kiwanja kukwama. Mkuu wa mkoa Makonda inaelezwa analijua tatizo na mkwamo huu.
Mheshimiwa Raisi ambaye ndiye mwenye mradi huu hajapewa update yake hata pale alipo kuwa Arusha majuzi.
inaombwa next time akija Arusha, ahitaji kuonyeshwa mpango wa AFCON City uliokamilika na kupitishwa na wizara ya Ardhi. Au la sivyo uwanja utakamilika ukiwa umezungukwa na squatters kama ilivyozoeleka hapa Arusha.