Mradi wa Bagamoyo: Hujuma Tanzania na ushindi kwa Kenya na Rwanda

Mradi wa Bagamoyo: Hujuma Tanzania na ushindi kwa Kenya na Rwanda

Zito siyo kwamba watu wanakushambulia bure tu hapana watu wako upande wa rais maana wanamwamini sana na wameshamwona kuwa yeye siyo kigeu geu kama mlivyo nyie ambao leo mnasema hivi kesho vile

Kwa kifupi hamuaminiki

Inawezekana uko sawa kabisa shida ni moja tu nyie wapinzani wa tz hamuaminiki kabisa na watz walio wengi kwa sasa washawashitukia
 
......on the same note, na wewe anza kwanza na protected benefits (in numbers) za makubaliano ya sasa na Barrick.

FYI, tangu ban ya makinikia ilipoanza tumepoteza significant income kama nchi and there's absolutely no guarantee makubaliano ya sasa yanaweza kufidia hata nusu ya upotevu katika lifetime iliyobaki ya migodi ya Barrick.

tuache mihemuko ya ki MATAGA!

Tumesamehe Trilion 424 tulizoibiwa kisha tumelambishwa Trilion 0.7 (Billion 700) tu. Unaacha Almasi unapewa kijiwe halafu unatoka hapo unashangilia kama zuzu

Hizi ndo akili za serikali ya awamu ya tano!

Unafikiri kwa akili za namna hii, wana uwezo na upeo wa kujua faida za mradi wenye manufaa makubwa kama wa bandari ya bagamoyo?
 
Inaitwa Transhipment Hub ambayo kwa sasa iko salala Oman ndio inayo lisha Bandari zote za Africa
Djbout bandari yao inaweza pokea Meli kubwa? Umemuelewa Zitto kwamba Lamu itahudumia hadi south Africa? Kwani South Africa haina Bandari?

Inazungumziwa Bandari ya kuwezesha meli kubwa kutia nanda kitu ambacho hakipo kabisa kwenye bandari karibia zote za Africa
 
Suala si kujenga tu bandari, bali masharti ya uwekezaji huo. Tusingekuwa makini tungeenda kama wenzetu wa Zambia na Sri Lanka walivyofikia. Walifurahia bandari, lakini kilichotokea ni majuto, hawakuweza kulipia deni na kilichotokea waChina ikabidi wachukue bandari kwa muda wa miaka 100. Yaani wachina wana maarifa kuliko wakoloni waliokutana na akina Chief Mangungo.
Mkuu tofautisha mkopo na uwekezaji. Hao walikopeshwa hivyo wanaweka assets kama collateral, sisi wanawekeza ila wanadai tu mazingira wezeshi ili huo mradu ufanikiwe. Sasa kivipi pesa yao wenyewe ikifeli tudaiwe sisi?? Mkuu ww huwa mtu makini usibebwe na propaganda za mitandaoni.
 
minyoo, post: 33288197, member: 145908"]
Bandari nyingi siyo kikwazo kwa Bandari zingine, TISS usiwahusishe na hili siyo wajinga hao wanajua faida ya Bagamoyo , kule South Africa kuna Bandari nyingi Capetown, East London, Port Elizabeth na Darban kila Bandari ina kazi yake maalum, mfano Bandari ya Darban kazi yake ni mizigo ya kimataifa Nchi jirani na za kusini mwa Africa, Tambua Bandari zingine haziwezi kufa kisa Bandari ya Bagamoyo hivyo ni visingizio vya kijuha toka kwa cyprian Musiba Le mutuz na wenzao wasiojielewa.
[/QUOTE]

Viva Taasisi ya rais, TISS na wote waliohusika kupindua meza ya majizi na mafisadi.
 
Mkuu tofautisha mkopo na uwekezaji. Hao walikopeshwa hivyo wanaweka assets kama collateral, sisi wanawekeza ila wanadai tu mazingira wezeshi ili huo mradu ufanikiwe. Sasa kivipi pesa yao wenyewe ikifeli tudaiwe sisi?? Mkuu ww huwa mtu makini usibebwe na propaganda za mitandaoni.

Bro kuna kitu inaitwa PFI/PPP. Kwenye hili kuna mambo mengi yanahusika. Moja wapo muwekezaji atahitaji government guarantee kule atakapokopa pesa za kuwekeza ili kusudi mradi ikishindwa kufanya vizuri, basi serikali itakuwa inalipa deni as per amortization schedule.
Pia demand risk inakuwa shifted to the government. Katika maana ya kuwa meli na makasha (containers) yasipofikia lengo (target) basi nchi itajazia upungufu.
Kwa ufupi ni hayo.
 
Ndugu ZZK ukiweka bandiko na watu wakaja na maswali tokeza kujibu la sivyo hakuwepo maana ya kuandika
1. Uje na numerical analysis ya jinsi tungefaidika na mradi huo
2. Utuambie kwa kusema Uongo au Ukweli kwa uthibitisho kuwa
A. Serkali ilidanganya kuwa mkataba ulitaka tusipate kodi kwa muda kadhaa
B. Kuwa masharti yaliyosemwa na serkali kuwa moja ya kigezo ni kutoendeleza bandari zetu pwani ya bahari ya hindi ni UONGO
C. Useme kwanini kwa muda wote Jk akiwa madarakani haukusaini je kuna vitu vilikuwa si sawa hivyo kuhitaji marekwbisho na tayari yalifanyika?

Kama hujibu tutajumuisha kuwa ni ule upinzani ambao hata ungetekelezwa leo ungeponda kwahiyo ni mtaka sifa na elinu yako ni ya makaratasi au ile white serving education .
Na kwa mlengo huo wale wengine hatuoni shida kuita mamuluki
.
Umesema reli kwenda kigali itafanya Rwanda tusiipate. Je mizigo itashuka wapi na kusafiri kwa usafiri upi to kigali?

Rejea ya Barrick inawaondolea sifa maana mungekuwa viongizi hamkuwa tayari kuishinikiza Bareick , bora hata anayekosea ila anapambana kupata haki. Nyie mnaimani na mahakama za kinataifa tu, je mnajua zile mahakama zipo kumsaidia nani?
 
Ukosoaji usio na staha!!! Na uchonganishi, naviona kwenye posti ya kwanza ya uzi huu.
 
Bro kuna kitu inaitwa PFI/PPP. Kwenye hili kuna mambo mengi yanahusika. Moja wapo muwekezaji atahitaji government guarantee kule atakapokopa pesa za kuwekeza ili kusudi mradi ikishindwa kufanya vizuri, basi serikali itakuwa inalipa deni as per amortization schedule.
Pia demand risk inakuwa shifted to the government. Katika maana ya kuwa meli na makasha (containers) yasipofikia lengo (target) basi nchi itajazia upungufu.
Kwa ufupi ni hayo.
Mkuu na hapa ndio shida inapokuja tuna generalise issues...... Issue ya PFI unafahamu kabisa ikitokea deni limekuja basi hyo asset inachukuliwa na kuwa controlled na public sector ndio deni linaanza kulipwa hivyo ni straight swap sio deni ni la mwekezaji alafu wwe unalipa tu hupati kitu kama inavyotafsiriwa.

Then kwanini tukipiga hesabu za miradi tusiopenda tunaangalia Risk za kufeli.... Mfano sijawahi sikia mkisema SGR (ambayo mpaka sasa 80% imejengwa kwa mikopo) isipokuwa viable basi tutakuwa na deni la zaidi ya trillion 20 (Plus interest) hivyo mabeberu watapora treni zetu?? Sijasikia mkisema hayo.

Yaani kivipi mradi wa bagamoyo msiangalie positive side kuwa UKIFANIKIWA then tutakuwa na Balance of payment inayoeleweka pamoja na mamilioni kuingia kwenye mzunguko hivyo kuleta ajira na kukuza biashara za ndani!!

Hii bias huwa siitegemei kwenye mijadala ya kitaifa.... Ni vizuri tuangalie pande zote mbili mnapopinga uwekezaji sio kulalia tu upande mmoja. Ni sawa na wale wanaodai zanzibar ikijitenga ITAKUWA DOLA YA KIISLAM huku hawasemi faida za uchumi zitakuaje!!

NB: Negotiations zimewekwa ili kuclear sintofahmu zote.... Na ndio maana kama huridhiki una-counter offer na kuja na amendment zako wakikubali mnasonga mbele mkiwa mnajua jinsi ya ku-averse risk zinazoweza jitokeza.

Golden rule is ''the higher the risk, the higher the returns''...... Tuepuke biasness
 
Moja ya mambo ambayo nimeandika hadi vidole vimegoma kuandika ni suala la bandari!!! Na eneo ambalo Magufuli nimeamini ni muongo wa kupindukia ni suala la Bandari ya Bagamoyo!!

Eti serikali haitapata chochote na mazuzu wanamshangilia!!!

Eti hata kodi hatutakusanya wakati duniani kote inafahamika kodi ni mali ya serikali!!!

Na kama alivyosema Zitto, hoja ya ardhi ni hoja ya kijinga!! Sheria ya ardhi inatamka wazi kwamba hati miliki inaweza kutolewa kwa miaka 33, au miaka 66 au 99!!!

Sasa mradi mkubwa kama wa bandari na economic zone hau-qualify hatimiliki ya miaka 99, ni mradi gani tena unaoweza ku-qualify?! Kama mradi mkubwa kama Bandari ya Bagamoyo stahili yake ni miaka 33, ni miradi ya aina gani tena itakayokuwa na sifa ya kuwa na hati miliki ya angalau miaka 66?!!

Ukweli ni kwamba, Magufuli anapenda sifa... angependa sana aonekane yeye ndie mwanzilishi wa ule mradi! Na hicho ndicho kinachomfanya akimbilie miradi mingi mikubwa ili apate hiyo status kwamba kama isingekuwa Magu, basi xyz usingekuwepo kama ambavyo amekuwa akitamba kwamba kama sisi yeye, ATCL isingekuwa na ndege!!!
Rejea Post # 14 ya uzi huu. Fungua hiyo clip na uitazame mwanzo mwisho. Kwa ufupi, hoja zako zote zimejibiwa kwenye clip hiyo.
 
Golden rule is ''the higher the risk, the higher the returns''...... Tuepuke biasness
Hiyo higher risk lazima uwe na strategic plan ya kui'manage'. Mtu anaulizwa strategic plan iko wapi anaangalia pua. Mtu huyu huwezi kuendelea kujadiliana naye hizo ' expected higher return projects'
 
Mkuu na hapa ndio shida inapokuja tuna generalise issues...... Issue ya PFI unafahamu kabisa ikitokea deni limekuja basi hyo asset inachukuliwa na kuwa controlled na public sector ndio deni linaanza kulipwa hivyo ni straight swap sio deni ni la mwekezaji alafu wwe unalipa tu hupati kitu kama inavyotafsiriwa.

Then kwanini tukipiga hesabu za miradi tusiopenda tunaangalia Risk za kufeli.... Mfano sijawahi sikia mkisema SGR (ambayo mpaka sasa 80% imejengwa kwa mikopo) isipokuwa viable basi tutakuwa na deni la zaidi ya trillion 20 (Plus interest) hivyo mabeberu watapora treni zetu?? Sijasikia mkisema hayo.

Yaani kivipi mradi wa bagamoyo msiangalie positive side kuwa UKIFANIKIWA then tutakuwa na Balance of payment inayoeleweka pamoja na mamilioni kuingia kwenye mzunguko hivyo kuleta ajira na kukuza biashara za ndani!!

Hii bias huwa siitegemei kwenye mijadala ya kitaifa.... Ni vizuri tuangalie pande zote mbili mnapopinga uwekezaji sio kulalia tu upande mmoja. Ni sawa na wale wanaodai zanzibar ikijitenga ITAKUWA DOLA YA KIISLAM huku hawasemi faida za uchumi zitakuaje!!

NB: Negotiations zimewekwa ili kuclear sintofahmu zote.... Na ndio maana kama huridhiki una-counter offer na kuja na amendment zako wakikubali mnasonga mbele mkiwa mnajua jinsi ya ku-averse risk zinazoweza jitokeza.

Golden rule is ''the higher the risk, the higher the returns''...... Tuepuke biasness

Bro uzuri nimeshiriki negations nyingi za kuwakilisha nchi zingine.

Ukweli ni kuwa PPP ni nzuri sana iwapo parties zita balance their interest. Mara nyingi nchi za Afrika zimekuwa zinyonywa kwa kutokuwa na utaalam, uweledi na uzoefu.

PPP ni nzuri sana, kwani ina kitu kinaitwa cash motivation. Katika maana ya kuwa, serikali haina haja ya kutenga pesa kwenye budget ili kutekeleza mradi, kama ilivyo kwenye conventional procurement. Private party anatafuta pesa za mradi.

Lingine ni innovation. Private sector wako vizuri kwa hili.

Pia kuna concept of value for money. Private sector wakisimamiwa vizuri wanatoa kitu chenye ubora.

Uzuri mwingine ni kupunguza urasimu. Private sectors hawahitaji approvals na vikao vingi ili kufanyika mabadiriko. Wako more flexible than the public sector.

Mbali na hizi faida, kama nilivyosema, umakini unahitajika sana. Hususan ni hii miradi tunayotaka kuitekeleza bila kuwa na upembuzi yakinifu, iwe kwa sababu hatuna fedha ya hiyo kazi, au utaalam hatuna (lacking technical capacity).
Nachelea kusema, miradi ni mizuri, but we need to be keen. Due diligence is of utmost important.
 
Hiyo higher risk lazima uwe na strategic plan ya kui'manage'. Mtu anaulizwa strategic plan iko wapi anaangalia pua. Mtu huyu huwezi kuendelea kujadiliana naye hizo ' expected higher return projects'
Mkuu mbona sijasikia mkiongelea hizi risk kwa SGR ama Air Tanzania kwamba biashara ikifeli tutakosa pesa za kulipa madeni ya nje hivyo mabeberu watakamata ndege/ Reli yetu?? Why Bagamoyo ndio RISK inaongelewa!!

Kuna wataalam serikalini na kazi yao ndio hyo kuandaa plan za muda mrefu jinsi ya kuepuka hasara..... Kumbuka PFI inasaidia sana kukamilisha mradi wako ndani ya wakati mdogo sana kuliko uunge unge pesa mradi mpaka ukamilike its 2060. Hyo benefit haionekani ila mnazungumzia RISK zake tu!!

Hvi bandari ya bagamoyo mtaweza jenga kwa pesa za ndani kwa mapato haya ya below 1 trillion a month?? Hvi hujui madeni yake ni makubwa kuliko hata PFI (If at all bagamoyo ingejengwa kwa makubaliano ya PPP)!!

Guarantee ya serikali isiwe kigezo cha kuogopa kufanya mradi...... marekani miaka ya 1900 mwanzoni wamejenga madaraja kwa bonds za miaka 50!! Sembuse sisi?

Kwanini hatujiamini kwa bagamoyo ila mnajiamini kwa SGR, Gesi n.k Ambayo nayo yako bound to same risks more so hela ya direct mkopo??
 
Dah hapa ndo naamini watanzania tuna minyoo kichwani.

1. Hivi wachina wajenge afu wasilipe kodi hata cent lakini wawe huru kufanya biashara.
2. Wakae kwenye ardhi yetu miaka 99
3. Haturuhusiwi kuendeleza bandari yeyote zilizopo
4. Wasimamie wao for the whole period kweli. Ndugu zangu hawa hawa

Wanapinga miradi kama
1. Stiglers gorge
2. Reli
3. Ndege
I ambayo hii unakwenda kwa mwananchi wa kawaida moja kwa moja.
Sijui watanzania tunataka nini

Sisi hatukuwa tayari kupata uhuru au tunatakiwa kutawaliwa kidikteta for while hadi hadi tupate akili
Bandari ya Bagamoyo haijengwi kwa mkopo kama Sri-Lanka na Zambia. Hela zote za mradi wanatoa Uchina na Oman: hapa mnaogopa nini ???
Ficha japo hata kidogo tu aibu ya ujinga uliokujaa kichwani!
 
Bro uzuri nimeshiriki negations nyingi za kuwakilisha nchi zingine.

Ukweli ni kuwa PPP ni nzuri sana iwapo parties zita balance their interest. Mara nyingi nchi za Afrika zimekuwa zinyonywa kwa kutokuwa na utaalam, uweledi na uzoefu.

PPP ni nzuri sana, kwani ina kitu kinaitwa cash motivation. Katika maana ya kuwa, serikali haina haja ya kutenga pesa kwenye budget ili kutekeleza mradi, kama ilivyo kwenye conventional procurement. Private party anatafuta pesa za mradi.

Lingine ni innovation. Private sector wako vizuri kwa hili.

Pia kuna concept of value for money. Private sector wakisimamiwa vizuri wanatoa kitu chenye ubora.

Uzuri mwingine ni kupunguza urasimu. Private sectors hawahitaji approvals na vikao vingi ili kufanyika mabadiriko. Wako more flexible than the public sector.

Mbali na hizi faida, kama nilivyosema, umakini unahitajika sana. Hususan ni hii miradi tunayotaka kuitekeleza bila kuwa na upembuzi yakinifu, iwe kwa sababu hatuna fedha ya hiyo kazi, au utaalam hatuna (lacking technical capacity).
Nachelea kusema, miradi ni mizuri, but we need to be keen. Due diligence is of utmost important.
Sasa mkuu kwa uzoefu wako uwe mkweli tu ni heri ya PFI au serikali ichukue mkopo directly ijenge bandari from the scratch?? Ipi ina RISK kubwa??
 
Dah hapa ndo naamini watanzania tuna minyoo kichwani.

1. Hivi wachina wajenge afu wasilipe kodi hata cent lakini wawe huru kufanya biashara.
2. Wakae kwenye ardhi yetu miaka 99
3. Haturuhusiwi kuendeleza bandari yeyote zilizopo
4. Wasimamie wao for the whole period kweli. Ndugu zangu hawa hawa

Wanapinga miradi kama
1. Stiglers gorge
2. Reli
3. Ndege
I ambayo hii unakwenda kwa mwananchi wa kawaida moja kwa moja.
Sijui watanzania tunataka nini

Sisi hatukuwa tayari kupata uhuru au tunatakiwa kutawaliwa kidikteta for while hadi hadi tupate akili
Mkuu ww naona ndio utakuwa mmoja ya wenye minyoo...

Hvi mtu anasema nataka unipangishie chumba kwenye nyumba yako yenye vyumba 10. Ila halipi kodi ya pango ila anamashine za cherehani hivyo ataajiri wapangaji, watakuja wageni kibao hivyo anayeuza maji atauza au mpangaji boda boda atabeba wageni wengi kuwarudisha barabara kuu n.k

Je mpangaji wa hivyo ni hasara au ana faida??
 
Sawa mkuu nimekuelewa. Nadhani uzi huu uendelee na nondo nyingine zaidi kama; Expected return from Investment ya Bagamoyo port ili tujue tungeanza kuneemeka baada ya miaka mingapi ya uwekezaji.

Pia Sikubaliani sana na wewe kwenye suala zima la kuamini kuwa uamuzi wa kusitisha Bagamoyo Economic zone ni uamuzi wa Rais peke yake. Bila shaka majasusi wa kiuchumi waliokuwa kazini kabla ya kusaini mkataba huu ndio chanzo cha kuukataa.

China ni rafiki yetu hilo sikatai, lakini China wa enzi za baba wa taifa (Socialist China) sio huyu China wa sasa (capitalist China).

Hamna majasusi wa kiuchumi hapa Tanzania, bali kuna kikundi cha wanaccm waliopo kwenye ulaji, na ujasusi wao mkubwa ni kufanyia wapinzani na wakosoaji wengine wa serekali ukatili ili serikali isihojiwe chochote.
 
Majasusi wetu huwa wanaanza kwa kuangalia hoja ya nani, kama ya Zitto wamemaliza ujasusi wao hapo hapo.
 
kushindana na Kenya ni kujishusha heshima.
 
Back
Top Bottom