Mradi wa Bagamoyo: Hujuma Tanzania na ushindi kwa Kenya na Rwanda

Huu ni mfano wa kijuha sana wewe mwenyewe inaelekea Akili zako ni mbili tu, mtu akija kupanga akija na mashariti yake na wewe unampa mashariti yako akiyakubali ndipo unampangisha nyumba, huo mfano halipi kodi mara hivi mara vile ni visingizio vya uongo vilivyotengenezwa ili kuwahadaa wananchi wapate kuwaunga mkono pasipo kuchunguza kwa umakini, mikataba ya wachina ilikuwa kwenye majadiliano haikuwa imetiwa sahihi haiwezekani kuwahukumu mia kwa mia.
 
Ngoja nimwagike ninachokielewa kuhusu miradi hii -Bagamoyo na Lamu kabla sijasoma mada.

Ni hivi Bandugu, tusipapatike sana na upotoshaji mwingi unaotoka kwa majirani zetu huko kaskazini. Mengi yanayotoka huko mara nyingi ni hoja za kutupiga vita.

Kwa mfano: hii Bandari ya Lamu ilikuwa inapigiwa upatu sana kupitia jina la 'LAPSSET" - Lamu Port, South Sudan and Ethiopia Project. Wazo hili limekuwepo toka miaka mingi tu (1975).
Wahusika wamejitahidi sana miaka ya hivi karibuni kuwavuta walengwa wa mradi huu kwa njia mbali mbali, lakini juhudi hizo hazijafanikiwa kutokana na bandari yenyewe ilipo.

Ethiopia hawawezi kuja Lamu waache bandari mbili za Djibouti na ile ya Erytrea. Sudan Kusini wanatumia bandari kubwa ya Port Sudan, kwa hiyo uhitaji wao wa Lamu hauna nguvu sana.

Kwa ufupi, LAPSSET umekuwa mradi usiotekelezeka kwa muda mrefu kutokana na kukosekana kwa msukumo wa nchi zilizolengwa.

Mafuta ya Uganda yalipopatikana, na kwa bahati yale ya Turkana nayo yakawepo, yakaipa matumaini zaidi bandari hiyo. Lakini kama sote tunavyojua, Uganda wakaamua vingine.

Katika miaka hii ya hivi karibuni, wenye mradi wakaona, ili kuweka msukumo zaidi waanze wao kwa kuwekeza katika ujenzi wa Bandari, kwa kujenga 'Berth' Namba 1 kati ya tatu za mwanzo.(lengo ni 'berth 32). Hii berth ya kwanza wameikamilisha imebaki tu kufunguliwa mwezi ujao.

Sasa kelele mpya hapo ndipo zinapoanzia, zinazowababaisha hata akina Zitto. Mradi umegeuka sasa, kutoka katika kulenga kuhudumia nchi zile za mwanzo, sasa wameugeuza na kuutafutia nguvu mpya.

Bandari, kumbuka nayo 'berth' moja tu hadi sasa, imegeuzwa kuwa Simba mla watu katika ukanda wote huu wa Afrika. Yale mameli makubwa yenye kubeba makasha 20,000 na zaidi, yasiyoweza kuzifikia bandari ndogo kama Mombasa na Dar es Salaam, kituo chao kitakuwa ni Lamu. Yakifika hapo yapakue makasha yale na kuyaingiza kwenye vimeli vidogo vitakavyotusambazia nasi vimizigo yetu Dar es Salaam na kwingineko.
Kwa hiyo Lamu sasa kitakuwa ni kituo cha kusambaza mizigo (Transshipment) katika ukanda wote huu wa mwambao wa Bahari ya Hindi. Huo ndio mpango mpya.

Je, mpango huo utakuwa na athari zipi katika Bandari zetu? Je, tumekwishafanya utafiti wa kutosha kuonyesha kwamba kweli hapa ndipo Lamu ilipotufungia bao la kisigino? Na mengi mengine ambayo hatuyajui.

Jambo hili kwa sasa halina tofauti sana na zile kelele nyingi sana zilizotaka kumkosesha usingizi Bwana Kikwete wakati wa "Coalition of the Willing." Sote tunajua zilipoishia zile kelele.

Hao watu wa huko Kaskazini hawaishiwi na hizi kelele, siku zote zitakuwepo hata kama wanayoyapigia kelele uwezo wa kuyatimiza hawana.

Kuhusu Bagamoyo: Nakubaliana kabisa na kusitisha mradi huo kama masharti yake ndio hayo yanayowekwa humu mitandaoni.
Swali, Je, nasi tujenge 'berth' moja hapo Bagamoyo kama walivyofanya huko Lamu ili tuweze kushindana na Lamu? Nadhani uamzi wa aina hii utakuwa ni wa kipuuzi.

Serikali ikae chini, na isipapatike na kampeni hizi zinazolenga kubabaisha watu kuliko uhalisia ulivyo.

Bagamoyo ipo, na itaendelea kuwepo. Tutaiendeleza kwa kuangalia mipango yetu na sio kwa kukimbizana na majirani. Tunachojua ni kwamba, eneo Tanzania yetu ilipo kijiografia, labda tushindwe tu sisi wenyewe. Hatuna ushindani wa kututoa kwenye reli. Rwanda hawezi kupeleka mizigo yake mbali kote kule kwa gharama kubwa na kuacha bandari zenye nafu zilizo karibu naye. Hivyo hivyo na nchi zingine.

Wao wanachoweza kung'ang'ania ni Uganda; wakilala usingizi nao tunawanyang'anya.

Ujumbe ni huu. Tuache kupapatikia kila wanachotuletea kutuondoa kwenye mambo tuliyopanga kuyafanya kwa taratibu tulizojiwekea wenyewe.
 
Ficha japo hata kidogo tu aibu ya ujinga uliokujaa kichwani!
Sawa ninyi wenye akili mliokubali kusamehe trilioni 400 kwa kupewa bilioni 700, halafu mkatulizwa kwa asilimia 16% za hisa kwenye Twiga Minerals Corporation huku Barrick akilamba 80% nzima.
 
Wakikujibu naomba usisahau kuniita.
 
Aliyetoa hoja kadai kutolipa kodi ndio faulo ya kwanza na ndio maana nimejibu je kama halipi kodi hakuna namna nyingine ya yeye kuacha faida??

Faida ya uwekezaji kama huo ni kuchochea uchumi na biashara kwa kuongeza mzunguko wa pesa hayo ya kodi ni madogo sana kuliko hizo faida za spillover.

Hyo ndio hoja nayojenga.... ''Uwekezaji ni zaidi ya kodi''.
 
LOoo! Chige Bhwanah. Unanikumbusha yale makinikia na malori ya tani sabasaba ya dhahabu tupu!

Na mara Paa! SGR ikaenda kwa waturuki! Hivi kweli tunajua sababu zilizosababisha badiliko hilo la ghafla? Huyu Kikwete na watu wake wote walikuwa hawalitakii mema taifa hili?

Heshima sana mkuu Chige.

Hili la kusema uongo ni tatizo kubwa. Na kweli, lengo ni hilo hilo ulilotaja. Sifa.

Pengine siku moja itatokea watu wajue ukweli. Sasa hapo hata kama atakuwa amejijengea 'legacy' ya kuyajenga yote hayo yeye, watu watamdharau kwa ubabaishaji aliolifanyia taifa kwa kujitafutia sifa binafsi.
 
Mkuu hapo ni kweli kabisa, maana hata sakata la dhahabu iliyokamatwa Mwanza lilianzia Kenya ambako pesa kutoka falme za kiarabu zilipokelewa na Ruto kwa ajili ya dhahabu, dhahabu zilipokamatwa ilibidi Uhuru Kenyatta aje amwambie Jiwe kuwa ni za mabeberu wa kiarabu ndio kasalimu amri kuzirudisha na kuwaachia wale askari nane kwa maelekezo ya mabeberu wa kiarabu na Jiwe akanywea back to the point ccm wajinga sana yaani wamekubali nchi ipandikiziwe uongozi na Bahima empire, matokeo yake ndio haya sasa, Hutu linaiua hii nchi.
 
Aisee kuna mapimbi duniani sijawahi kuona, yaani Zitto Nondo alizoshuka hajaelewa? Halafu Jiwe tunamjua vizuri.kuleta kivuko kibovu, meli ya samaki, wakandarasi hewa bilioni 356, raia wapige mbizi, nyumba za serikali, niendelee, hamna mtu hapo.
 
Very good analysis.
 

Asante sana
 
Zitto anafikiri Watanzania wajui kitu. Yeye ndiye anaye jua. Bandari ijengwe Bagamoyo yote iwe chini ya wamiliki kwa miaka 99yrs. Aturuhusiwi kufanya chochote Kule ata ulinzi ni wao muda huo wote
Walioruhusu ndege kuruka toka migodini bila kukaguliwa kina nani? Ndege kuruka toka mbuga za wanyama kina nani? Loliondo mbuga mpaka simu inakuambia sasa umeingia nchi za falme za kiarabu? Niendelee.
 
Majasusi gani? Ndo hao walio mshauri kwamba Serikali ikanunue korosho kwa kutumia Jeshi? Kama ndo hao basi tuna shida kubwa na majasusi wetu.
Nimelewa ni kiasi gani Kenya National inteligemce service NIS inavyozidi ujanja TISS linapokuja swala la maslahi ya taifa, kumbe zile mbwembwe za kujemga urafiki kati ya Uhuru na Raila ilikuwa ni mbinu ya kumkamata mzee wa misifa?? Naye bila kujua akaingia mtegoni.

NIS iliwalazimisha uhusiano mwema kati ta Raila na Uhuru ili.kulinda maslahi ya wakenya.

Sasa Lamu port hii itaifikisha mbali sana. Hata hizi meli ndogo tu haizifiki dar port lazima zipite Mombasa.
 
Aisee kuna mapimbi duniani sijawahi kuona, yaani Zitto Nondo alizoshuka hajaelewa? Halafu Jiwe tunamjua vizuri.kuleta kivuko kibovu, meli ya samaki, wakandarasi hewa bilioni 356, raia wapige mbizi, nyumba za serikali, niendelee, hamna mtu hapo.
Pia kajenga uwanja wa ndege chato kwa gharama kubwa pesa za walipa kodi
 
Kenya wanaenda kupiga pesa nyingi hata mizigo ya somalia itapitia hapo hapo
 

UONGO MTUPU.

1. Hakuna ardhi inayouzwa. Ardhi ya Tanzania ni LEASEHOLD na Sheria yetu inasema unaweza kuwa na lease ya miaka 99. Hii ni hali ya kawaida kabisa.

2. Mradi huu ni JOINT VENTURE yaani Serikali inakuwa na hisa kutokana na ardhi kama EQUITY. Tanzania itakuwa ni sehemu ya umiliki. Pia Bandari ni suala la Sheria na kuna Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari. Eti hatuna control nayo ni UONGO.
3. Mradi huu sio mkopo ni UWEKEZAJI. Ni FDI. Ukiwa wa hasara anayepata hasara ni mwenye mtaji.
4. UONGO unaotokana na ujinga. Sheria za Kodi zipo vile vile.
5. Hakuna dhamana yeyote. Ni Uwekezaji
6. UONGO unaotokana na ujinga. Huu sio mkopo ni FDI hakuna riba
7. 8 na 9 ni UPUUZI
 
Tena kibaya zaidi ambacho wanasahau ni kwamba mwekezaji anapewa Derivative Right hivyo ardhi haiwi yake, kwenye hati ya umiliki ardhi jina linatokea ni la Export Processing Zones Authority (EPZA) ambaye yeye ndiyo atawapa Uchina na Oman wafanyie biashara (Joint Venture).

Sheria za nchi yetu haziruhusu mtu kumiliki ardhi, sembuse mgeni!
 
Blaa blaa na siasa nyingi, lakini Story yenyewe haina substance.

Rais Magufuli ninacho kuomba zidisha kasi ya reli ya SGR ya central corridor ifike DRC, Rwanda na Burundi na ikiwezekana jenga nyingine mpaka Tunduma. Hii treni ya Tunduma ita serve mizigo ya Lubumbashi, Mufulira na miji ya kaskazini mwa Zambia.

Treni za umeme zutafanya usafirishaji wa mizigo kuwa na gharama nafuu na hivyo utaifanya bandari ya Dar es salaam kuwa busy sana na hivyo kutoa ajira nyingi.

Wekeza hela nyingi kwenye SGR iishe kwa haraka itakuwa ukombozi mkubwa sana kwa watanzania. Achana na kununua mandege ambayo yanagharama kubwa ya kuyaendesha.

Vile vile nakuomba achana na Mabasi ya mwendo kasi badala yake tengeneza Trams na underground trens au wenyewe wanaita Metro na pia sky trens.

Watu wengi watakuja kutalii na hivyo kuwafanya watanzania kuwa na ajira.

Vitu vingine jenga ma funace ya kuoka chuma na mtambo wa kusindika gas, yaani LNG. Tukiwa na chuma yetu tutawafanya vijana wengi wajihusishe na matumizi ya chuma na hivyo kupanua uwezo wao wa kuwa wabunifu. Hivyo hivyo kwenye LNG.
 
Summary ya majibu ya serikali.

Government rejected and revised five stringent demands made by Chinese investor because they were not beneficial to the country.
Once the Chinese firm agrees in principal with the government’s new conditions, the project can move to the next stage which is execution in collaboration with the Oman’s State General Reserve Fund (SGRF).

Tanzania Ports Authority chief executive Deusdedit Kakoko said the government rejected and revised five stringent demands made by the investor—Beijing-based China Merchants Holdings International—because they were not beneficial to the country.

1. The Chinese investor has now been offered a 33-year lease instead of the 99-year one asked for.

2. The investor has been informed that there will be no tax holiday and they will be subjected to all taxes designed by the Tanzania Revenue Authority.

3. That there would be no special status and they would be required to pay the market rate for water and electricity like any other investor.

4. They could not start and run any other business they deemed necessary within the port without government’s approval and were open to scrutiny and regulation by relevant agencies in line with law like any other investor.

5. They were informed that the government of Tanzania was free to develop other ports to be in direct competition with Bagamoyo.

Once the Chinese firm agrees in principal with the government’s new conditions, the project can move to the next stage which is execution in collaboration with the Oman’s State General Reserve Fund (SGRF).


Serikali inapinga vigezo vitano (stringent demands)

1.Miaka 99 wamewapa 33, wapi duniani utapata mkataba wa miaka 99 kama ule wa wa kitapeli wa Hong Kong au Liberia na mpira. Jiulize kama China wanaweza kukupa mkataba kama huo.

2. Kigezo cha pili nafikiri serikali inaweza kuwa flexible hata kuwapa mwaka mmoja, wa Tax holiday, lakini kwa baadhi ya tax ambazo zinaweza kuchangia kukua kwa ajira, mapato ya serikali as a gesture of goodwill.

3. 100% ninakubaliana na serikali. Maji, Umeme , lazima yalipiwe ili hizo pesa zipelekwe kuwasaidia maskini vijijini na mijini.

4. Muhimu sana, otherwise hakuna, hatuna Serikali. Ni kama exactly Waingereza walivyowafanyia Wachina. Mkataba ule uliowaruhusu Waingereza kuuza madawa ya kulevywa China pia ulikuwa na kipengele kama hiki.

5. Nchi inawezaje kuitwa huru kama haiwezi kuendeleza bandari zake nyingine kama Mtwara, Tanga, Lindi, Dar. Kujua nini kinaingia na kutoka, faida yao na hasara?

Mkataba kama huo Lamu, Kenya wakiuchukua, imekula kwao ni vilio vingi huko mbeleni.

Tanzania iko sehemu nzuri sana strategically, hata kama hawa watakataa masharti wengine watakuja.

Tupo karibu na Malawi, Zambia, Congo DRC, Burundi na nyingine nyingi tu kwenye ukanda wetu Pia tuna mahusiano mazuri na nchi zote hizo zote za karibu.

Muhimu kusaini mkataba wenye tija, kuliko kukurupuka.

Kwa hiyo wewe Mr Zitto ungesaini na kukubali haya Masharti?
 
Kenya wanaenda kupiga pesa nyingi hata mizigo ya somalia itapitia hapo hapo
Sio somalia tu hata yetu itaita hapo hapo maana itakuwa rahisi kupitisha Kenya kwa meli kubwa kuliko meli ndogo, urahisi wa bandari unaleta nafuu pia kwa bidhaa zinazoingia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…