Tunataka Miradi mingi katika taifa letu, Lakini tunataka miradi ambayo kiukweli italeta ukombozi wa maisha ya wananchi
Mradi wa Bandari ya Bagamoyo, ni mradi mkubwa na unaumhimu wake, Lakini kwa nini usiwe wazi?
Hivi zile ndege za Mwendazake mnazoshangilia huku zikiendelea kulitia hasara taifa, mmeshawahi kudai uwazi kwenye ununuzi wake?
kwa nini tunadhani JPM pamoja na aliyekuwa mgombea Uraisi kupitia Chadema 2015 mh EL wamekuwa waongo kuukataa huu mradi kwamba hauna manufaa yoyote kwa nchi yetu?
HIvi unadhani Lowassa ni kilaza namna hiyo?! Jombaa, that's politics... kama politics za Magu na CCM yake ya kutoa 50M kwa kila kijiji, na laptop kwa wanafunzi!!!
Moja ya hoja zinazotolewa na wapinzani wa Mradi wa Bandari ya Bagamoyo ni kwanini isijengwe Bandari ya Tanga!!! Sasa inakushangaza Lowassa akiwa Tanga kwenye kampeni kusema atasitisha Mradi wa Bandari ya Bagamoyo na serikali yake ku-focus Bandari ya Tanga?
Kuanzisha mradi wa Bandari Bagamoyo bila kuwepo uwazi wa mkataba uliotiliwa mashaka na viongozi mbalimbali wa nchi hii, ni uhujumu uchumi mkubwa na kuziua bandari zetu ambazo ni tegemeo kubwa la uchumi wetu
Hivi nyie wafuasi wa Magu mmewahi kuoneshwa mkataba upi tangu taifa hili lianzishwe?! Of course, suala la uwazi wa mikataba limekuwa ni kilio cha muda mrefu hadi bungeni, lakini mbona hatuwaoni mkililia kuonesha mikataba kama ya SGR, ununuzi wa ndege, Mradi wa Bwawa la Nyerere, n.k?!
Hivi ni kweli hoja yenu ni kuona mkataba au mnajaribu ku-justify hoja za Magu na kujificha kwenye issue ya mkataba?!
Hivi, Tanzania ni lini tutafahamu kwamba, uwingi wa miradi na sifa ya kuwepo wawekezaji wengi wasio na faida haituongezei chochote zaidi ya kutufanya tuwe taifa tegemezi na lisiloweza kujikomboa na umasikini..!
Umetumia vigezo gani ku-conclude hiyo hoja yako?! Magu alipuuza hata miradi ya gas kule kusini, na akaishia kudanganya watu kwamba eti gas imeuzwa bila kutaja wauzaji ni nani, na waliouziwa ni akina, na serikali yake inachukua hatua zipi!!
Je, unataka kusema uwekezaji kwenye gas hauna faida wakati hadi sasa kuna kiasi kikubwa kabisa cha umeme tunaotumia unatokana na gas, wakati ni sehemu ndogo tu ya gas iliyochimbwa hadi sasa!!
Kuwa na wingi wa miradi haina maana kwamba ni kuondoa umasikini, Umasikini unaweza kuondoka tu pale tutakapokuwa tukifanya uwekezaji wenye tija na kuingia miktaba isiyokandamizi,
Hiyo miradi mingi ni ipi?!
Kushindana ki miradi na nchi fulani bila kujali hiyo miradi inafaida gani ni kujiumiza sisi wenyewe
Mungu ibariki Tanzania na Mungu bariki viongozi wetu
Tunashindana na nchi ipi?! Fuatilia historia uone ndoto ya bandari ya Bagamoyo imeanza lini!!!