kama imetupwa vile ? Mradi huu umefia wapi ?
Nilipokujibu hapo juu kifupi, nilikuwa sijasoma andiko lako lote hadi mwisho.
Sasa nimelisoma lote, na nina machache ninayoweza kukuchangia.
Awali ya yote, majibu ya maswali yako mengi kumbe umekwishayajibu mwenyewe, kwani unao ufahamu wa ujio wa bandari ya Bagamoyo, ambayo kwa kiasi kikubwa inakidhi hayo uliyoyataja juu ya bandari ya Mwambani, hata kama siyo yote.
Kwa hiyo, inaonekana unao ufahamu wa mambo yalivyogeuka toka Tanga hadi Bwagamoyo, lakini bado unauliza maswali, nadhani kwa kutaka tu watu wajadili mada yako. Siyo vibaya.
Nieleze wazi, niko upande wako. Nimechangia mara nyingi kwenye mada za namna hii zilizoletwa humu JF, nikiipambania Mwambani, kwa sababu najuwa ina manufaa makubwa zaidi, kama ulivyoelezea wewe kwenye mada yako, na hata zaidi; kama vile kwa Tanzania kutotegemea bandari ya Mombasa, huku tukiwa na powani ndefu kabisa. Hivi unajuwa kwamba asilimia karibu ya 7.2 ya mizigo inayopitia Mombasa kwenda nje ya Kenya ni ile inayokuja Tanzania? Uganda ikichukuwa zaidi ya asilimia 82?
Maajabu ni kuwa, hata tumewajengea barabara nzuri kabisa toka Holili, ikipitia Moshi/Arusha kwenda Singida na kuchepuka kuelekea Tabora na Burundi? Nchi yetu hii, imechukua mikopo WB, ili barabara ijengwe kupitisha mizigo inayotokea Mombasa kwenda Kaskazini mwa Tanzania, na hadi kuipeleka Burundi! Lakini tunashindwa kabisa kuendeleza/kujenga bandari ambayo ipo jirani kabisa na maeneo haya ili nchi yetu ipate faida zaidi!
Kuna watu hupenda sana hizi 'conspiracy theories' za kusema huenda tuna mapandikizi ndani ya nchi yetu yanayoshika nafasi za juu ku-'undermine' juhudi zetu kwa manufaa ya watu wengine. Mambo kama haya yanapojitokeza hivi, inakuwa ni vigumu sana kutowazia haya ma-'conspiracy' yanayosemwa mara kwa mara
Bagamoyo ni nzuri, lakini nadhani Mwambani ingekuwa nzuri zaidi. Na yaliyosemwa kilaghai na Kikwete wakati akiwatuliza watu wa Tanga juu ya kuwanyima ahadi yao ya bandari ya Mwambani, ni kwamba mpango huo ungeweza kuendelea kama mwanzo, eti kwamba watu binafsi watachukuwa jukumu la kuuendeleza. Huu ni ulaghai wa kijinga sana kuwaambia watu, ambao alikuwa amewapa matumaini makubwa juu ya bandari ile.
Nakusihi usiwe mvivu wa kurejea michango iliyomo humu JF, kwani kuna mambo mengi sana yalikwishaandikwa kuhusu haya yote unayotaka yajadiliwe tena.
Nimetiririka tu, kama kuna makosa, naomba radhi. Sikufanya masahihisho.