Yeah
Inakera Sana ,halafu tulivyo mafala tunakomoana wenyewe Kwa wenyewe
Mfano hili Suala la uharibifu wa mazingira , wakenya walikua wanalishupalia ,ila huwezi kusikia Wajerumani au Waitaliano wakiwasagia kunguni ufaransa au uingereza
hata bwawa la umeme la Mwl Nyerere, wazungu walisema tunaharibu mazalia ya samaki kamba, Januari na wenzake wengi tu waliunga mkono, bila magufuli lile bwawa tusingekuja kulijenga. kwenye hili bomba la total, wameandamana hadi kwenye mabunge yao ati tunavunja haki za binadamu kwasababu hatulipi watu fidia, kumbe hawajui kama tz ardhi ni mali ya umma na fidia watu walishapewa, na wakasema tunahatarisha mazingira. wakati hapohapo tangu enzi kuna bwawa la mafuta toka DSM hadi zambia, halijawahi kuleta hitilafu tangu miaka ya sabini hadi kesho. mzungu huwa hapendi mwafrika afanikiwe.