Mradi wa bomba la gesi asili toka Tanzania kwenda Kenya

Mradi wa bomba la gesi asili toka Tanzania kwenda Kenya

Unadhani $1 billion ni nini kwa uchumi wa $100 billion? Wacha mchezo bwana. $1 billion sio kitu

Uchumi wa 100 billion kwa watu wangapi? Huo ni Uchumi mdogo sana kuujengea Bomba la Gesi la zaidi ya 1 Billion USD
 
Unadhani $1 billion ni nini kwa uchumi wa $100 billion? Wacha mchezo bwana. $1 billion sio kitu
Tatizo lenu ninyi wakenya ni uwezo mdogo wa kufikiri. Huu mradi ukifanikiwa viwanda vya Kenya vitapunguza au kuacha kabisa matumizi ya umeme, hivyo kupunguza gharama za uzalishaji, hiyo tu pekee itapunguza gharama za maisha za wakenya na kuvutia wawekezaji watakaotengeneza ajira kwa Wakenya.

Faida hiyo moja tu inazidi kwa mbali sana $4B mliyoitumia kujenga SGR ambayo ni mzigo kwa wakenya kwa sasa.
 
Siyo swala la kuwa Mwafrika au la, ni swala la kiuchumi, haya mambo ndiyo yaliyotufikisha hapa, kuwekeza 1 bilion USD kwa nchi kama Tanzania ni pesa nyingi sana, na Kenya hakuna uchumi wa kuhalisha huo uwekezaji.
Weka facts sio hisia. Leta facts za kiuchumi kuonyesha kuwa Kenya itakosa $1 b ya kujenga hii pipeline.
 
Uchumi wa 100 billion kwa watu wangapi? Huo ni Uchumi mdogo sana kuujengea Bomba la Gesi la zaidi ya 1 Billion USD, ...
Kwani utadhani TZ itatoa hio pesa yote? Itakuwa cost sharing.
 
Tatizo lenu ninyi wakenya ni uwezo mdogo wa kufikiri. Huu mradi ukifanikiwa viwanda vya Kenya vitapunguza au kuacha kabisa matumizi ya umeme, hivyo kupunguza gharama za uzalishaji, hiyo tu pekee itapunguza gharama za maisha za wakenya na kuvutia wawekezaji watakaotengeneza ajira kwa wakenya.

Faida hiyo moja tu inazidi kwa mbali sana $4B mliyoitumia kujenga SGR ambayo ni mzigo kwa wakenya kwa sasa.
Nakubaliana na wewe kwenye sula zima la gesi lakini naomba kupinga katika suala la Sgr.
 
Weka facts sio hisia. Leta facts za kiuchumi kuonyesha kuwa Kenya itakosa $1 b ya kujenga hii pipeline.

Swala siyo kukosa pesa, wanaweza hata kutoa billioni 50, lkn swali ni kwamba kama italipa kibiashara kwa TZ kufanya uwekezaji kama huo na kupata faida, Kenya haina industries za kuweza kununua hiyo gesi na kuufanya huo mradi ulete faida kwetu, ...
 
Nakubaliana na hii point yako. Serikali imetoa idhini dhidi ya kukata miti. Sasa hivi tunatoa mbao za kuunda viti na mambo mengine Tanzania na Congo. Bei ya makaa imepanda ajabu.
Ukweli ni kwamba, umuhimu wa mradi wowote katika nchi yoyote ile hasa nchi masikini ni pale huo mradi unapuwasaidia wananchi wa kawaida moja kwa moja, hizi flyover na interchange japo ni muhimu lakini haziwagusi watu wengi "directly" hasa wa mikoani na vijijini

Nchi inapofanikiwa kusambaza maji mitaani na vijiji, umeme au gas kwa wananchi, effect yake ni kubwa mara kumi ya hii miradi ya flyovers na Interchange. Kenya you need this pile very urgently.
 
Kaka tofautisha mamba mawili katika biashara ya gesi

1)Compressed gas = Hii ni lazima ujenge kiwanda kwa ajili ya kuigeuza iwe kwenye 'liquid form" iweze kuingia katika meli na mitungi midogo kwa kusafirishwa.

Hiki kiwanda pekee kinagharimu $30B, ndio mazungumzo yapo katika hatua za mwisho ili wawekezaji waanze kujenga hicho kiwanda huko Mtwara ili gesi yetu iweze kupelekwa nchi mbali mbali duniani.

Kutokana na uwekezaji wa pesa nyingi katika kujenga kiwanda, matokeo yake gharama ya gesi inakua juu sana kwa wananchi masikini kuweza kupikia majumbani

2)Non compressed= Hii gharama yake ni Kihinga bomba toka kwenye visima hadi majumbani, unatumia kama maji, bei yake ipo chini sana, wananchi wengi wanaweza kulipia.

Kiwanda cha kugeuza gesi kuwa maji ni biashara kubwa kwa hiyo ni private sector, lakini bomba la gesi zaidi ni serikali kwasababu ni sehemu ya huduma kama umeme na reli.
Hii gesi ambayo haijakuwa compressed inaweza kulipuka kama ile iliyo compressed kwenye mtungi au hii ni safe hailipuki?
 
Nakubaliana na wewe kwenye sula zima la gesi lakini naomba kupinga katika suala la Sgr.
Jaribu kufuatilia mijadala ya David Ndii kuhusu SGR ya Kenya, kubali au kataa, SGR ya Kenya haina faida yoyote beyond Nairobi, hasa kama haitofika Kampala.

Bandari za Lamu na Bagamayo, ni duplication of the projects za Dar na Mombasa ports, hazina faida kwa uchumi wa hizi nchi.

Mombasa Nairobi high way, haina faida kwa sasa hasa baada ya kukamilika kwa SGR ya Mombasa-Nairobi
 
Kwa hivyo kulingana na wewe nchi haifai kuwa na reli na barabara zinazounganisha cities mbili kwa wakati mmoja? Ni lazima nchi ichague njia moja ya kusafiri. Either reli au barabara lakini sio zote mbili?
 
Hii gesi ambayo haijakuwa compressed inaweza kulipuka kama ile iliyo compressed kwenye mtungi au hii ni safe hailipuki?
Inavyotoka pressure yake ni Kama ya kwenye mitungi, kumbuka kwamba lazima isukumwe na mashine ili ipate pressure ya kufika mbali kwa kiwango kinachohitajika.

Kama umekaa Ujerumani, nchi ambayo inatumia gasi inayotoka Russia moja kwa moja kwa kutumia bomba la gasi, utajua inavyofanya kazi.

Tofauti kati ya hii "Natural gas", ni nyepesi kwahiyo ikitokea umesahau kufunga koki, basi inatoka hara kupitia dirishani, wakati hii ya "Liquefied Petroleum gas"(LPG) ambayo ni nzito zaidi ya "air" haitoki inabaki jikoni ukiwasha moto inalipuka na kuunguza nyumba au watu.

Uwezekano wa Natural gas kulipuka ni mdogo sana kama madirisha yatakuwa Open all the time.
 
Kwa hivyo kulingana na wewe nchi haifai kuwa na reli na barabara zinazounganisha cities mbili kwa wakati mmoja? Ni lazima nchi ichague njia moja ya kusafiri. Either reli au barabara lakini sio zote mbili?
Barabara iliyopo ikisaidiana na reli inatosha, Kenya haipaswi kujenga Thika high way nyingine toka Nairobi hadi Mombasa kwa sasa, uchumi hauruhusu na si kipaumbele kwa sasa hivi, kuna shida nyingi na za msingi kuliko hiyo barabara kwasasa
 
Mimi huwa napinga Mombasa-Nairobi expressway. Hata ukifuatilia posts zangu za zamani utaona. Hio barabara ya sasa inatosha. Reli pia imesaidia Kenya kwa sababu mizigo haichelewi kwenye port hata kidogo. Wafanyibiashara wa Nairobi wanachukulia container zao Nairobi, sio lazima waende Mombasa. Turnover ya Mombasa port imeimprove. Badala ya kupakua container 105 katika malory 105 na kupoteza muda mwingi, sasa container 105 zinapakuliwa katika treni moja na hio treni inafika Nairobi kwa masaa manane. Mizigo ikifika Mombasa port, itapakuliwa na kufika Nairobi kwa haraka ukilinganisha na enzi ambazo tulikuwa tunatumia malory. Najua huwezi kubali kuwa Sgr ina manufaa yoyote katika uchumi wa Kenya kwa sababu uliichukia hii Sgr kutoka zamani ila hakuna mradi usiokuwa na uzuri wake.
 
Binafsi siamini kama Kenya kuna Uchumi wa kuhalalisha uwekezaji wa 1 bilion USD, hiyo ni pesa nyingi sana, na hakuna Viwanda wala households za kurudisha hiyo gharama, Uchumi wao hautoshi, kwa maoni yangu ni bora Gesi yetu tungejikita kwenye kuexport kwenye Industrialized countries, huko ndiko kutakapo lipa, kama tukijaza Meli na Gesi na kuiuza Ulaya, Asia au hata USA ingawaje wana yao pia, lkn hasa Ulaya na Asia italipa, lkn kwa Kenya Uchumi wao ni mdogo mno kuhalalisha 1 billion Dollar USD investment hasa kama italipwa na walipa kodi wa uchumi mdogo kama wetu au Kenya.
Tanzania ilijenga kutumia $mil 500 hio hela inapatikana kama wakiamua
 
Naelewa yote hayo, hiyo 1 billion ni bora tuwekeze kwingine lkn kupeleka Kenya kwa maoni yangu hailipi kwani ni pesa nyingi sana kwa Uchumi kama wetu, usisahahu kuna maintenance ya hiyo infrastructure pia.
Yeah..kwa sasa bora pesa iende kiwingne ila uwezo upo..
 
Mimi huwa napinga Mombasa-Nairobi expressway. Hata ukifuatilia posts zangu za zamani utaona. Hio barabara ya sasa inatosha. Reli pia imesaidia Kenya kwa sababu mizigo haichelewi kwenye port hata kidogo. Wafanyibiashara wa Nairobi wanachukulia container zao Nairobi, sio lazima waende Mombasa. Turnover ya Mombasa port imeimprove. Badala ya kupakua container 105 katika malory 105 na kupoteza muda mwingi, sasa container 105 zinapakuliwa katika treni moja na hio treni inafika Nairobi kwa masaa manane. Mizigo ikifika Mombasa port, itapakuliwa na kufika Nairobi kwa haraka ukilinganisha na enzi ambazo tulikuwa tunatumia malory. Najua huwezi kubali kuwa Sgr ina manufaa yoyote katika uchumi wa Kenya kwa sababu uliichukia hii Sgr kutoka zamani ila hakuna mradi usiokuwa na uzuri wake.
Soma vizuri nimesema haina faida beyond Nairobi, lakini Mombasa to Nairobi inasaidia ndio sababu nikasema umuhimu wa Mombasa to Nairobi super high way haupo tena kutokana na kuwepo hiyo reli
 
Ni kweli kabisa. Cha msingi wanatakiwa waache mawazo yao ya zamani. Mawazo mgando yaliyopitwa na wakati ya kujifanya eti wapo juu kiuchumi.

Kama tutafanikisha suala hili hakika tutaanza kuwa control kisiasa na uchumi wao utaanza kutegemea Tanzania.
Wategemee tz mara ngapi? Hawa ni wana wetu.

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom