Hii sio mambo ya battle kati ya KE na TZ. Mimi nazungumza ukweli tu. Kama unijuavyo, ukweli ndio kitu cha muhimu kwangu. Kwanza TZ haijasign revenue sharing contract na wawekezaji. Pili, Mwekezaji hajatoa FID (final investment decision). Tatu, mwekezaji hajaanza kujenga kiwanda hapo TZ.
Upande wa Mozambique, mkataba kati ya serikali na mwekezaji ulitiwa saini zamani. Mwekezaji ameshatoa final investment decision (yaani mwekezaji ameshaamua kuenda mbele na ujenzi) halafu tatu, mwekezaji amesha order ujenzi wa meli iliyobeba kiwanda cha kucompress gas kianze kujengwa huko South Korea.
sasa sijui ni kwa nini huoni kuwa Mozambique walishawapita zamani na wao ndio watakuwa wa kwanza kucompress gesi. Kama Kikwete bado angekuwa rais basi mngekuwa wa kwanza kwa sababu yeye alijua jinsi ya kuongea na wawekezaji na kuwapa matumaini, ila huyu wa sasa anatia wawekezaji uoga hadi wanatoroka.