Mradi wa Bwawa la Nyerere tulijilisha upepo au ndiyo mwendelezo wa siasa chafu za kibepari?

Mkuu huku tunakorudi hatutapiga hatua, ni sawa na kukanyaga mafuta mengi wakati gari iko kwenye free gear!
Hiyo power master plan yenyewe mwendazake aliibadilisha akaweka huo mradi..
Mjadala nadhani ungekua kwamba;
※ Kwanini aliamua kufinance hiyo project kwa mikopo ya kibiashara tena ya muda mfupi na riba kubwa. Juzi tumeambiwa marejesho yameshaanza na project haijakamilika ikabidi tutumie mkopo mwingine kulipa huo mkopo kitu ambacho nakiona kama ukichaa!
 
Ninawasi wasi sana na huu mradi kuwa na tija hapo baadae maana watanzania hatuna historia ya kuendesha miradi mikubwa ,Mwl nyerere aliacha mashirika makubwa sana yakiwa na hari nzuri lakini mengi yamekufa kama si kubinafsishwa kwa hasara,moja ya kosa la serikari ni mkandarqsi alipewa kujenga mradi Mwarabu muda mwingi yeye ni kunywa kahawa na kupiga fitna mchina ambae ni sub anawakimbiza kwa kufanya kazi kwa wakati ukumbuke kila unavyoongeza muda katika miradi garama zinazidi na mbatika katika lengo,swari je serikari na tanesco wamejiandaa kikamilifu hapo baadae kuendesha mradi?je tabia ya watanzania katika usimamizi wa mali za umma umebadilika?sina hakika kama tutamudu kuendesha huu mradi na kurejesha garama hapo baadae nionavyo tutarudi kwenye kuubinafsisha tu muda ni mwalimu mzuri sana hivyo tusubili
 
Maswali konki kabisa haya
 
Point yako ni ipi sasa?
 
Mkuu hakuna cha winch wala winji ni porojo tu zile nipo eneo la mradi katika nafasi ya mfanyakazi wa JV hamna kitu &January angekuwa na akili na yule mwingine alieugua corona wangewauliza watanzania jamani eeeee ni nini kinaendelea hapa?wangewasikiliza nazani wasimamizi wa mradi wangefukuzwa kazi hapo hapo kuna madudu ya hovyo sana huku
 
Kabla hayo unayotaka yajadiliwe nadhani ungeleta hiyo master plani ya hiyo hadi 2050 aliyokuomba mleta mada tuone.
 
Sasa si muumakize huu mradi basi au zile cranes za Makamba ya katani bado kufika
 
Asante kwa kudadavua kwa mapana yake.
Umeme wa JKNHPP ni lazima.
 
Japo sijaisoma sababu ndefu sana ila najua lazima itakua nzuri so naunga mkono hoja
 
Mkuu, ili kupata taswira ya inakokwenda ni lazima tufahamu tulikotoka ili makosa yasijirudie.
Mimi nimekuuliza maswali machache kuhusu Power-Master-Plan 2025 ili niweze kufahamu ni lini ilitengenezwa, kwa kiwango gani ilitekelezwa kabla ya 2015, fungu lake ni kiasi gani na kufahamu ni kiasi gani cha umeme kingeweza kuzalishwa mpaka 2050.

Lilikuwa ni suala dogo tu, kunipa hata chanzo ili nitakafute mwenyewe. Ntashukuru ukinasaidia kupata vyanzo ili nijifunze zaidi.....
 
Ninawasi wasi sana na huu mradi kuwa na tija hapo baadae maana watanzania hatuna historia ya kuendesha miradi mikubwa
Tukitumia mantiki ya hoja yako, ina maana tusitishe miradi yote mikubwa inayoendelea nchini kwasababu hatuna uwezo wa kuiendesha. Eti kaka Chige unakubaliana na huyu ndugu ???
 
Hiyo masterplan ilieditwa na Jiwe..
Na mimi sikusave ile ya mwanzo..kwa sasa ina sura mpya
Someni historia.
Wazo la Stieglers power scheme zilianza zamani sana.
Miaka ya Mwalimu alidiriki kuanzisha mradi huo kwa kuanzisha RUBADA(Rufiji Basin Development Authority).
Hivyo haikuwa original idea ya Magufuli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…