mwanamabadiliko
JF-Expert Member
- Oct 30, 2010
- 938
- 1,540
Toka nchi hii uanze kutekeleza miradi ya Maendeleo ni muda mrefu na miradi mingi ya kimkakati imetekelezwa ,ikiwemo pamoja iliyotekelezwa na wakoloni mfano mradi wa Reli ya Kati.
Ukiachana na miradi iliyotekelezwa na wakoloni, nimejaribu kupima na kuangalia ukubwa na umuhimu wa miradi iliyowahi kutekelezwa nchini, kipindi nchi ikijiongoza yenyewe na c wakoloni.
Nimeangalia na kujiridhisha kwamba ni kweli miradi imefanyika mingi, ikiwemo Bomba la Gesi kutoka mtwara, Daraja la busisi, mradi wa Reli ya SGR, unaoendelea, Chuo cha UDOM.
Kutokana na sababu hapa chini pamoja impact na changamoto iliyotatua nadhani Mradi wa Stiglers George, uliotekelezwa na "MAGUFULI PEKE YAKE" ndio mradi Bora wa muda wote kuwahi kufanywa nchini na hivyo namuweka kuwa mradi wa Karne.
1. Mradi huu ulikuwa na Vikwazo vingi, kutoka watu wa Ndani Chadema baadhi na CCM baadhi, watu wa mazingira. Lakini pia MABEBERU USA, UMOJA WA ULAYA, serikali ya Ujerumani walipinga mradi huu Kwa nguvu , na kama asingekuwepo Magufuli mradi huu ungebaki kwenye makaratasi.
2. Mradi huu umekuwa mgumu pia kwasababu ya Gharama za utekelezaji wake, Mradi umegharimu Tsh Trilioni 6.5 + Variation (+40%) ambayo imehitaji uthubutu mkubwa kuutekeleza.
3. Katika miradi iliyoleta na itakayoleta impact kwenye maendeleo basi ni huu.
Kwanza Mgao wa Umeme Umekwisha japo tatizo la kukatika Umeme lipo kutokana na uchakavu wa miundombinu. Mradii huu unamwaga MW 940 kwenye Gridi ya Taifa na huku mashine 4 ziliwa zimeingia, Sasa nawaambia zikifika mashine 5, basi Stiglers itakuwa na uwezo wa kuhudumia nchi nzima peke yake.
Pili mradi huu unachochea miradi mingine mikubwa kama Mradi wa Migodini inayotumia Umeme mwingi sana, SGR, Bomba la Mafuta.
Namalizia kwakusema, Mradi wa Bwawa la Stiglers George utakaozalisha MW 2115, ndio mradi Bora wa muda wote kuwahi kutekelezwa na Watanzania wote wakiongozwa na Magufuli.