Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 5,352
- 15,876
Mradi huo umefadhiliwa na Mfuko wa Mazingira Duniani (GEF) kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP).
Akizungumza katika hafla hiyo, Mhe. Chana amesema mradi huo unalenga kuongeza ustahimilivu wa misitu dhidi ya athari za mabadiliko ya tabianchi kwa kuimarisha mifumo ya ulinzi, kusaidia shughuli rafiki kwa mazingira kama vile utalii, na kuimarisha mipaka, vituo vya ulinzi, pamoja na vifaa vya kukabiliana na majanga kama moto wa msituni.
Aidha, amesema mradi utasaidia jamii zinazozunguka misitu kwa kuwapatia shughuli mbadala za kiuchumi zitakazosaidia kupunguza utegemezi wa moja kwa moja kwenye misitu.
“Mradi huu wa miaka sita, kuanzia Septemba 2023 hadi 2029, unatekelezwa kwa ufadhili wa GEF na UNDP kwa gharama ya Dola za Kimarekani 5,837,010,” amesema Mhe. Chana.
Amesema mradi huo utatekelezwa katika misitu tisa ya hifadhi iliyoko kwenye mikoa mitano: Hassama Hills, Nou na Mlima Hanang (Manyara), Uzigua na Pugu–Kazimzumbwi (Pwani), Pindiro na Rondo (Lindi), Mwambesi (Ruvuma) na Essimingor (Arusha).
Aidha, Waziri amewapongeza wadau wa maendeleo na asasi za kiraia kwa mchango wao mkubwa katika juhudi za Serikali za kuhifadhi misitu, na kusisitiza umuhimu wa kuendeleza ushirikiano huo kwa manufaa ya taifa na vizazi vijavyo.
Kwa upande wake, Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Hassan Abbasi amesisitiza juu ya wananchi kutunza na kuhifadhi maliasili za misitu huku akitoa onyo kwa wanaokiuka taratibu za uhifadhi kuchukuliwa hatua kali.
Naye Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Shigeki Komatsubara amesema mradi huo ni muhimu kwa Tanzania kutokana na athari mbambali zinazoikumba misitu ikiwemo mabadiliko ya tabianchi, uchomaji moto hivyo utasaidia kuirisha maisha ya na vipato vya wananchi kwa kuacha kutegemea misitu.
Hafla hiyo imehudhuriwa na viongozi kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Wizara ya Fedha, TAMISEMI, wilaya ya Kisarawe, Wizara ya Maliasili na Utalii, TFS, pamoja na wadau wa maendeleo.