Mradi wa Julius Nyerere wakamilisha mtambo namba nane na kuingiza umeme kwenye Gridi ya taifa

Mradi wa Julius Nyerere wakamilisha mtambo namba nane na kuingiza umeme kwenye Gridi ya taifa

Pfizer

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2021
Posts
590
Reaction score
807
IMG-20240615-WA0020.jpg

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema tayari mtambo namba nane kutoka kwenye Mradi wa kufua umeme wa Julius Nyerere umekamilika na sasa unaingiza megawati 235 kwenye gridi ya taifa.

Dkt Biteko ametoa taarifa hiyo tarehe 14 juni 2024 wakati akizindua taarifa za utendaji katika Sekta ndogo ya Umeme, Gesi Asilia na Mafuta kwa mwaka 2022/2023 jijini Dodoma ambapo amesema kwa sasa Jumla ya megawati 470 zinazalishwa kutoka JNHPP na tayari zimeingizwa kwenye gridi ya taifa.

Kuhusu sekta binafsi amesema, “Sekta binafsi imetutoa kimasomaso, Serikali haiwezi kufanya kila kitu, wamefanya kazi kubwa mno kwenye mafuta, gesi na hata kwenye uzalishaji umeme, wito wangu kwenu msibaki nyuma changamkieni fursa, na kwa taasisi zilizo chini ya Wizara msione sekta binafsi kama watu wajanjawajanja, tuwape kipaumbele.” Amesema Dkt. Biteko

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba amesema kuwa katika tathmini iliyozinduliwa inaonesha Sekta ya Nishati imepiga hatua kwenye maeneo mengi ikiwemo uhakika wa upatikanaji umeme, upatikanaji na usambazaji wa mafuta kuimarika hasa baada ya Mhe. Dkt. Doto Biteko kuanza kuongoza Wizara ya Nishati.
IMG-20240615-WA0022.jpg

Ameongeza kuwa, taarifa ya Benki ya Dunia kwa nchi za Dunia ya Tatu zinazofadhiliwa na Benki hiyo inaonesha kuwa Sekta ya Nishati kwa Tanzania inafanya vizuri zaidi katika nchi zote zinazoendelea na Bara la Afrika kwa ujumla na hii ni matunda ya usimamizi madhubuti wa Mhe.Dkt. Doto Biteko ambapo eneo lililofanya vizuri zaidi ni usambazaji umeme vijijini na miradi mingine ya nishati kama JNHPP na mradi wa TAZA.

Ameongeza kuwa Benki ya Dunia imeidhinisha Dola.za Marekani milioni 300 ili ziendeleze sekta ya umeme kutokana na ufanisi huo wa Tanzania.

Akitoa taarifa za utendaji katika Sekta ya Nishati, Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Dkt. James Andilile alisema kuwa Sekta ya Nishati inaendelea kuimarika ikiwemo uwekezaji kwenye miundombinu ya umeme uwekezaji umeongezeka katika uzalishaji, usafirishaji na usambazaji, upotevu wa umeme unazidi kupungua na kubainisha wateja wa umeme wameongezeka kutoka milioni 3.8 mwaka 2021/22 hadi milioni 4.4 mwaka 2022/2023.
IMG-20240615-WA0021.jpg

Kwa upande wa changamoto zilizoainishwa kwenye taarifa hiyo katika sekta ya umeme ni uchakavu wa miundombinu ambao bado unaendelea kufanyiwa kazi kwa ukarabati wa miundombinu na uwekezaji endelevu.
 
ambapo amesema kwa sasa Jumla ya megawati 470 zinazalishwa kutoka JNHPP na tayari zimeingizwa kwenye gridi ya taifa.

MRADI WA UMEME WA JULIUS NYERERE RUFIJI JNHPP

Naibu Waziri wa Nishati, amesema kuwa utekelezaji wa mradi wa umeme wa Julius Nyerere (JNHPP) ukikamilika utazalisha umeme wa kiasi cha megawati 2,115

Hivyo June 2024 Bwawa la umeme la JNPP linazalisha 470MW sawa na asilimia 22 ya uwezo wa Bwawa la JNHPP :

470MW/2115MW ×100= 22%
 
Awali mtambo no 9 ulipokamilika tuliambiwa zimeongezeka megawati 235, leo zimeongezeka 235 hesabu inarudi kinyume nyume kuwa megawati zinazozalishwa kutoka bwawa hilo ni 470. Imekaaje hii.
 
470MW zaongezwa gridini
ilihali huku hakuna umeme tangu asubuhi
kama si laana ni nini

Megawatts 470 bado umeme mdogo sana, tusubiri uzalishaji wa bwawa la JNHPP Rufiji ukiwa unaingiza jumla ya Megawatts 2115 za umeme katika gridi ya taifa.
 
Awali mtambo no 9 ulipokamilika tuliambiwa zimeongezeka megawati 235, leo zimeongezeka 235 hesabu inarudi kinyume nyume kuwa megawati zinazozalishwa kutoka bwawa hilo ni 470. Imekaaje hii.

Necta ulipata division ngapi ?

Jibu la swali lako.

Mitambo imepewa namba kama majina vile. Hivyo inawashwa zamu zamu kwa jina la namba hiyo.

Mwanzo waliwasha jina namba 9. Sasa wamewasha jina namba 8.

Majina mengine bado hayajawashwa. Zamu yao haijafika.

Kila mtambo uwezo wake ni mw 235. Hivyo mpaka sasa imewashwa miwili tu ndio maana unaona 470 tu . Mingine 7 bado haijawashwa
 
Siku kitongoji changu kukipata umeme ndiyo siku nitaamini mambo haya... Kitongoji ni ndani ya km 3 yalipoakao makuu ya Wilaya hakina umeme hii ni aibu kubwa sana
 
Necta ulipata division ngapi ?

Jibu la swali lako.

Mitambo imepewa namba kama majina vile. Hivyo inawashwa zamu zamu kwa jina la namba hiyo.

Mwanzo waliwasha jina namba 9. Sasa wamewasha jina namba 8.

Majina mengine bado hayajawashwa. Zamu yao haijafika.

Kila mtambo uwezo wake ni mb 235. Hivyo mpaka sasa imewashwa miwili tu ndio maana unaona 470 tu . Mingine 7 bado haijawashwa
Baelezeye shogolaa. Kuna batu bengine buwezo wabo wa kuelewa mambo ni mdogo sana; tunamshukuru jukwaa kuwa na watu wavumilivu kama wewe wanaoweza kudadavua mambo kwa ufanisi kabisa ili hata habo bengine baelewe!
 
Back
Top Bottom