Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Habari mbaya kwa wachawi wote hata walio wahi ongoza hiyo wizara miezi nane iliyopita!View attachment 3018057
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema tayari mtambo namba nane kutoka kwenye Mradi wa kufua umeme wa Julius Nyerere umekamilika na sasa unaingiza megawati 235 kwenye gridi ya taifa.
Dkt Biteko ametoa taarifa hiyo tarehe 14 juni 2024 wakati akizindua taarifa za utendaji katika Sekta ndogo ya Umeme, Gesi Asilia na Mafuta kwa mwaka 2022/2023 jijini Dodoma ambapo amesema kwa sasa Jumla ya megawati 470 zinazalishwa kutoka JNHPP na tayari zimeingizwa kwenye gridi ya taifa.
Kuhusu sekta binafsi amesema, “Sekta binafsi imetutoa kimasomaso, Serikali haiwezi kufanya kila kitu, wamefanya kazi kubwa mno kwenye mafuta, gesi na hata kwenye uzalishaji umeme, wito wangu kwenu msibaki nyuma changamkieni fursa, na kwa taasisi zilizo chini ya Wizara msione sekta binafsi kama watu wajanjawajanja, tuwape kipaumbele.” Amesema Dkt. Biteko
Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba amesema kuwa katika tathmini iliyozinduliwa inaonesha Sekta ya Nishati imepiga hatua kwenye maeneo mengi ikiwemo uhakika wa upatikanaji umeme, upatikanaji na usambazaji wa mafuta kuimarika hasa baada ya Mhe. Dkt. Doto Biteko kuanza kuongoza Wizara ya Nishati.
View attachment 3018058
Ameongeza kuwa, taarifa ya Benki ya Dunia kwa nchi za Dunia ya Tatu zinazofadhiliwa na Benki hiyo inaonesha kuwa Sekta ya Nishati kwa Tanzania inafanya vizuri zaidi katika nchi zote zinazoendelea na Bara la Afrika kwa ujumla na hii ni matunda ya usimamizi madhubuti wa Mhe.Dkt. Doto Biteko ambapo eneo lililofanya vizuri zaidi ni usambazaji umeme vijijini na miradi mingine ya nishati kama JNHPP na mradi wa TAZA.
Ameongeza kuwa Benki ya Dunia imeidhinisha Dola.za Marekani milioni 300 ili ziendeleze sekta ya umeme kutokana na ufanisi huo wa Tanzania.
Akitoa taarifa za utendaji katika Sekta ya Nishati, Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Dkt. James Andilile alisema kuwa Sekta ya Nishati inaendelea kuimarika ikiwemo uwekezaji kwenye miundombinu ya umeme uwekezaji umeongezeka katika uzalishaji, usafirishaji na usambazaji, upotevu wa umeme unazidi kupungua na kubainisha wateja wa umeme wameongezeka kutoka milioni 3.8 mwaka 2021/22 hadi milioni 4.4 mwaka 2022/2023.
View attachment 3018056
Kwa upande wa changamoto zilizoainishwa kwenye taarifa hiyo katika sekta ya umeme ni uchakavu wa miundombinu ambao bado unaendelea kufanyiwa kazi kwa ukarabati wa miundombinu na uwekezaji endelevu.
Ana hoja huyu usimtukane we chawa wa watawalaNecta ulipata division ngapi ?
Jibu la swali lako.
Mitambo imepewa namba kama majina vile. Hivyo inawashwa zamu zamu kwa jina la namba hiyo.
Mwanzo waliwasha jina namba 9. Sasa wamewasha jina namba 8.
Majina mengine bado hayajawashwa. Zamu yao haijafika.
Kila mtambo uwezo wake ni mb 235. Hivyo mpaka sasa imewashwa miwili tu ndio maana unaona 470 tu . Mingine 7 bado haijawashwa
Wanacheza na hisia zako nini..! Lia machozi ya damu wakuelewe kwamba hujawahi mkubali JPM na ingawa huo ndio ukweli mlimpinga sana kwenye hili na sasa hamtaki tena kuelewa kwamba lilikuwa jambo zuri kwa nchiKipindi limesuasua mlisema Samia kafeli, likifanikiwa ndio sifa kwa JPM. Kama sio unafiki ni nini
SIMU yako Ina chaji maana yake umeme upo. Kukatika kwa muda ni jambo la kawaida!470MW zaongezwa gridini
ilihali huku hakuna umeme tangu asubuhi
kama si laana ni nini
235 (Namba 9) + 235 (Namba 8) = ?
Ova
Kumbuka jpm aliishia 23% tu. Mama amejenga zilizobaki. Sasa aliyejenga nani. Jpm hela ilikataView attachment 3018057
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema tayari mtambo namba nane kutoka kwenye Mradi wa kufua umeme wa Julius Nyerere umekamilika na sasa unaingiza megawati 235 kwenye gridi ya taifa.
Dkt Biteko ametoa taarifa hiyo tarehe 14 juni 2024 wakati akizindua taarifa za utendaji katika Sekta ndogo ya Umeme, Gesi Asilia na Mafuta kwa mwaka 2022/2023 jijini Dodoma ambapo amesema kwa sasa Jumla ya megawati 470 zinazalishwa kutoka JNHPP na tayari zimeingizwa kwenye gridi ya taifa.
Kuhusu sekta binafsi amesema, “Sekta binafsi imetutoa kimasomaso, Serikali haiwezi kufanya kila kitu, wamefanya kazi kubwa mno kwenye mafuta, gesi na hata kwenye uzalishaji umeme, wito wangu kwenu msibaki nyuma changamkieni fursa, na kwa taasisi zilizo chini ya Wizara msione sekta binafsi kama watu wajanjawajanja, tuwape kipaumbele.” Amesema Dkt. Biteko
Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba amesema kuwa katika tathmini iliyozinduliwa inaonesha Sekta ya Nishati imepiga hatua kwenye maeneo mengi ikiwemo uhakika wa upatikanaji umeme, upatikanaji na usambazaji wa mafuta kuimarika hasa baada ya Mhe. Dkt. Doto Biteko kuanza kuongoza Wizara ya Nishati.
View attachment 3018058
Ameongeza kuwa, taarifa ya Benki ya Dunia kwa nchi za Dunia ya Tatu zinazofadhiliwa na Benki hiyo inaonesha kuwa Sekta ya Nishati kwa Tanzania inafanya vizuri zaidi katika nchi zote zinazoendelea na Bara la Afrika kwa ujumla na hii ni matunda ya usimamizi madhubuti wa Mhe.Dkt. Doto Biteko ambapo eneo lililofanya vizuri zaidi ni usambazaji umeme vijijini na miradi mingine ya nishati kama JNHPP na mradi wa TAZA.
Ameongeza kuwa Benki ya Dunia imeidhinisha Dola.za Marekani milioni 300 ili ziendeleze sekta ya umeme kutokana na ufanisi huo wa Tanzania.
Akitoa taarifa za utendaji katika Sekta ya Nishati, Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Dkt. James Andilile alisema kuwa Sekta ya Nishati inaendelea kuimarika ikiwemo uwekezaji kwenye miundombinu ya umeme uwekezaji umeongezeka katika uzalishaji, usafirishaji na usambazaji, upotevu wa umeme unazidi kupungua na kubainisha wateja wa umeme wameongezeka kutoka milioni 3.8 mwaka 2021/22 hadi milioni 4.4 mwaka 2022/2023.
View attachment 3018056
Kwa upande wa changamoto zilizoainishwa kwenye taarifa hiyo katika sekta ya umeme ni uchakavu wa miundombinu ambao bado unaendelea kufanyiwa kazi kwa ukarabati wa miundombinu na uwekezaji endelevu.
Uneongea kitu dahihi kakaMAOFISA WA MWASILIANO / HABARI WAWE WAKWELI KTK TAARIFA ZAO KWA UMMA
Tanzania nchi ya ajabu katika kutoa taarifa, hutoa habari nusu nusu badala ya kusema katika mradi wa kuzalisha umeme bwawa la JNHPP RUFIJI kati ya vinu (turbines) tisa, hadi sasa wamefanikiwa kufunga na kuzalisha umeme katika vinu / turbine namba 9 na namba 8 tu huku vinu 7 bado kazi inaendelea kuvifunga ili kuongeza uzalishaji umeme kwenda gridi ya taifa.
Taarifa nusunusu za kisiasa zinaleta mtafaruku kwa kuwa uzalishaji unaonekana kwa mwananchi wa kawaida kama vile vinu vyote tisa sasa vinazalisha umeme wakati siyo kweli ni vinu viwili tu ndivyo vinazalisha.
Ukija kwa reli mpya SGR pia taarifa vinatolewa kisiasa kama vile sasa mradi wote wa SGR umekamilika kumbe ni kipande cha Morogoro na kinasafirisha abiria tu.
Maofisa habari wa taasisi za umma na wizara wajifunze kutoa taarifa sahihi, kamilifu na zinazotoa picha halisi ya miradi ilipofikia.
Uneongea kitu dahihi kaka
Ila wa tz wengi ni wa.....
Kwanza hawajiulizi
hawapambanui
Hawaghabui
Wanapenda story kuzidi uharisia
Siass imeshika hatam
Tumbo ndio kitu cha kwanza na sio nchi
Kila mtu anaweza jinsi ya kuendelea kula na sio kunufaika kwa taifa hili
Negative negative negative tu470MW zaongezwa gridini
ilihali huku hakuna umeme tangu asubuhi
kama si laana ni nini
We zoea tu sisi ni wanafiq mnooooAcheni unafiki, kipindi bwawa limesuasua mlisema mama hawezi kamilisha mradi. Mmeona amefanikiwa ndio sifa mnataka za JPM.